Mpiganaji Athumani Hamisi Apata Mapokezi ya Kishujaa.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,467
113,578
Saturday, May 8, 2010
MPIGANAJI ATHUMANI HAMISI APATA MAPOKEZI YA KISHUJAA

Mpiganaji Athumani Hamisi ambaye alikuwa matibabu sauzi kufuatia ajali ya gari mwaka jana akipokea maua toka kwa Bi. Mwanakombo Jumaa, mpiga picha na afisa habari mwandamizi wa MAELEZO alipotua jijini Dar leo jioni na kupokelewa na umati mkubwa wa wapiga picha wa habari, ndugu jamaa na marafiki wakiongozwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu Salva Rweyemamu, Kaimu Mhariri mkuu wa Daily News na HabariLeo Mkumbwa Ally, Mhariri Isaac Mruma, baba yake Athumani, Mzee Hamisi Msengi na wadau wengine kibao.
Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu Bw. Salva Rweyemamu
akimpokea Athumani Hamisi kwa furaha
Athumani Hamisi akiwa na Baiskeli ya umeme anayotumia akiongoza umati uliojitokeza kumpokea
Mhariri Isaac Mruma akimpokea maua Athumani
ambaye kaja na nesi maalumu (wa pili shoto)
Mwenyekiti wa Chama cha Wapiga picha za habari Mwanzo Millinga akimkabidhi Athumani Hamisi kadi maalumu iliyosainiwa na wapiga picha wote kumkaribisha nyumbani
Baba Mzazi wa Athumani Hamisi mzee Msengi akimpokea mwanae
Athumani Hamisi akitoka machozi baada ya
kumtia machoni rafiki yakeMatina Nkurlu wa Vodacom na dada yake (shoto) Mpiga picha mkuu wa Globu ya Jamii Francis Dande akimpokea Athumani Hamisi
Ankal akirekodi ujio wa Athumani Hamisi akitumia FlipVideo
athumani akielekea kupanda ambulance iliyokuja kumpokea
.. Athumani akiingizwa kwenye ambulance kabla ya kuelekea nyumbani kwake ambako atahudumiwa na nesi maalumu aliyekuja naye kutoa mafunzo yamwezi mmoja kwa mtu atakayemhudumia wakati wote. Mpiganaji Athumani Hamisi, pamoja na kuwa amepooza mwili mzima, ameonesha ushujaa wa aina yake kwa kuweza kumtambua kila aaliyemuona na kuongea naye kwa ucheshi wake wa kawaida. Globu ya Jamii inaungana na ndugu, jamaa na marafiki kumuombea apate nafuu na kurejea katika ulingo wa mapambano ya habari.
Source: Blog ya Michuzi.

Pole Mkuu Athumani!
Mungu atakujaalia urudi katika afya yako ya zamani!

Labda Pasco ungefafanua alipata ajali akiwa katika misafara ya kazini?...au ilikuwaje?

BTW, kazi zake commendable ni zipi, au ni vile mwanahabari ndo kapewa heshima kubwa ya publication namna hii?...Maana niliposikia MPIGANAJI nilitegemea kupata habari iliyopelekea kuitwa mpiganaji...anyway, labda ni semantics za ki-habari zaidi!
 
Karibu nyumbani Mpiganaji Athumani. Mungu ni mwema kama amekufikisha hapa ulipo leo wala husitie shaka kwani utapona na hakika utashuhudia utukufu wake. Karibu sana na pole kaka mkubwa
 
Pole Mkuu Athumani!
Mungu atakujaalia urudi katika afya yako ya zamani!

Labda Pasco ungefafanua alipata ajali akiwa katika misafara ya kazini?...au ilikuwaje?

BTW, kazi zake commendable ni zipi, au ni vile mwanahabari ndo kapewa heshima kubwa ya publication namna hii?...Maana niliposikia MPIGANAJI nilitegemea kupata habari iliyopelekea kuitwa mpiganaji...anyway, labda ni semantics za ki-habari zaidi!
PJ, Athumani Hamisi alikuwa mpiga picha wa The Guardian Ltd tangu lilipoanzishwa. 2005 aliacha kazi na kujiunga na campaign trail ya Mkulu, hivyo alizunguka nchi nzima, baada ya kazi nzuri, alitulizwa Daily News akafanywa mpiga picha mkuu baada ya Michuzi kupandishwa cheo.

Alipata ajali akiwa kazini akiwa na wanahabari wengine 2 ambao wote walisalimika, ila mmoja wa waliosalimika alipata ajali nyingine ambayo ilichukua maisha yake.

Anaitwa Mpiganaji kutokana na kuwa ni mwana habari anayejituma sana.
 
Pole Mkuu Athumani!
Mungu atakujaalia urudi katika afya yako ya zamani!

Labda Pasco ungefafanua alipata ajali akiwa katika misafara ya kazini?...au ilikuwaje?

BTW, kazi zake commendable ni zipi, au ni vile mwanahabari ndo kapewa heshima kubwa ya publication namna hii?...Maana niliposikia MPIGANAJI nilitegemea kupata habari iliyopelekea kuitwa mpiganaji...anyway, labda ni semantics za ki-habari zaidi!

PJ

Kwa uchache tu Athumani Hamis ni mmojawapo ya wapiga picha za habari(mwandishi wa habari huyu) maarufu nchini...Mpaka anapata ajali alikuwa ni Mpiga Picha mkuu wa gazeti la Habari Leo(pia aliwahi kufanya kazi The Guardian Ltd)..Alipata ajali mbaya tarehe 12 Septemba,2008 eneo la Kibiti mkoani Pwani akiwa njiani kwenda Kilwa mkoani Lindi, kwa ajili ya kuripoti matukio ya Taasisi ya Vodacom Foundation kufuturisha watoto wa mjini humo.

Mpigapicha huyo alikuwa na wenzake wawili, Heri Makange wa Channel Ten na Anthony Siame wa New Habari Corporation, ambao hata hivyo, hawakuumia sana kulinganisha na Athumani ambaye aliumia sana sehemu za kichwani na kifuani....

Baada ya ajali alilazwa MOI na kisha kupelekwa Afrika ya Kusini kwa matibabu zaidi(tarehe 28 Septemba,2008) na tangu wakati huo amekuwa huko kwa matibabu hadi jana aliporejea...

Nawapongeza sana Wanahabari(waandishi na wapiga picha) wa Tanzania kwa moyo huu wa upendo waliouonesha kwa mpiganaji mwenzao Athumani Hamis...Inatia moyo kwa kweli
 
Hii dhana ya 'mpiganaji' ni direct translation au kuna ujumbe uliojificha ambao wengine hatuufahamu? Upiganaji upi hasa unaoongelewa?
 
Upiganaji wa kuipigania jamii ipate haki stahiki na maisha yako binafsi
 
PJ

Kwa uchache tu Athumani Hamis ni mmojawapo ya wapiga picha za habari(mwandishi wa habari huyu) maarufu nchini...Mpaka anapata ajali alikuwa ni Mpiga Picha mkuu wa gazeti la Habari Leo(pia aliwahi kufanya kazi The Guardian Ltd)..Alipata ajali mbaya tarehe 12 Septemba,2008 eneo la Kibiti mkoani Pwani akiwa njiani kwenda Kilwa mkoani Lindi, kwa ajili ya kuripoti matukio ya Taasisi ya Vodacom Foundation kufuturisha watoto wa mjini humo.

Mpigapicha huyo alikuwa na wenzake wawili, Heri Makange wa Channel Ten na Anthony Siame wa New Habari Corporation, ambao hata hivyo, hawakuumia sana kulinganisha na Athumani ambaye aliumia sana sehemu za kichwani na kifuani....

Baada ya ajali alilazwa MOI na kisha kupelekwa Afrika ya Kusini kwa matibabu zaidi(tarehe 28 Septemba,2008) na tangu wakati huo amekuwa huko kwa matibabu hadi jana aliporejea...

Nawapongeza sana Wanahabari(waandishi na wapiga picha) wa Tanzania kwa moyo huu wa upendo waliouonesha kwa mpiganaji mwenzao Athumani Hamis...Inatia moyo kwa kweli
Balantanda, asante kwa kumbukumbu sahihi, huyu ni RIP, aliitwa kwa ajali ya pikipiki muda mfupi baada ya kusalimika ajali ya gari, alioa na kuitwa muda mfupi baada ya harusi yake.

Hata mimi nimeguswa na umoja wa Wapigapicha za Habari.
 
Upiganaji wa kuipigania jamii ipate haki stahiki na maisha yako binafsi

From my knowledge... this guy was/is "Muhidini Michuzi" type..... oppotunists.... In short, hawa ni wapiganaji wa matumbo yao. Nadhani watu (waandishi) wamekuwa touched kwa sababu ni mwenzao ...na ajali imemwacha katika hali mbaya! Anyway I wish you a very quick recovery Mr..
 
Macho_mdiliko, sio lazima udilike kwenye kila hoja, Muhidin Michuzi namfahamu mpaka type zake nazijua, ni mpiganaji, hata kama katika mapambano hayo pia atachumia tumbo mumo kwa mumo. Athumani Hamisi sio Michuzi type hata kama na yeye alikuwa na opportunities zake.
Isijekuwa kuwa kila mpiganaji atakayeipigania CCM basi ndio opportunist ila wapambanaji wa CUF na Chadema ndio wapiganaji wa kweli?.

Leave alone Michuzi on this, he is doing a good job kwa watu wa type yake!.
 
Kuitwa mpiganaji bado sijapata jibu hapa! Anapigania nini? alipigania nini?
 
From my knowledge... this guy was/is "Muhidini Michuzi" type..... oppotunists.... In short, hawa ni wapiganaji wa matumbo yao. Nadhani watu (waandishi) wamekuwa touched kwa sababu ni mwenzao ...na ajali imemwacha katika hali mbaya! Anyway I wish you a very quick recovery Mr..

Usemacho chaweza kuwa kweli, lakini lest not condemn those who help us in way or another simply because we differ in ideas or beliefs, hasa ukizingatia hii ni thread ya "mpiganaji Athuman" so if you have issues basi anzisha ya kwako ya opportunists wa matumbo yao!!!

Sikumjua authumani lakini nilipoona picha zake kabla na baada ya ajali, machozi yalinitoka hasa baada ya kuona ile picha akilia... tukumbuke sisi ni binadamu na hujafa hujaumbika!!! sijui kwanini alilia lakini niliweka a million questions in my head bila jibu hata moja... je anatamani asimame?, je ataweza kufanya kazi tena?, je ni mapenzi kiasi gani yameonyeshwa na waliompokea? aliyategemea mapokezi yale?

we are all humans na when you face tragedy, siku zote ni huzuni kuu... nampa pole yeye na wote wanaompenda

Pasco na Balantanda.... when you talk of Heri, it makes me very sad too, he went too soon na aliacha mjane kijana sana wakiwa na maisha mafupi sana kwenye ndoa!!!

sisi tumebarikiwa sana kuwa wazima, na hata kufikia kurusha tuwezavyo vineno, but God has all the passwords to our destiny!!!

Karibu athumani, mshukuru mungu kwa yote
 
De Novo...
yeyote atakayeona hizo picha... kama yu kweli binadamu aliyekamilika atasikitika sana sana sana. Pia mimi nimesikitika sana sana sana. Lakini kuhoji 'upiganaji' wake sio kutokumsikitikia...
 
MPIGANAJI ni neno analotumia MR MICHUZI kwa mtu yeyote anayefanya shughuli yoyote halali kuendeleza maisha yake mf.mwandishi wa habari,mfanyakzi au mjasirimali yoyote yule.
 
Mpemba bana..................u hali gani lakini?

Aaahh nipo shwari mwana, najiweka sawa hapa na gahwa na halua kabla hatujenda kumshuhudia Mildifilda wa zamani wa Rossoneri mzee wetu Carlo Ancelloti na kikosi chake ghali zaidi ktk EPL akinyakua title. Nadhani ni masaa machache kutoka hivi sasa.
 
Back
Top Bottom