Mpira wa adhabu ndani ya 18 (freekick inside penalty box)

IAmShedeOne

JF-Expert Member
Jul 2, 2015
202
382
Mchezaji akifanyiwa madhambi (foul) ndani ya eneo la hatari (penalty box) kinachofata ni mpira wa adhabu ambao hujulikana kama mkwaju wa penati, lakini ulishawahi kujiuliza kuhusu hii (kwenye video).

Kuna hii inaitwa Indirect Free Kick (IFK) mpira wa adhabu usio wa moja kwa moja yaani penati!. Kama Refa ameona, ikiwa kuna ukiukwaji dhidi ya kipa:

Kipa kudaka mpira uliopigwa kwa mguu au kurushwa kutoka kwa mwenzake (wa timu moja)

Kipa kushikilia mpira kwa muda mrefu sana (muda mrefu zaidi ya sekunde 6) bila mpira kugusa ardhi baada ya kudaka.Rejea baadhi ya mechi huwalazimu makipa kuudundisha mpira chini kuepuka adhabu hii.

Kipa kudaka mpira mara mbili, yaani baada ya kudaka na kuuachia mpira chini kisha kudaka tena kabla ya mchezaji mwingine yeyote kuugusa mpira.

Kutokea kwa makosa hayo matatu ni IFK.

Kuna faulo mbili za wachezaji wa uwanjani ambazo zitasababisha IFK kwa timu inayoshambulia katika eneo la Adhabu (au mahali popote uwanjani):

Kumzuia mpinzani kucheza mpira bila mawasiliano yoyote (filimbi ya refa)

kumshutumu, kupinga maamuzi au kutoa lugha chafu au alama chafu kwa mpinzani pia husababisha IFK


Ally Maulid Kanungu
30th June 2021
 
Back
Top Bottom