MPs Kigwangalla, Gekul Vs Waziri Mwinyi juu ya MGOMO WA MADAKTARI ndani ya Tuongee Asubui ya Star TV

Let me tell you being a president or member of parliament doesn't mean you have done something in a country by your title.

What we citizen measures are responsibility and accountability. Sasa nakushangaa mh unamuuliza mtoa mada cheo, unadhani cheo chake kitasaidia kuendesha nchi? Au wewe umefanya nini katika cheo chako kusukuma nchi, ungemuuliza katika kada yake anafanya nini kuisaidia nchi kimaendeleo ningekuona mstaarabu kama unavyohitaji watu wawe na sio personal attack kwa irrelevant issues.

Hujawahi kujiuliza ni kwanini uliacha kuingia wodini ukaenda kwenye political medicine na mwisho kubadili kabisa taswira au kwanini uliingia MD at first place ukapoteza miaka 5 kama lengo lilikuwa kuwa na MBA?

Kuna Prof mmoja aliwahi kusema, "usione watu wanakimbia kutibu wagonjwa na kuenda kwenye political medicine ambayo hata ukimpa diwani mwongozo anaweza kuact, ni vile tu hajiamini katika kutoa huduma na hawezi kujenga rapport na wagonjwa ili hata akianzisha hosp yake au akienda kuomba kazi ya part time aweze kuwavuna"

Nakushukuru Daktari, kijana anatakiwa awe responsible in the first place kabla hajawataka wengine wawe responsible, usinipeleke huko, siyo lengo langu
 
Hivi wewe imara uliwahi kufanya nini kwa nchi hii? Mwinyi aliwahi kuwa Rais, wewe umewahi kuwa nani? Acheni kejeli na matusi kwa wazee kama Mwinyi jamani...hivi hamuwezi kuongea na kujenga hoja zenu hata kama ni za kupinga bila kutoa matusi kwa viongozi? Usomi unafundisha uvumilivu na ustaarabu kwenye mawazo yaliyo kinyume na yako, unless kama hajuenda shule labda nitakuelewa hapo! Lakini kama unafanya maksudi basi haipendezi

Nakubaliana nawe kwa sehemu, lakini wewe nawe ni DHAIFU katika kusimamia mambo ya msingi. Ukitishwa na magamba wenzio unafyata mkia kama mb.a koko.
 
Naona kila mmoja anatetea ulaji wake huku wagonjwa wanateseka kwa kukosa huduma bora mi nilidhani madaktari humu wanagombea kuhudumia wagonjwa wao zaidi.!!!!!!!
 
Kesho asubuhi kuanzia saa moja kamili asubuhi wabunge wawili wa kamati ya kudumu ya bunge ya huduma za jamii, mh Dkt Hamis Kigwangalla (CCM) na Mh Dkt Hussein Ali Mwinyi ambaye ni mb na waziri wa afya kwenye serikali ya jamhuri ya muungano wa tanzania watakuwa kwenye kipindi cha tuongee asubuhi kinachorushwa na kituo cha Star TV kutokea bungeni dodoma wakijadili sakata la mgomo wa madaktari. kila jumanne, star TV hurusha topic inayohusiana na mambo ya afya ya jamii. kipindi hiki huwa ni laivu na hivyo watazamaji mnaweza kuuliza maswali na kutoa michango yenu moja kwa moja

Kama atakuwa Dr Kigwangallah yule ninayemjua mimi, ambaye pamoja naye mwaka 2005/06 Dr Mwinyi alitudanganya pale ukumbi wa Korea tulipogoma....basi atamchana chana Dr Mwinyi am'malize! Go Kigwa...
 
Nimeona chini umesign elimu yako, sina uhakika ulisomea wapi MD yako au MPH ila naomba ukiwa na huyo waziri wako hiyo kesho mwambie afute kauli ya kuwa wanaafunzi wate wa MD wanapata grant ya serikali.......ataje chuo kimoja ambacho serikali inafanya hivyo na ktk vyuo binafsi huwa inalipia wanafunzi wangapi. Nasikitika kuwa waziri amekuwa irresponsible kiasi hicho na kupotosha umma kwa kusikiliza maneno ya vijiweni bila kuhakikisha, kwanini ukubali madaraka ilihali hata hamjui mnapopaomgoza wala hutaki kujifunza? Imagine kwasasa kwa wazazi ambao wamemuamini huyu waziri mahusiano yao na watoto wao yapoje? Atoe tofauti ya chou cha udaktari cha serikali na vyuo vya binafsi. Pia tofauti ya grant na mkopo, ambayo vyote katika vyuo vya binafsi havitoshelezi na wazazi wa wanafunzi hao wamekuwa wakichangia (top up).

Sina hakika kama huyu Kigwangala (aka Hamis Bagaile) anajua tofauti ya GRANT na LOAN kwa tafsiri ya serikali ya ccm. Tarajia blah blah.
 
Hivi wewe imara uliwahi kufanya nini kwa nchi hii? Mwinyi aliwahi kuwa Rais, wewe umewahi kuwa nani? Acheni kejeli na matusi kwa wazee kama Mwinyi jamani...hivi hamuwezi kuongea na kujenga hoja zenu hata kama ni za kupinga bila kutoa matusi kwa viongozi? Usomi unafundisha uvumilivu na ustaarabu kwenye mawazo yaliyo kinyume na yako, unless kama hajuenda shule labda nitakuelewa hapo! Lakini kama unafanya maksudi basi haipendezi

Katika wanasiasa wa nchi hii, namheshimu Mwalimu Nyerere, Kawawa na wenzao. Hao ndiyo pekee yao walitoa mchango mkubwa, na walikuwa tayari kuacha kazi zao za mshahara na kuamua kuwa wabangaizaji ili kuifanya Tanzania iwe huru kwa matarajio kuwa baada ya uhuru wananchi wote wangepata maendeleo.

Wanasiasa wa leo wa Tanzania hasa kupitia CCM, sio tu hawana mchango kwenye ujenzi wa Taifa, bali wamekuwa ni hasara kwa Taifa. Ukipima faida yao kwa Taifa, ni aheri ya vijana wanaokaa vijiweni bila kufanya kazi, maana wale hawazalishi na hawaibi, lakini wanasiasa wa CCM hawazalishi na badala yake wanaiba.

Upeo mdogo wa Kigwangala unaonekana anapofikiria kuwa na cheo cha kisiasa kama Rais, Waziri, mbunge, n.k. basi ni mchango chanya kwa Taifa. Kuna wanasiasa wengi tu Duniani ambao wamekuwa ni majanga katika nchi zao kiasi cha wananchi wao kufikiria kuwa aheri watu hao wasingelizaliwa kabisa. Kama hii serikali yetu ya ulaji ya CCM utasema ina mchango kwa Taifa au ni hasara kwa Taifa? Kama nafasi yako ya ubunge wa kupewa na chama utasema ina faida kwa wana-Nzega au ni hasara kwao? Hao wabunge wa CCM waliojaa bungeni kwa kutumia rushwa na hadaa kuna mchango wowote chanya kwa Taifa? Mchango mkubwa kwa Taifa tunaouona kutoka uongozi wa CCM ni mchango hasi, yaani wizi, ufisadi na ubadhirifu, mbaya zaidi wizi huu ni wa kimfumo na unasimamiwa na dola. Katika uhalisia, mimi nina mchango mkubwa katika Taifa hili kwa vile ninalipa zaidi ya shilingi milioni 4 kwa serikali kila mwezi kuliko wewe unayekula kodi yangu na ya Watanzania wengine halafu unaenda kusinzia au kupiga kelele za Ndiyoooo, bungeni. Shame on you people who have and continue to be deleterious to our loved nation.

Na hao Star TV ili kuleta heshima kwa television yao wawe wanatafuta watu wanaoeleweka misimamo yao kushiriki katika mijadala. Huyu Kigwangala si ndege si mnyama, leo anaunga mkono hiki kesho anapinga hicho hicho alichokuwa amekipinga, anatupotezea muda.
 
  • Thanks
Reactions: SMU
kwa nini unakuwa mvivu wa kufikiri mkuu??huoni kuwa unajidhalilisha na kujitia aibu mbele ya wanajukwaa???

Mimi nadhani wewe ndio unajidhalilisha ni kweli MWINYI waziri hana jipya kama baba ake kwani baba ake alifanya nini zaidi ya kuuza LOLIONDO kwa waarabu walioingia ubia na mke wake mama SITI alishindwa kujenga barabara ata ya KM 20 sasa huyo kama si DHAIFU ni nani hivi unatetea upuuzi una data au ni mahaba tu kwa wanaume wenzio acha kupenda kiasi icho wewe mtoto wa kiume utaishia kubaya shauri yako.
 
Mkuu, unapaswa kumwomba radhi mzee Mwinyi maana umemtumbukiza tu kwenye hii thread wakati yeye wala hahusiki. Anayezungumzwa hapa Husein Mwinyi, siyo mzee Mwinyi. Kama ungetaka kutueleza juu ya udhaifu wa mzee mwinyi basi ungeleta thread yako ukielezea kwa ufasaha jinsi unavyouona udhaifu wake na wanajamvi wangechangia kwa mtazamo huo. Zungumza habari ya Mwinyi aliyetajwa, siyo yeyote tu anayekuja kichwani.



Kweli kabisa mkuu. Mzee Mwinyi ahusiki kabisa katika thread hhi. Nikuumuonea tu
 
wewe umeifanyia nini nchi hii

Alionyesha unafiki kwa kuandamana juzi eti kwa ajili ya mambo ya migodi, pia alijifanya kuipinga bajeti lkn akiwa kichochorono hakudhubutu kuipinga hadharani, ni mnafiki mzuri sana asiyesimamia anachoamini na anayesimamia asichokiamini, ni magamba wale wale na Dawa yake iko jikoni mwaka 2015 harudi ddm, vijana wa huku tumeshaanza kujipanga!!!!! HICHO NDIO ALICHOKIFANYIA NCHI YETU!!!!!
 
Mi binafsi, naona kumwingiza mzee mwinyi kwenye thread hii ni kumwonea. Hapa hoja ni dr.mwinyi na sio mzee mwinyi. Labda mtoa hoja angeanzisha thread yake aelezee udhaifu wa mzee mwinyi watu waje wachangie mada.
 
Ni kweli utawala wa baba yake ulikua dhaifu,hata yeye ni dhaifu. Sifa nzuri ya mzee Mwinyi ni uungwana na ustaarabu wake!

Kwa wale wenye kumbukumbu, Mzee Alli Hassan Mwinyi ndiye aliyeanzisha sera ya kuruhusu watu wenye uwezo kuagiza vitu toka nchi za nje na ndio maana anaitwa MZEE RUKSA!! Bila huyu Mzee kuruhusu uagizaji toka nchi za nje,sasa hivi nchi hii isingekuwa na amani hata kidogo kwani hali ya maisha ilikuwa mbaya sana na bila shaka wanajeshi wangeipindua serikali!! Hatuna budi kumshukuru na kumuenzi kwa busara zake.
 
Hivi wewe imara uliwahi kufanya nini kwa nchi hii? Mwinyi aliwahi kuwa Rais, wewe umewahi kuwa nani? Acheni kejeli na matusi kwa wazee kama Mwinyi jamani...hivi hamuwezi kuongea na kujenga hoja zenu hata kama ni za kupinga bila kutoa matusi kwa viongozi? Usomi unafundisha uvumilivu na ustaarabu kwenye mawazo yaliyo kinyume na yako, unless kama hajuenda shule labda nitakuelewa hapo! Lakini kama unafanya maksudi basi haipendezi

Kigwangala, unatakiwa ufike mahali pia ujue kuwa kujitokeza kwako mara kwa mara kwenye media kumefanya wengi tujue ulivyodhaifu. Unajitahidi kutafuta umaarufu kupitia media bila kujua kuwa wanaosikiliza na kufuatilia vinavyoongewa wengi huwa wako makini. Jitahidi kujipanga vizuri
 
nasikia kama ni dhaifu ujitahidi kukaa kwenye ndege si chini ya saa 150 kwa mwaka unakuwa imara.
 
Hivi wewe imara uliwahi kufanya nini kwa nchi hii? Mwinyi aliwahi kuwa Rais, wewe umewahi kuwa nani? Acheni kejeli na matusi kwa wazee kama Mwinyi jamani...hivi hamuwezi kuongea na kujenga hoja zenu hata kama ni za kupinga bila kutoa matusi kwa viongozi? Usomi unafundisha uvumilivu na ustaarabu kwenye mawazo yaliyo kinyume na yako, unless kama hajuenda shule labda nitakuelewa hapo! Lakini kama unafanya maksudi basi haipendezi
Labda na wewe utueleze umefanya nini kwa nchi yako,nadhania hamna la maana ulilolifanya.La maana ulilolifanya ni kukimbia fani yako,ndio maana ukachukua MBA badala ya surgery,peadiat,obst...Yote hayo hauna mapenzi ya dhati
kwa wagonjwa.Sasa mtu kama wewe uliyekimbia fani yako kesho utaongea nini zaidi ya unafiki.Nakushauri nenda kasome
MMED,na urudi muhimbili kwenye fani yako.
 
Mh H.Kigwangala Dr Mbunge wa Nzega nimekuona Star tv hakuna ulichoongea ila kutuambia utaikwamisha Bajeti ya Wizara ya Afya
Nasikitika ww upo nyuma ya Madaktari wa Muhimbili na sio ma Medical Assistant wa Nzega, Puge Bukene Mwanhala nk ambao pamoja bba mabibi Afya, Maendeleo ya Jamii manesi wa JWTZ na Polisi hawamo hata kwenye calling au night waongezewe posho nyie mnataka na wenzenu tu mpate kuanzia 3.5m
Mkumbuke Sarungi alikuwa anavua ubunge anaenda tibu wagonjwa Emergency lakini nawaapia waTZ wote ww Mh huwezi kwa sababu upo nyuma yao wagome
Hivi hizo nyongeza za MaDr tu karibu Bilioni 18 kwa mwaka zitatoka wapi? Mgodi wa Nzega? Bulyankulu? Au Vodacom? Je za Manesi je za Polisi
Baba yangu mzazi alikuwa Dr Nzega Govt Hosp lakini wote hamfundishwi Budget ila asprin na Moyo ili usimame ni kugoma mgomo.
NASIKITIKA NI wATANZANIA WACHACHE wanaona matokeo ya mgomo huo ni kupandisha ada ya kujiandikisha Mahospitalini itafikia 100,000/ nado kulazwa au dawa
Mwisho Mh DR Kigwangala Wizara ya Fedha wameshasoma makadirio yao usiipinge km wenzio wasiojua watapata wapi hela hiyo au mtatupandishia ada Mahospitalini ujue na walimu watafuata, Walinzi mipakani nao watafuata
Napinga mgomo wa MaDr mpaka mtakaposema mtazipata wapi wakati viDispensary vya Abbortion ambavyo mbbavyo
Nashauri wasiotaka wasaini OFF watakuja wengine
 
FRESH NEWS: UKWELI KUHUSU MGOMO WA MADAKTARI.
Leo ningependa turudijamvini kujadili kidogo kuhusu huu mgomo wetu, awali katika sehemu ya kwanza yamada hii, nilijaribu kuainisha madaiyetu, makubaliano na kuacha kwako mwanya wa kufikiri utendaji wa serikali yetu"SIKIVU" ilivyo na inavyofanya hadi sasa (kamahukubahatika kusoma hebu itafute facebook na Jamii forum ili upitishe machoKIDOGO TU ikiwa na thread title UKWELI KUHUSU MGOMO WA MADAKTARI)..leonilifikiri si vibaya tukijadili kuhusu madhara ya mgomo huu.
HALI HALISI HOSPITALINI:
Hospitali ya Taifa Muhimbili, Ocean Road Institute, Temeke,Mwananyamala, Amana, Bugando, Mbeya, KCMC, ST.Francis, Haydom, Dodoma n.k. huku kote hakuna kinachoendelea..madakatarikwa maana ya General practitioner na Specialist, sio Assistant Medical Officer,AMO(KWANI KUNA UTOFAUTI KATI YA NGAZI ZAUDAKTARI KUTOKANA NA KISOMO/ELIMU-nisingependa kwenda katika hili) .. Hii ni TOTAL TOOLS DOWN,(TTD), episode III..
Kama tulivyosema awali hatudai posho, na ongezeko la mishaharatu(hii si priority hata katika madai), ila eti kulingana na majibu ya serikali,tutegemee madai hayo katika next next fiscal year(2013/2014) lakini hebu jiulize
1. Madai ya madaktari yalianza lini?
2. Madiwani waligoma ama kudai mshahara/posho lini??!
3. Priority ya Taifa ni wananchi(kupitia madai ya madaktari) au viongozi(kupitia poshompya za madiwani zilizotangazwa Bungeni)?
4. Nyongeza ya posho ya madiwani imetokea wapi?? ilipangwakatika bajeti?
5. Viongozi au wananchi hamuoni haya??

SISEMI TUNAHITAJI MISHAHARA YETU ILINGANE NA WABUNGE, MAWAZIRI, WAFANYAKAZI WATRA, BOT, n.k..LA HASHA!! ILA UNAPODAI MAZINGIRA BORA YA KAZI, NYONGEZA YAMSHAHARA,POSHO NA UNAPEWA MAJIBU YA DHARAU,.. NA WENGINE KAMA VIONGOZIKUJIONGEZEA(duringthe same period of our claims), HAPO NDIPO COMPARISON INAPOTOKEA, NAKULAZIMISHA TUFANANE NA NYIE!!
Katika hospitali tajwa hapo juu, Wakurugenzi, wakuu wa idarawamekuwa wakifanya vikao na kulipwa 50,000/=TSHS@SIKU toka mgomo kuanza23.06.2012.., Je, wananchi mnayajua haya? Jiulize kuna idara ngapi katikahospitali hizi? Nani anayetoa pesa hizi? Zitatoka hadi lini? Lengo kuu nikushawishi, kushurutisha madaktari turudi kazini… !!

VYOMBO VYA HABARI:
Katika "episode" mbili za "series" yetu hii ya Mgomo waMadaktari, vyombo vya habari vilianza kuripoti kuwa hakuna migomo, hadi palewatu wa HAKI ZA BINADAMU walipoingilia kati!!
Nasikititishwa sana na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC),kutotoa taarifa halisi wakati watu wanazidi kupoteza maisha, kweli hawaoni? Hawajuiau wanapuuzia?
Halafu mnatuitamadaktari si wazalendo? KWELI?? Napata shida sana kuelewa inakuwaje watanzaniawanaumia na viongozi kutotilia maanani madai yetu, ni kweli uhai wa mtuhauwekwi rehani lakini hatukuingiakatika mgomo huu kwa kuweka maisha ya watanzania wenzetu katika mizani, na ndiomaana muda wa mazungumzo ulikuwepo nahata kabla ya mgomo, muda wa wiki mbili ulitosha kujipanga, kwamba kama Serikaliikishindwa kutekeleza madai, AU kuonyesha njia mbadala ya kuyatatua basiijipange kuhudumia wananchi.
Kama leo hii tunaangalia luninga(TV-mfano Mh. W/Afya paleStar TV kukimbia), tunasikiliza redio lakini mambo yanayofanya na serikali nihaya, umekwisha jiuliza ingekuwaje, ama Serikali yetu ingetutendea nini kamatungekuwa hatuwaoni wanachofanya pale Bungeni(Mfano Takwimu za uongo), nakwingineko? Hali hii itaendelea hadi lini?
MKAKATI:
Usalama wa taifa wako kila hospitali, swali ni hili
1. Ni usalama wa Taifa au wa chama tawala?
2. Wanatumia pesa ya nani?
3. Last‘episode" walileta wanajeshi,
KAMA MADAI YAMADAKTARI SI YA MSINGI NA SERIKALI IKOSAHIHI KWANINI WANAJESHI HAWAJATOA HUDUMA KAMA WALIVYOTOA HAPO MWANZO??
KWANINI HAWAKUWA TAYARI HATA WALIPOOMBWA KUFANYA KAZIMNAYYOIITA KAZI YA WITO????

MAKOLIGI (colleague)??
Ni lini wananchi waliingia mkataba na sisi juu ya afyazao??sasa mbona wanatulalamikia na kutushambulia??..nadhani wananchi mnakoseakidogo, dhamana ya afya zenu ni kwa hiyo serikali "sikivu", hivyo lawama, maombi, na hisia zotepelekeni huko….ila sisi kurudi ni hadi pale madai yataposikilizwa, this time sikwenda kazini halafu yafanyiwe kazi? HAPANA..HII IELEWEKEVIZURI..HATUDANGANYIKI… hadi yafanyiwe kazi na kuthibitishwa au njia mbadala.
Najua wanasema when you get in a fight you should dig, twograves but I guess you should not fightwith someone who has NOTHING to loose,..We either overestimated the power of Government's responsibility orThey(Government) underestimated our power, and I really doubt of the latter because they KNOW they cant stopus.. you cant stop what you cant catch,because the more they will push us the worse this is going to get…
..Solidarityforever..
 
Mh. Kigwangalla
Mahojiano yako Star Tv yamesaidia nini katika kutatua mgomo wa madaktari? Kumbuka upo kwenye chombo chenye kutunga sheria ambacho kimegeuzwa kama rubber stamp; kama bunge lenu lingekuwa ni bunge makini nina uhakika mgomo huu usingetokea; tatizo wapiga porojo ni wengi ndio sababu mnakimbilia maandamano na kwenye Tv; mimi nilitegemea ukiwa kama daktari ungejitolea kwenda kutibu wagonjwa angalau kina mama na watoto na kama mbunge ungewasilisha mswaada binafsi wa kuishinikiza serikali kutekeleza madai ya madaktari; huo ndio uzalendo; mlisimama kidete kupigania posho hili la madakatari kuitaka serikali iboreshe huduma nalo limekuwa gumu kwenu au kwasababu nyie waheshimiwa matibabu yenu ini India na South Africa? Mh. Kigwangalla ni ukweli upi unao usimamia?

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
Back
Top Bottom