Mpigapicha TBC apigwa

Msharika

JF-Expert Member
May 15, 2009
947
69
MPIGAPICHA wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Josias Charanga ameshambuliwa na kuporwa kamera yake na Ofisa Usalama wa Taifa wakati akipiga picha maandamano ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala (KIU).

Wanafunzi hao zaidi ya 200 waliandamana jana hadi Ofisi ya Waziri Mkuu wakitaka msaada kwa madai kwamba wamedanganywa kwamba chuo hicho kimesajiliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) hali ambayo si kweli.

Katika maandamano hayo, walikuwamo waandishi wa habari wakifanya kazi yao akiwamo mpigapicha huyo wa TBC ambaye alipigwa na kunyang’anywa kamera yake.

Kabla ya kipigo hicho, ofisa huyo alimfuata mpigapicha wa Mwananchi na kumwuliza sababu za kumpiga picha na kuchukua kamera aliyokuwanayo na kumwamuru afute picha alizopiga.

Baada ya hapo, alimfuata mpigapicha wa TBC na kamera yake na kumkwida shati na kisha kumwingiza Mapokezi na kumpiga vibao kwa madai kwamba alimpiga picha wakati akiwatuliza wanafunzi hao.

“Usinipige picha, nitachukua kamera yako,” alisema ofisa huyo, maneno ambayo yalifuatiwa na kipigo na kunyang’anywa kamera mpigapicha huyo wa Kituo cha Televisheni cha Serikali.

Mapema wakizungumza kwa nyakati tofauti, wanafunzi hao walidai kuwa wamekuwa wakikosa haki za msingi sawa na vyuo vingine, kutokana na kudanganywa kuwa wamesajiliwa na TCU, hali ambayo si kweli kwa sababu chuo hicho ni cha masomo ya Posta, kwa kuwa kiko Kampala na huku ni tawi tu.

Walidai kuwa kama wangeambiwa mapema kuwa chuo hicho hakijasajiliwa, wasingejiunga, kwa sababu wapo wenye vigezo vyote vya kuingia vyuo vingine vilivyosajiliwa na TCU tofauti na hicho.

Tatizo lingine wanafunzi hao walidai kuwa ni ada kubwa wanayotozwa ya Sh milioni 2.7 ambapo pia walisema wamekuwa wakitozwa Sh 70,000 kwa kila mwanafunzi anayetakiwa kurudia mtihani baada ya kutofanya vizuri kitendo ambacho walidai si sawa.

Walisema kuwa wameshalalamika mara nyingi na kufikisha malalamiko yao mpaka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, lakini mpaka sasa wamekuwa wakiambulia ahadi na kuamua kuandamana hadi kwa Waziri Mkuu ili kufikisha kilio chao.

Hata hivyo, baadaye wanafunzi hao walitakiwa kutoa wawakilishi watano waingie ndani kuwasilisha hoja zao na baadaye mmoja wa wanafunzi aliyeingia ndani aliwatangazia wenzake kuwa watapewa majibu leo saa 5 asubuhi.

Source:HabariLeo | Mpigapicha TBC apigwa


 
Kazi kweli kweli.... UTAWALA WA SHERIA NA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI ITACHUKUA MUDA SANA KWA TANZANIA KUTIMIZA HILI....
 
Hawa polisi wa Tanzania wana matatizo. Either hawajui majukumu yao, au wanaenda beyond majukumu yao kwa makusudi as hakuna wa kuwauliza.
 
Hata sipati picha, mpiga picha wa TBCapigwa kwa ajili ya kupiga picha wanafunzi waliondamana , wapi na wapi? Tanzania inaelekea kubaya sasa.
 
Nahisi kama kiongozi mkubwa yuko kimya mno kwa mambo ya msingi katika kuendesha nchi hii... TAMKO KUTOKA KWENYE MAMLAKA ZINAZOHUSIKA NI MUHIMU SANA KWA UTATUZI WA MAMBO MAKUBWA KAMA HAYA....
 
WAVAMIA_IKULU.JPG
 
Back
Top Bottom