MPESA: Kutoa Tsh. 10, 000 wanakata Tsh. 1,500

Ni makubwa sana, siku hizi palipo na uwezekano natumia benki, huduma za mobile money ni ghali sana siku hiz
Kwa aliyeko Nanjilinji hana namna... maana ni bora hayo makato kuliko kusafiri kufuata huduma hiyo hiyo mahala ilipo... fikiria ipo Lindi... then inakuwaje.!?
 
Kuna mtu alinipa hela yake nimuhifadhie kwa muda usiojulikana,nikaamua kuiweka kwenye Mpesa nikijua ataweza kuichukua kesho au kesho kutwa,hakuchukua,sasa ameniambia ataihitaji mwisho wa mwezi huu,nimeangalia makato nitakayotozwa kuitoa hiyo hela nikashtuka,itanilazimu kuzama mfukoni ili nijazie hela ya watu,najuta.
 
TCRA wamenabweka tu ila hawana meno
Walisema mitandao ya simu ipunguze gharama za MB internet bundles lakini ni yale yale tu hakuna kitu Mitandao ya simu hawajabadili
 
Back
Top Bottom