Mporogomyi adaiwa kugonga mtu na kuua; kufikishwa mahakamani

Luteni

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
2,274
301
MBUNGE wa Kasulu Magharibi, Kilontsi Mporogomyi (CCM), leo anatarajiwa kupandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya Dodoma kwa tuhuma za kusababisha kifo baada ya kumgonga mtembea kwa miguu na gari lake hadi kufa.

Mbunge huyo, ambaye alikuwa akiendesha mwenyewe, anadaiwa kumgonga mtu mwenye jinsia ya kiume ambaye jina lake halikupatikana mara moja anakadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 28 na 30.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Zelothe Steven, aliiambia Tanzania Daima ofisini kwake mjini hapa jana, kuwa ajali hiyo ilitokea usiku wa kuamkia jana, majira ya saa 5:30 usiku katika eneo la Wajenzi mjini hapa.

Alisema, mbunge huyo alikuwa akiendesha gari aina ya Toyota Land Cruiser lenye namba za usajili, T 288 ASJ, ambapo alimgonga mtu na kumsababishia mauti papo hapo kutokana na majeraha makubwa aliyoyapata sehemu mbalimbali za mwili.
 
kumbe ni ajali...! poleni wahusika wote wa ajali hiyo......na shame kwa wale watafutao umaarufu kwa matatizo ya wengine
 
Ajali inaweza kusababishwa na mtu yeyote na inaweza pia kumkumba mtu yeyote, kuwa mbunge kusiwe sababu ya kumfanya alaumiwe. Tuangalie ni jinsi gani utaratibu utafuatwa baada ya kufikishwa kwenye mikono ya sheria, otherwise ni ajali tu.
 
Ajali inaweza kusababishwa na uzembe, kwa mfano kuendesha kwa mwendo kasi sehemu ya makazi, kuendesha ukiwa umelewa na vipimo vya polisi kuonyesha hivyo nk. Hapo kesi inaweza kubadilika. Pole mbunge na wafia
 
Pole zake MH na walofiwa, japo nadhani Mhe ana bahati mbaya, kwani alikuwa na kesi kama hii huko miaka michache iliyopita kama sikosei Pwani !
 
Back
Top Bottom