Mpigania Haki umetia sahihi hati ya Kifo chako

akashube

JF-Expert Member
Dec 24, 2009
401
23
Wanasheria, Mawakala wa usalama, Askari, Viongozi, wanasiasa, wafanyabiashara, waandishi wa habari, Mahakimu, .....

Unapoamua kuwa mkweli, ukaamua kusimamia haki na kuamua kupigania wanyonge wasionewe bila kurudi nyuma wala kusitasita, unakuwa umejitenga na wengi, na umetia sahihi mwenyewe hati yako ya Kifo.

Martin Luther King Junior, Solomon Mahlangu, Kwameh Nkurumah, John F Kennedy, Stan Katabalo, Patrice Lumumba, Ken Saro-Wiwa na wengine wengi ni mfano tu wa hatima inayotegemewa kwa mpiganaji yeyote.

Hivyo kama mpiganaji hutakiwi kuogopa, na unatakiwa uwe imara kukabiliana na matokeo yeyote ya kusimamia na kupigania haki. Hapo ndipo Afrika itakombolewa na kupata Uhuru Mamboleo.

Mpiganaji Solomon Mahlangu Muda mfupi kabla ya kunyongwa kwake alisema maneno yafuatayo.

''Waambie watu wangu kwamba nawapenda, na kwamba ni lazima waendeleze mapambano. Damu yangu itarutubisha mti utakaobeba matunda ya uhuru. Aluta Continua!"

ALUTA CONTINUA!
 
Back
Top Bottom