Mpenzi wangu kaniacha baada ya kugundua kuwa nina watoto wawili

IsaacMG

Member
Dec 6, 2019
63
51
Aisee jana ilikuwa siku mbaya sana kwangu pale aliyekuwa mpenzi wangu alipoona picha za wanangu kwenye status ya WhatsApp. Aliniuliza na nikaamua kumwambia ukweli bila kuficha kitu kuwa nina watoto wawili tayari japo sijaoa. Alishindwa kunielewa nikabembeleza akagoma kunielewa na kuniambia kuwa mahusiano yangu na yeye yaishie hapo.

Aise niliumia sana na ukizingatia huyu binti nilikuwa nimemuelewa sana maana ana sifa zote za nje na ndani -- zote anazo.

Naombeni ushauri wenu, nitumie maneno gani aweze kunielewa au nifanye nini nimsahau kabisa ili maisha mengine yaweze kuendelea?

Wazoefu ushauri wenu unahitajika katika hili.

Asanteni sana.

GOD is GOOD
 
Mkuu jaribu kumbembeleza. Mtafute kwa bidii zote mkae muongee. Kama anakupenda atakuelewa tu. Mwonyeshe kuwa kuzaa kwako hakuna athari yoyote kwenye mahusiano yenu. Kila la heri mkuu. Na pole sana.
 
Ulichofanya ni sahihi hata kama imetokea kwa bahat mbaya, kama u were destined to each other kuwa na watoto haitakua big deal kwake.

Bora amejua kabla hujamuoa
 
Back
Top Bottom