Mpongeze, mshukuru na kumwambia maneno yenye hamasa mpenzi wako

Mtayarishaji

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
291
199
Unaweza ukawa unafanya mambo mengi mema kwa mpenzi wako lakini anaangalia na kunyamaza akifahamu ndani yake kwamba ni wajibu wako kufanya vile.

Wapo baadhi ya watu wenye kiu na maneno ya kupongezwa, kushukuriwa au ya kuhamasisha. Kwa mfano, mwenzako amekusaidia kuanua nguo zako nje, akimaliza au unapogundua nguo zimetolewa na lilikuwa jukumu lako kuzitoa, usione ugumu wa kumwambia mpenzi asante kwa kunisaidia kuanua nguo.

Anaweza akaamua kumlisha mtoto wewe ukiwa unafanya mambo mengine, usichukulie kirahisi tu kwamba na yeye si mzazi lazima amlishe mtoto pia, hapana, mwambie mpenzi nakushukuru umenisaidia kumlisha mtoto na mimi nikaweza kufanya hiki na kile.

Akipendeza mwambie umependeza, nguo hiyo inakutoa vyema sana, akifanya kitu hata kama ni kidogo mpongeze na kumwambia unatambua mchango wake mzuri. Wako wenye kiu kubwa na maneno haya na kwao wasipoyasikia ni kama vile hawajapendwa kabisa na unaposema neno hili kwake unanyanyua kitu kikubwa sana ndani yake.

Ni vyema ukafahamu kama mpenzi wako ni mwenye lugha hii ya mapenzi na ukifahamu basi usimnyime chakula cha nafsi yake. Mpongeze, mshukuru na kumwambia maneno yenye hamasa yatakayomshibisha.
 
Last edited:
Umenikumbusha kisa fulani kwa jimama langu.
Niliamua kumpeda na kukubali familia yake hasa mtoto wake.. hivyo niliwajali kama familia na kuwapenda.... nilihakikisha mtoto anakuwa vizuri kimasomo na mambo mengine
Itatokea tukahitiliafiana... yeye aliona kama sitimizi wajibu hivyo nikamwambia nini nimefanya kama sehem ya wajibu wangu... baada ya mda akaniita sehem akaniambie hiyo ni sehem ya wajibu wako... ndio maana hakuona kama nimefanya kitu
 
Pole.

Hiyo ni changamoto sio kwa huyo pekee ni kwa wanawake wengi.
 
  • Thanks
Reactions: lup
Back
Top Bottom