Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Mpiga zumari mkuu wa kijiji chetu anaanza kuogopa zumari za wenzake; hataki kusikia wenzake nao wakipuliza zumari zao; hataki vipaji vipya kwa hofu wakisikika wengine atadharaulika na nyimbo za zumari yake zitachuja.
Wakati akipuliza kwa nguvu wanakijiji woote tulicheza na kumshangilia maana alipuliza kwa umahiri na ustadi wa hali ya juu. Wakati anashangiliwa waimba pambio wake walibeza wapiga zumari wengine eti hawana nyimbo mmpya; mpiga zumari kawafilisi na hawawezi puliza zumari zao tena. Wapo walioamini hivyo; wapo waliojiapiza kuwa wapiga zumari wengine wa kijiji hicho wameishiwa.
Wenzake wapo tayari na wao kuanza kupuliza zumari eti wanaambiwa wataaharibu nyimbo za mpiga zumari mkuu wa kijiji; wanataka kwenda vitongojini na wao wakapulize zumari zao wananchi wa huko wasikie wakaambiwa eti watasababisha vitongoji visifanye kazi ya uzalishaji mali
Wapuliza zumari wengine waliodhihakiwa kuwa wameishiwa wameanza kukamatwa na kutishwa na wagambo wa kijiji; wanapelekwa lock up eti kwanini nao wanataka kupuliza. "Huu mchezo haujitaji hasira"