Mpenzi wangu hana hisia nami tena, roho inauma sana

Some broken heart never mend...ebu Mungu nisaidie!....
 
Mm ni mvulana, nampnz wangu nimedumu nae karibia mwaka 1, lakn kama mwezi umepita mpnz wangu ame nibadilikia sana, kwasabu nampenda nimevumilia mengi sana, cha kuchangaza nimeongea nae, ana niambia hana hisia na mm tena! Hawezi fanya chochote na mm, Sijawa mkosea pia sistahili adhabu anayo nipa..nmejaribu kumpotezea nimeshindwa, hata kuanzisha uhusiano na mtu mwingine naona ntakuwa najidanganya.. nampenda sana, roho inauma, naumia sana. Wapendwa nakosa furaha hata kula naona tabu, nina miaka 24 yeye ana miaka 21 , nime maliza chuo na yeye ndio ameingia kwaka wa tatu, kumpotezea siwezi naombei ushauri jinsi ya kurudisha hisia zake kwangu!..nina hali mbaya sana

Ndugu huyo siyo wako, unakumbuka threat iliyokuwepo juu ya jamaa na mkewe, aliyepata kazi mkoani, yeye akabaki Dar? alipomuuliza mkewe juu ya sms akaambiwa 'nilikuwa nakusubiri tuachane nimempata anaenifaa zaidi, jamaa akajifanya mkali na kusema nipeleke kwa huyo jamaa, akapelekwa jamaa akasema hatuachani, na wako kwenye ndoa, lkn ww ni urembo tu ambao unaweza badirisha marashi? achana nae baana!
 
samaha kwa kuyatamka haya maneno........ that girl is very stupid ever, anadai hana hamu wala hisia juu yako halafu.... anafanya hayo?

Sasa kaka, huu ni ushauri wangu wa mwisho....... make call divert for her numbers, make sure you set your phone to reject her call and sms all the time. Achana na huyo mpuuzi anarudisha nyuma maendeleo yako, badala ya kuwaza mawazo ya kimaendeleo, ya namna gani ujikwamue katika dimbwi la umaskini tulionao katika jamii yetu unakalia kuwaza mambo yake which are not productive in your life. ukishindwa kufanya hivyo omba msaada kwa rafiki wako wa karibu akusaidie kuset simu yako.........au call me 0775155411 ntakusaidia.
Vinginevyo kaka tujue tu moja kuwa bado una interest nae......kama yes....... basi vumilia matusi yake....... lakini kumbuka siku moja atakuonyesha jamaa zake wakiwa wamempanda wanamduuu..... hapo sasa presha yako haitokuwa ya kupanda tena bali ya kuteremka

u always av some wonderful words of wisdom!
 
we vp, keshapigwa kibuti uyu, mshauri achape lapa, vinginevo ajiandae kuwa mshika pemba watoto wa mjini wakikamua.
We dogo acha ufala wako usimpende demu kwa 100% hawa ni km kungulu leo mti uu kesho ule pia hawafugiki, dawa yao chapa mimba pia chapa lapa kwa mpigo

hata wanaume hawafugiki leo huyu kesho yule, wadada siku hizi wanatahadhari sana na wanaume, kuhusu mimba wala usijidanganye kabisa mdada wa siku hizi akibeba mimba kaamua wala sio kwamba umemkomoa, nani anabeba mimba za bahati mbaya sasa hivi labda ukutane na wale ziro brain.
 
hata wanaume hawafugiki leo huyu kesho yule, wadada siku hizi wanatahadhari sana na wanaume, kuhusu mimba wala usijidanganye kabisa mdada wa siku hizi akibeba mimba kaamua wala sio kwamba umemkomoa, nani anabeba mimba za bahati mbaya sasa hivi labda ukutane na wale ziro brain.

unayo yasema ni ya kweli na mm kosa nililo fanya ni kumpenda kwa dhati!
 
Suprise, umenipa moyo kidogo na mimi, mana nina tatizo kama hilo, nimegombana na mpzn wangu jana nimejaribu kuplease but anaonekana kukaza usi wa kuvunja mahusiano, sababu ni kuwa namfuatilia sana analalamika kuwa hana uhuru kwani namfuatilia sana kwenye simu na facebook kwa watu anaochati nae, na sasa yuko chuo na nimemsaidia sana kipindi cha kwanza wakati anaripo chuo mana wazazi wake hawakuwa vizuri kifedha wakati huo, nimekuwa nae karibu sana kwa muda wote huo, kiukweli naweza kusema ni mwaminifu kiasi mana amekuwa muwazi kwangu kwa kila kitu, ila anapenda sana kuchati na nikifuatilia nakuta hakuna uhusiano wa kimapenz na hao anaochati, sasa amechukia na amewaomba ushauri wenzake huko hostel wakamshauri eti aachane na mimi kwani namfuatilia sana,na hii ni mara yapili kukosana but tulisameheana, nimemuomba msamaha sana lakini amekataa anasema ni mara pili nimerudia hivo ni tabia yangu hii anaogopa, jinsi alivyo ni mtu ambae si mwepesi wa kuchukia but ni mgumu kusamehe akishachukia, naombeni msaada wenu wadau, nimvutie muda afu nirudi tena kuomba msamaha au nipotezee? mana kwa sasa niko mabli nae ila nimemwahidi kwenda wikiend ijayo lakini amekataa, hayuko tayari kuonana na mimi, hivyo nimemuacha pending kwanza! nipeni ushaurini ndugu zangu,
samahani kwa kukurukia thread isiyo yangu,

Hapo kaka usifanye kitu ambacho yeye hakimvutii,ushagundua tatizo,ushauri wangu sikuzote kwa tatizo aina yako ni kufanya kitu kigumu,mpe mwanamke nafasi akumiss,kama unamganda sana jitahidi umpotezee,kwa wewe kaa kama siku nne usimtext wala kumkol,baada ya hapo call her,usiombe msamaha mara ya pili,huo ni ubwege,mkol jitahidi kumchekesha na usiongee suala la mapenzi,halafu mpotezee tena hata wiki ukiweza,na acha kumfatilia sana bwana,mwanamke hachungwi,wewe attitude yako ndo itamfanya atulie na ww na wala hutokua na wasiwasi.



Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Hapo kaka usifanye kitu ambacho yeye hakimvutii,ushagundua tatizo,ushauri wangu sikuzote kwa tatizo aina yako ni kufanya kitu kigumu,mpe mwanamke nafasi akumiss,kama unamganda sana jitahidi umpotezee,kwa wewe kaa kama siku nne usimtext wala kumkol,baada ya hapo call her,usiombe msamaha mara ya pili,huo ni ubwege,mkol jitahidi kumchekesha na usiongee suala la mapenzi,halafu mpotezee tena hata wiki ukiweza,na acha kumfatilia sana bwana,mwanamke hachungwi,wewe attitude yako ndo itamfanya atulie na ww na wala hutokua na wasiwasi.



Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

total i agree' uo ndo ukwel mkuu..
 
Mkuu wangu hii kitu ilinitokea acha tu,kuna uzi nilianzisha humu,tatizo unajuwa na mimi nilikuwa hivyo hivyo nilimpenda sana wangu akawa ananiendesha kama mtoto mdogo,unajuwa nini cha kufanya,kata mawasiliano na kama akikucall ongea in short hamna haya ya kujielezea anythin,vile vile tafuta msichana mwingine mzuri kumzidi utaona mwenyewe,now hawa watu wanaitwa wanawake hawanisumbui akili,ukimpenda mwanamke usimuonyeshe kwa 100% ndio inakuwa vizuri zaidi.....la sivyo atakuendesha sana na utajuta....

Kuwa mpole kaka na mpotezeee tu najuwa ni ngumu ila ndio hivyo jitahidi tu utaweza najuwa...

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Naona hata usingizi huupati kila kitu unaona kibaya,piga moyo konde na mtoe kwenye mawazo yako chukua chombo kikali zaidi yake,afadhali yako wewe ila me nilihudumia kila kitu na kumpangishia nyumba nikapangisha ila ndio akaja kuleta visa vya ajabu ajabu na vituko vingi sana iliniuma sana sasa wewe ni rahisi kumfuta kwenye akili yako. Tatizo huko vyuoni wanadanganyana sana ndio problem kubwa iliyopo hapo na wanamshauri vibaya

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
ndugu mapenzi ya chuo ni mabalaaa, fanya kumpotezea fanya maisha zen akirudi chakachua tena na tena
# IF YOU LOVE SOMETHING SET IT FREE, IF IT COMES BACK TO THEN ITS YOURS BUT IF IT DOESN'T HUNT IT DOWN AND KILL IT.....me nalala bana
 
Hapo issue mkaushie kitambo au kama vipi tafuta kuku wa kienyeji uwe una mnyonyoa wakati unasikilizia ulikotoka.Na kuhakikishia utajisikia poa
 
Sometime unatakiwa ufanye maamuzi magumu, mbona gals wapo wengi? Huyo uliyempenda sana ashakudhihirishia kuwa wewe sio chaguo lake, so mvungie cku kadhaa usipoona reaction yoyote toka kwake tambua alichokuambia hakuwa anatania.
 
Mwanangu, kama kuku wako kapotea, unaanza kumtafuta halafu ukaona lundo la manyoya ya huyo kuku, ujue ameliwa!!!
 
Ukiona hivyo jua ushapinduliwa. Lazima kutakuwa na mtu ambaye ana hisia naye. Anyways, huenda umezidiwa kete au mpenzi mwenyewe ni kiruka wa kawaida.
 
ahsante mdida tatzo, hisia zote zpo kwake jinsi ya kuamisha hisia kwenda kwa mwingine

Meku naona unakomazwa kimahusiano. Hatua hii ni muhimu kwako, umejifunza kwa maumivu.
Umejua kwamba mapenzi sio asali peke yake, kuna shubiri pia....tena ya kutosha.
Nikisoma maandishi yako kati ya mistari naona kama umekua mwema mno kwa huyo mwenzio, mwema mno kiasi cha kumkifu. Hebu mpe nafasi kidogo, mwache aone umuhimu wako...pia punguza kufanya kila analotaka.....be yourself.

Ni muhimu kujua kwamba ndani ya asali ya mapenzi kuna shuburi pia!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom