Jamani isitokee ktk kifo cha huyu babu wetu, kamanda wetu mkaanza unafiki na majungu. Dr.Kyaruzi na Nyerere wote walikutana Tabora secondary, ikiitwa Milambo secondary. Na wote walikwenda Makelele Uganda. Nawaomba sana msome maelezo yake mwenyewe marehemu Dr. Kyaruzi ukurasa wa 394 pia ni vizuri sana mkisoma habari hii toka nyuma na kuendelea mpate kujua mengi ya historia ya nchi yetu na watu waliohusika ambao hadi leo hawafahamiki na kwa sababu mbali mbali. Kifupi dr. mwenyewe anasema Nyerere alikuwa na tabia ya kuamini watu wasioaminika na kweli kabisa haya ndio mapungufu makubwa ya Nyerere ambayo yame tugharimu sana.Haya ndo mapungufu ya Mwl Nyerere,Aliwapoteza kwenye Historia akina Kyaruzi ili abaki pekee kwenye Historia na kuna vijitu vinaamini uhuru wa nchi hii ni matokeo ya harakati za miaka 6 i.e 1954 (kuzaliwa TANU) mpaka uhuru wa 1961, Hawajui kuwa Tanu imekuja kukamilisha kazi za wakongwe kama DR.Kyaruzi, Kwa mfano ukiwauliza vijana wasomi wa kisasa wakutajie wapigania Uhuru 10 wa nchi hii,itawachukua muda sana na kama wakijitahidi watakutajia waliokuwa mawazir wa kwanza wa Serikali wakati hao wapigania uhuru walitupwa kulleeeeeeee!!!!!! Watoto wetu hawajui kuwa Professa Babu ni Nguli wa Siasa ya Ujamaa Duniani mpaka leo wajamaaa Dunia nzima wanaadhimisha SIKU ya kifo chake kwa Mijadala yenye Afya.Buriani Dr.Kyaruzi historia ya VITABUNI umeachwa lakin kamwe vifuani mwa wapenda ukweli utadumu!
RIP Dr. Kyaruzi - Mpambanaji.