Mpina agiza bei ya maziwa kwa wanunuzi kunufaisha wafugaji

waziri2020

Senior Member
May 31, 2019
190
451
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina amekiagiza kiwanda cha Galaxy Food and Beverage limited kuhakikisha kuwa kinathibiti viwango vya Bei ili kuondoa hujma za kiabiashara ambazo zinaweza kufanywa ili kushusha thamani ya Maziwa ambayo yanayozalishwa hapa nchini.

Mpina alisema kuwa mifumo ya Bei inapaswa kuangaliwa kwa Ukaribu Sana kwa kuwa Maziwa yanaweza kuuzwa kwa mawakala kwa Bei nafuu lakini, sokoni Bei ikawa juu hali ambayo itashindwa kutofautisha na maziwa ambayo yanatoka nje ya nchi.

Akizungumza wakati alipofanya ziara ya kikazi mkoani Arusha alipotembelea kiwandani hapo kujionea uzalishaji wa maziwa kiwandani hapo,Mpina alisema kuwa serikali imeweka mazingira rafiki ya Biashara ili kuwezesha maziwa yanayozalishwa hapa nchini yanafanywa vizuri sokoni

"Katika Bajeti ya Serikali ya mwaka huu kupitia wizara ya fedha tumeondoa tozo na Kodi mbalimbali ili kuwezesha Uwekezaji huu kuendelea kuleta tija na Matokeo chanya hapa nchini,hivyo tozo na Kodi sio tatizo tena Sasa jipanueni nchi zima hizi asilimia 70 hazitoshi fikisheni 100"alisema Mpina.

Aidha aliongeza kuwa Maziwa yanayozalishwa na kiwanda hicho ambayo hufahamika Kama Kilimanjaro Fresh,yana Ubora ambao unatakiwa huku akiwataka kupelekea bidhaa hiyo katika mikoa ya dar es salaam,Mwanza na masoko yote ya ndani kwa kuwa uhitaji Ni mkubwa Sana.

Mpina alikipongeza kiwanda hicho kwa kununua maziwa kwa wafugaji kwa Bei inayoridhisha ya zaidi ya shilingi 800,kwani katika Bajeti ya wizara ya Mifugo na Uvuvi swala Bei liliwekwa kipaumbele.

Kwa Upande wake kaimu msajili wa bodi ya Maziwa Noely Byamungu,alisema kuwa uwepo wa kiwanda hicho ni muhimu katika kukuza uchumi wa wafugaji na Uchumi wa nchi.

Pia alisema kuwa kazi ya bodi hiyo ni kusimamia,kuratibu na kuendeleza tasnia ya Maziwa na wafugaji ikiwa Ni pamoja na kuhakikisha kuwa wafugaji wanafuga kisasa na kuzalisha malighafi zenye ubora unaohitajika sokoni.

Hasheem Said ambaye yupo katika kitengo cha Uendeshaji kiwandani hapo ameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuanzisha viwanda na kufufua kwani Vijana wamepata Ajira.

Hata hivyo ameiomba Serikali kusimamia Sera ya unywaji wa maziwa ili kuwezesha Watanzania kuongeza kiwango Cha utumiaji maziwa ili viwanda hivyo viweze kufanya vizuri zaidi.
IMG_20200816_112937_5.jpg
IMG_20200816_114018_1.jpg
IMG_20200816_110051_0.jpg
 
Maziwa ni kwa matajiri tu.

Sh 800 kwa lita toka kwa mfugaji kwenda kiwandani, unadhani toka kiwandani kwwnda kwa mlaji ni sh ngapi?

Kama mnataka raia ama kila mTz anywe maziwa kuboresha afya, serikali tieni ruzuku yenu huko ili bei irekebike na kila mTz aambulie angalau glass1 kwamwezi.
 
Back
Top Bottom