Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Habari wanaJF,
Nikiwa kama mtanzania leo nimekutana habari za kusisimua kiasi chake kuhusu usalama na siri za serikali kuwa hatarini. Nimesoma kupitia gazeti la Raia Mwema.
Rais John Magufuli amepelekewa faili lenye jumla ya kurasa 28 ambazo zina tuhuma mbalimbali dhidi ya Idara ya Mpigachapa Mkuu wa serikali, ambazo ni pamoja na bosi wa Idara hiyo kuvujisha siri za serikali kwa viongozi wa kubwa wa vyama vya upinzani nchini.
Katikati ya tuhuma hizo ni Mpiga chapa Mkuu wa Serikali Cassian Chibogoyo ambaye ameshikilia wadhifa huo kwa takribani miaka 22 sasa. Tuhuma hizo zieandikwa na watumishi wazalendo wa Idara hiyo katika barua yao ya Mei 05, 2016. Iliyopelekwa katika Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi (Ikulu).
" Ana uhusiano wa karibu sana na viongozi wa chama xha siasa cha upinzani. Kuna siri za serikali alikuwa akizitoa kwa chaama hicho. Kuna wakati tulikuwa tunashuhudia viongozi wa chama hicho wakija idarani kwa siri nyakati za usiku amabapo baada ya kufuatilia tuligundua kuna baadhi ya nyaraka ambazo ni top secrets za serikali"
Baada ya tuhuma hizo mpiga Mkuu wa idara hiyo alisema " Hapa sasa natamani nistaafu nikapumzike na wajukuu. Maana hii kazi inapresha nyingi. Kama ningekuwa situnzi siri ningedumu kwenye hii ofisi kwa miaka 22? Ninaowapa kazi wanakizi vigezo"
Idara ya mpiga chapa mkuu wa serikali ni miongoni mwa idara kongwe ikiwa imeanzishwa na serikali
ya mkoloni mwaka 1905 na makao makuu yake ya kwanza yakiwa mkoani Tanga.