Mpigachapa wa Serikali Kassian Chibogoyo ukimaliza Interview jitizame tena ulivyochemsha!

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
59,949
119,214
Akiwa bado anazungumza mubashara Clouds tv Kipindi cha 360 Mpigachapa Mkuu wa Serikali Bwana Kassian Chibogoyo leo ndiyo ama hakika amenithibitishia kuwa kumbe kuna Watu huko Serikalini wameziba tu nafasi za wengine na kihalisia hawastahili kuwepo hapo.

Nilipomwona hapo Studioni nilitegemea kuwa ningepata maelezo mazuri na yenye tija hasa kutokana na kile alichoitiwa hapo kukielezea ambacho kimsingi ni Wimbo wa Taifa, matumizi yake na faida zake kwa Taifa letu.

Badala yake huyu Mpigachapa wa Serikali Bwana Kassian Chibogoyo muda wote anabwabwaja tu, anazunguka zunguka tu, hajui anasema nini, muda wote anasoma tu katika Karatasi halafu kibaya zaidi anaonekana kuwa hakujipanga vizuri kwa interview kitu ambacho kimemfanya atumie mbinu moja ya Yeye kuongea sana ili tu asiwape muda akina Babie Kabae na Hassan Ngoma ya kumuhoji maswali magumu magumu ambayo yatafanya yamfikirishe.

Cha kuchekesha sasa hivi wakati Kipindi kinaendelea Mpigachapa huyu wa Serikali ameshaanza kupandisha jazba Studioni hasa kwa Mtangazaji Hassan Ngoma kwa swali moja kabambe alilomuuliza na amezidi tena kujitia aibu kwa kusema kuwa kama hao Watangazaji walikuwa wanataka ufafanuzi wa maswali yao mengine basi walitakiwa wamtumie maswali hayo mapema ili Yeye ajipange kuyajibu.

Mpigachapa wa Serikali Bwana Kassian Chibogoyo ama hakika leo umetokota na tunakushukuru kuwa umetusaidia kutuonyesha kuwa kumbe kuna Watendaji wengi huko Serikalini ambao mna Vyeo vikubwa lakini kiuhalisia hamna uwezo wowote na pengine ndiyo nyie nyie mnaoitia aibu Serikali. Unachelewa nini Kustaafu tu Mzee?

Kazi ipo hakyanani! Clouds tv hasa 360 tafadhalini siku nyingine na nyie muwe mnaangalia nani wa kuwaalika hapo Studioni kwenu na nadhani katika Wageni wote ambao mliwahi kuwaalika hapo Studioni nadhani huyu Mpigachapa Mkuu wa Serikali Bwana Kassian Chibogoyo ametia fora kwa kuharibu na ni kama vile ameifedhehesha Serikali kwani hakuna alichokisema na kikaeleweka.

Serikali huu ni wakati sasa mwafaka wa kutangaza nafasi ya Kazi ya MPIGACHAPA WA SERIKALI ili mpate competent candidate na siyo hao Watu wa hovyo hovyo.
 
Wako wengi hao. Si unaona hata gavana wa mkoa wanauliza vyeti vyake kwakuwa anachokifanya hakioneshi kuwa kaenda shuleni vizuri. We unatangaza kumtuhumu mtu leo J5 halafu unamwambia mkutane Ijumaa kisha unakwenda kumsachi Jumamosi. Kama sio utoto ni nini hicho? Ndio maana watu wanaitisha vyeti kwani huu si utendaji wa kisomi. Hawa wanaohakiki vyeti wangehamia kwa watendaji wakuu serikalini mpaka wa juu kabisa kwani wapo wengi wa namna hii.
 
Hao hao ndio wakikaa kwenye media unakuta wanasema "Vijana wa kitanzania hawana ujuzi na uzoefu katika kazi ndio maana hawaajiriki". Jinsi hiyo Mzee alivyojivua nguo najaribu kupata picha ni kwanini nchi ya kusadikika na vi-wonder inakuwa ngumu.
 
Ni Mwandishi habari au na je ni Ofis kabisa ina wafanyakazi au yuko peke yake tu.. Kweli hata mimi sijaelewa
 
Kujieleza na utendaji wa kazi ni vitu viwili tofauti.
Vingenevyo wale wanaojifanyaga kuchambua soka la ulaya wangesajiliwa wao wacheze.
Kabisa kaka jambazi..... Na Boss wangu ye hawezi kujieleza kabisa lakini ni mtu Wa kazi kabisa...sa hizi Nsengabwayo zinakuja na hoja za kipuuziii?!!!
 
Back
Top Bottom