Mpiga kampeni wa CHADEMA atekwa nyara: Hajulikani alipo kwa siku 5 sasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mpiga kampeni wa CHADEMA atekwa nyara: Hajulikani alipo kwa siku 5 sasa

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by mpinga shetani, Mar 29, 2012.

 1. mpinga shetani

  mpinga shetani JF-Expert Member

  #1
  Mar 29, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 3,268
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Mkazi wa Sakina, Omari Abdul maarufu kama 'Omari Matelefone!" amepotea na hajulikani aliko.

  Omari ni kada mtiifu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo na ni mmoja wa wapiga kampeni maarufu katika kinyang'anyiro cha ubunge wa Arumeru-Mashariki.

  Tayari tukio la kupotea kwake limeripotiwa polisi na kwa mujibu wa jamaa yake Chris Mbajo, Omar alitoweka tarehe 25 march mara baada ya kampeni za joini za chama chake kule Usa-River.

  Usiku huo Omar alionekana katika ukumbi wa Tripple A' pale Sakina akiwa kwenye ugomvi mkali na kada wa vijana wa CCM Benno Malisa na inaelezwa kuwa maofisa usalama waliingilia kati ugomvi huo lakini cha kushangaza walisikika wakimuamuru Omari 'avue "magwanda yake ya chadema" ambapo alikataa.

  Leo tarehe 29 March mkewe alienda kuripoti polisi kuwa mumewe haonekani nyumbani tangu tarehe 25.

  Waandishi wa habari walipoipata hiyo walimpigia Benno Malisa ambaye kwa sasa ni prime suspect na alichojibu kada huyo wa CCM Ni;

  "Simfahamu Omari wala kuwahi kumuona mtu wa namna hiyo!" kisha alikata simu na tangu hapo hakupatikana tena.

  Ni matumaini yangu kuwa Kwa kudra za Mungu Omar bado yuko hai ....................................................!!!!!!!!!!
   
 2. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #2
  Mar 29, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Je huyo mkewe alipata ushirikiano gani polisi?
  Je ndugu zake wameshatumia njia nyingine za kumtafuta, kama kuweka picha zake kwenye maeneo anayopendelea, kutangaza redioni au kwenye TV ...?
  Hata hivyo haya yote yana mwisho, na mwisho wake ni 1st April, lakini ni matendo yasiyovumilika.
  Poleni sana
   
 3. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #3
  Mar 29, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Hawa magamba wasije wakawa wamemfanyia huyu kada wa CDM yale waliyomfanyia kada mwingine Igunga. Hawa kuua binaadamu hawaoni shida kabisaa
   
 4. amkawewe

  amkawewe JF-Expert Member

  #4
  Mar 29, 2012
  Joined: Dec 9, 2011
  Messages: 2,029
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mungu saidia
   
 5. Ishina

  Ishina Senior Member

  #5
  Mar 29, 2012
  Joined: Dec 27, 2011
  Messages: 170
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tumuombee Mungu, huko alipo awe salama!! wao wana fedha, sisi tuna Mungu. Tusingependa kusikia yale yaliyotokea Igunga
   
 6. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #6
  Mar 29, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Duh benno malisa on marder scandal,patamu hapo
   
 7. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #7
  Mar 29, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,641
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Yameanza, dalili za mvua hizo!!
   
 8. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #8
  Mar 29, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ni habari mbaya sana kwa familia na wanaCDM kwa pamoja.
   
 9. k

  kagame Senior Member

  #9
  Mar 29, 2012
  Joined: Dec 6, 2008
  Messages: 159
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tetesi za kupotea au kuwekwa vizuizini kwa makada wa chadema Arumeru mashariki tulishazisikia tangu awali, lengo ni kupunguza idadi ya wapiga kura wa Chadema, inasemekanika uratibu wa haya mambo upo chini ya maafisa wa polisi waliotoka makao makuu Dsm pamoja na maofisa wa usalama wa taifa! Tuombe kamanda wetu omary awe mzima wasije wakamkolimba tu hao magamba na vyombo vyao vya dola.
   
 10. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #10
  Mar 29, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Utashangaa kusikia maiti imeokotwa mahala fulani!As Magamba iyo kazi wanaiweza
   
 11. Mundali

  Mundali JF-Expert Member

  #11
  Mar 29, 2012
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 749
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  CCM, Polisiccm, na ccmiss ni mavampire. How long shall they kill our people while we stand aside and look? How many are they so that every day they keep on threaten us, until when they will keep on deciding the well being of our life? Wake up every body, fight for your rights and justice (No peace without rights).
   
 12. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #12
  Mar 29, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Ngoja tuone mwisho wake,lakini hizi kauli za wao wana kile sisi tuna Mungu si za kujifariji hata kidogo,haya mambo yanatakiwa jino kwa jino!tusijenge fikra kua watu walio kwenye vyombo vya dola wote wanaridhishwa na udhalimu unaofanywa!hiyo si kweli hata kidogo!
   
 13. measkron

  measkron JF-Expert Member

  #13
  Mar 29, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 3,713
  Likes Received: 365
  Trophy Points: 180
  Wakamteke mkewe pamoja na mtoto ili aseme alipomficha Omar!
   
 14. N

  Nascoba JF-Expert Member

  #14
  Mar 29, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 214
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  jamani tutasubiri makada watekwe na kuuawa hadi lini?kwa nini tusichukue hatua muafaka na sisi nchi si yetu sote?tulianzisheni basi.
   
 15. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #15
  Mar 29, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  Huyo benno malisa ni wa kushikiliwa kwa uchunguzi akany** debe huyo!
   
 16. Idimulwa

  Idimulwa JF-Expert Member

  #16
  Mar 29, 2012
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 3,384
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Toka kwenye keyboard mkuu...uingie front.
   
 17. Ng`wanakidiku

  Ng`wanakidiku JF-Expert Member

  #17
  Mar 29, 2012
  Joined: Apr 18, 2009
  Messages: 1,196
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nadhani watakuwa wamemuua kama walivyofanya igunga:
  1. Walimumwagia kada wao tindikali
  2. Wakawaua na baadhi ya wana CDM
  Mi nadhani kama itakuwa huyu jamaa wamemuua basi hiyo laani itawatafuna wote walio husika. Maana Mungu aliye mkuu husimamia wenye haki na malipizi huwa hapa hapa duniani na wala siyo kusubiri siku nyingi. Na huyo Beno anaonekana ni muuaji maana ingekuwa vema kama angeongea tu vizuri na Omar kwani siku nyingine anaweza badili msimamo na kuwa CCM, lakini wao wanawatukana CDM kama vile wao siyo watanzania. Hapo ndiyo huwa nawachukia magamba wenzangu.
   
 18. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #18
  Mar 29, 2012
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,183
  Likes Received: 1,183
  Trophy Points: 280
  Hi ni turufu kwa cdm wakiunganisha na ya igunga kwa wana propaganda wazuri
   
 19. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #19
  Mar 29, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Sasa hii si demokrasia, Ocamp anatakiwa kulijua hili.
   
 20. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #20
  Mar 29, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Kama kweli ilo limetokea,na kwa Arusha ninavyo ifahamu,huyo mshukiwa atakua hayupo salama kabisa
   
Loading...