Mpina ataka kumuumbua Waziri Mwigulu bungeni, apatwa na kigugumizi, Spika ambana "mi sielewi"

Rais angekuwa anajua watanzania wanataka nini, hivi leo mwigulu asingeendelea kukalia kiti cha waziri wa fedha. Na rais kuendelea kushupaza shingo kwa ajili ya mwigulu anajipunguzia ushawishi kwa watanzania, sema hili la kupungua ushawishi chawa hawata mwambia, maana kazi yao kubwa ni mapambio. Maana hata malkia akiwa utupu wao haiwahusu. Ila kwa nia njema tu, na kwa maslahi mapana ya nchi yetu, haijarishi una chama au hauna chama. Ila mwingilu angemtafutia kazi nyingine ya kufanya. Ili kurudisha imani kwa watanzania, inayozidi kuporomoka siku hadi siku.
Ati nini? ... asingeendelea kukalia kiti cha ...?
Hili liwaziri ni mashine kubwa hata the late alikuwa analigwaya. Sema Mpina ni jasiri. Labda wanajuana na pengine wanabifu. Ni jasusi bobevu. Linaijua Nchi ndani na nje. Kuna wakati Jiwe mambo yalimlemea likawa assigned wizara Internal affairs. Wajeuri wakashikishwa adabu. Nchi ikatulia. Siyo jamaa la kuchukulia poa. Ni mtu-kazi kwelikweli. Hata Mama analijua. Lipo fedha purposely.
Kwa nguvu lilizonazo serikalini lina ndoto ya kuja kuwa Kiongozi mkubwa kabisa wa Nchi hii. Maybe baada ya Mama.
Simpuli za hili jasusi-bobezi ni pamoja na hiki kijamaa kinaongoza Nishati pamoja chenzie cha Michezo. Ni hatari hivi vijamaa. Ni timu msoga. Wazee wao ndiyo wamekishika chama-dola. Wanaongoza dola kwa remote. Hupenyi mpaka wakutambue na kukuhakiki wasije waka-risk tena kama walivyokosea 2015.
Haijulikani ni nani atatuongoza baada ya awamu hii kati ya hii miamba miwili, yaani, Fedha na Nishati. Labda ilikwishajipanga. Vina akili na strategies Usipime. Hiki cha Michezo kwa wakati huo kinajua kitakujakuwa kiPM au kinaweza kuwa opted kuchukuwa nafasi aliyonayo Afande babake ili kuendelea kuimarisha chama-dola. Chama ni mali yao Usije ukajichanganya ujue!
Msoga Jr. haijajulikana sana. Inaonekana aliingizwa kwenye siasa siyo mapenzi wala karama yake. Sijui. Labda kadiri siku sinasonga atabadilika. Lakini anaweza kubadilika. Anampenda na kumheshimu mno Msoga Sr babaake. Lakini kwa vyovyote Msoga Jr. anaweza wakati huo kushika, aidha, Fedha au Mambo ya ndani.
Ooh, ni majitu yenye akili sana. Utafanya makosa makubwa kuyachukulia poa.
Hii ni tafakuri yangu binafsi.
 
Back
Top Bottom