Mpishano wa miaka kati ya mme na mke kwenye swala la uowaji na uolewaji

nikubhilikile uje

JF-Expert Member
Jun 26, 2016
264
250
Salama ndugu zanguni.

Mimi sijaoa ila nimejaribu kujiuliza sana kati ya mke na Mme wawe wamepishana miaka mingapi? Kwani nimejalibu kufanya uchunguzi kwa wazazi wangu na Ndugu zangu nimegundua kuwa kunampishano mkubwa wa kiumri katika ndoa zao na hicho kinawezekana kuwa ni sababu ya kudumu na kueshimiana katika ndoa zao na kuzeeka katika hali inayoendana.


Ni kirejea katika ndoa za Siku izi unakuta wanandoa kiumri wamepisha miezi au miaka michache sana na hiki kinaweza kuwa tatizo la ndoa nyingi kuvunjika au kutokuwepo na heshima katika ndoa?

JE? Katika kuoa inatakiwa mpishane kiumri miaka mingapi? Ili mwendane na mwenzako, naombeni tushare hili swala
 

Perfectz

JF-Expert Member
May 17, 2017
6,677
2,000
SIDHANI KAMA KUNA UPISHANO SAHIHI WA UMRI KATIKA MAPENZ AU NDOA.CHA MUHIMU PAPUCHI NA DYUDYU VILIDHIANE
 

Big5

Member
Sep 25, 2014
34
95
Kupishana miaka mingapi kwenye ndoa siyo sababu ya wanandoa kudumu na kuheshimiana,kwani kuna ambao wana umri sawa lakini ndoa bado zinadumu. Sababu ni mliependana kweli au mlitamaniana? Fahamu kuwa ndoa ni kuvumiliana kwan kila mmoja anakuwa na malezi aliyokulia
 

nikubhilikile uje

JF-Expert Member
Jun 26, 2016
264
250
Ila swala la kupisha miaka kuanzia 5 kuendelea linafaa kwanini wenzetu wa ke jinsi walivyo miili yao nitofauti na miili yetu ya me
 

cocochanel

JF-Expert Member
Oct 6, 2007
24,459
2,000
Hayo ya umri yaache kabisa kuyafikiria.

Wewe sali tu yaani sali upate mtu mwema kwako bila kujisumbua kichwa sana, mtakayeendeana na kuwa pamoja hadi kifo kiwatenganishe.
 

Ushimen

JF-Expert Member
Oct 24, 2012
25,858
2,000
Sasa kama wewe umefanya uchunguzi tayari kwa ndugu pamoja na wazazi wako, na ukatuletea majibu ya research yako hapa.
Sisi ulitaka tukushauri nini bila research....
 

sab

JF-Expert Member
Jan 25, 2013
5,738
2,000
Hakuna specific namba ya miaka kati ya muowaji na muolewaji, isipo kiwa tu mwanaume akiwa na umri mkubwa zaidi ya mwanaumke inafaa sana kuliko mwanamke kuwa na umri mkubwa kuliko mwanaume,

Ki halisia mwanamke anakuwa haraka ki mwili na kiakili tofauti na mwanaume hukuwa taratibu sana , ndio maana wale wote walio owa wanawake walio lingana nao umri mwisho wa siku mwanaume anabakia kijana mwanamke amesha kongoloka,

Hivyo mwanaume akiwa na umri mkubwa alafu mwanamke akiwa na umri mdogo basi utakuwa wanazeeka pamoja japo mwanamke umri wake unakuwa mdogo lakini anakuwa kimwili na kiakili mwishowe kongolo wote
 

bbade

JF-Expert Member
Mar 15, 2013
6,676
2,000
Nachoweza kufikiria kwa juu juu, ni kwamba. ....wazazi wetu au kipindi cha huko nyuma wanaume walikuwa wanaoa baada ya kupata kazi. ...na wengi wao walipendelea kuoa mwanamke aliye chini yake kimaendeleo. ..kwahiyo unakuta mke lazima awe mdogo. (anakuwa bado anasoma au atasitisha masomo aolewe wahamie mjini)

Sababu ya ndoa zao kudumu....kuna uwezekano wanawake walikuwa wanavumilia mengi ili kulinda ndoa,nawasilete aibu kwenye Familia...akizingatia yeye na familia yake(upande wa mke) inamtegemea mumewe.

Ukifuatilia ndoa za miaka ya sasa.....
wengi wasomi na uchumi unasababisha watu waoane wakiwa tayari wamesha jiendeleza kimaisha ili kusaidiana majukumu. Mwanamme anataka kuoa mdada mwenye kazi yake. ... (kiumri hawawezi kutofautiana sana)

Hali tegemezi haipo kama zamani, mwanamke wa sasa haoini Sababu yakuvumilia mateso angali anaweza kujitunza yeye na familia yake bila kutegemea mumewe.

Mnisamehe kama nimetoka nje ya mada. .....
 

harder king

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
3,593
2,000
Mkuu kupishana kiumri au kulingana ainaga tatizo kiumri.
Tatizo litakuja kama mnapishana kiakili/kimawazo
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom