Mpiga chafya aleta balaa kwenye gari, Wananchi wamteremshia Bunda kisa hofu ya Corona

kindikwili

JF-Expert Member
Oct 5, 2016
1,862
2,871
Wakuu sitaki tuchoshane, amani iwe kwenu!

Leo asubuhi kuna jamaa yangu moja wa kitambo yuko huko Musoma kanipigia simu akinieleza kuwa kuna mgonjwa wa corona Bunda na mwingine Musoma mjini. Nikamdadisi hakuwa na taarifa sahihi nikamwambia asipanik na wala asieneze uzushi wanaweza kuleta taharuki kubwa. Ikabidi nimtafute jamaa mwingine huko Musoma kumuuliza hiyo habari , jamaa kasema kwasasa hata mgonjwa wa homa anaogopwa kwasababu hata manesi na madaktari huko hawana uelewa wa kutosha na wana hofu kwa kila homa.

Musoma huko kuna mtu alikuwa na homa tu ya mafua na kikohozi cha kawaida kwa maelezo ya mtoa taarifa ila alipoenda hospitalini (jamaa hajasema ni hospital gani) manesi na madaktari wakawa wanamkwepa vile alivyokuwa anakohoa na kupiga chafya sasa wananchi waliokuwa pale wakajiongeza na kusababisha rumors kubwa ndiyo hiyo habari ikaenea ila si kweli. Nimemuonya ajiepushe na kutoa taarifa kwa tetesi.

Huko Bunda nimefuatilia kwa jamaa zangu huko wanasema kuna jamaa raia wa Kenya alikuwa anaenda Mwanza (kumbuka njia ya Sirari -Mwaza inapitia Bunda mjini) ,huyu jamaa alikuwa na mafua na akawa anapiga chafya mfululizo. Sasa toka Tarime watu wamemvumilia lakini walipofika Bunda uzalendo ukawashinda ikabidi wamshushie hapo Bunda mjini japo mwingine anasema walimuachia pale DDH (Hospitali hapo Bunda).

Huyu raia wa Kenya usiulize kapitaje maana mtu kutoka Sirari kwenda Kenya na kutoka Kenya kuja Sirari ni jambo lisiloweza kuzuilika kirahis. Akiwa mjaluo au mkurya utadhani alienda kununua chumvi upande wa pili sasa anarudi kwao akapike mboga.

Naomba serikali itoe elimu pia kwa wananchi wasiwe na hofu na wasiwasi sana maana huu ugonjwa umekuja umekuta watu na mafua yao na lazima watu wakohoe ,wapige chafya na kupenga makamasi yao, sasa hofu ikiwa kubwa ina maana waliokuwa na homa zao tangu awali watapata shida na wanaweza hata kushushwa kwenye usafiri kama hawa ndugu zetu.

Lingine Serikali ipige marufuku na iwe kosa kubwa mtu yeyote kujitangazia kama kuna mgonjwa wa corona mahali, wenye mamlaka wawe ni watu waliopewa mamlaka hayo na serikali. Bila hivyo hata bei ya vyakula vitapanda kizembe kwasababu ya panic purchase.

Kindikwili.
 
Tukiachana na hizo habari nyingine, mpaka wa sirari ni moja ya mipaka ambayo iko lose sana.

Kwa ugonjwa kama huu ni rahis sana mgonjwa kutoka nchi moja kwenda nyingine bila kushtukiwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tukiachana na hizo habari nyingine, mpaka wa sirari ni moja ya mipaka ambayo iko lose sana.

Kwa ugonjwa kama huu ni rahis sana mgonjwa kutoka nchi moja kwenda nyingine bila kushtukiwa.

Sent using Jamii Forums mobile app

Umenena mkuu ule mpaka uko lose sana lakini pia mpaka wa Tanzania na Kenya nadhani kwa ujumla ni mgumu sana kuudhibiti maana ni ndefu mno.

Ukianzia Tanga Mpaka uko Tarime na Rorya ukiachana na mipaka yenye utaratibu kama Holili, Sirari nk bado ziko njia za kuvukia (njia za panya chungu nzima).

Kule Tarime na Rorya baba moja ana wake nchi zote mbili sasa kuenea kwa magonjwa kama haya yanaweza kuwa changamoto sana bila kusahau visa vya wamama wa Rombo
 
Tukiachana na hizo habari nyingine, mpaka wa sirari ni moja ya mipaka ambayo iko lose sana.

Kwa ugonjwa kama huu ni rahis sana mgonjwa kutoka nchi moja kwenda nyingine bila kushtukiwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mpaka wa sirari watu na bodaboda zinavuka bila ya kupitia immigration.

Plus kuna chocho flani bodaboda wanaitumia kupitisha magendo
 
Back
Top Bottom