Mpenzi wangu aombwa rushwa ya ngono ili apate kazi.

..Ajira ktk sekta rasmi zimekuwa ngumu sana siku hizi-hata kama umesoma vizuri. Sasa vijana wetu wengi vyuoni hawako realistic, wanakuwa na matumaini makubwa sana ya kupata ajira na "kufanikiwa kimaisha" mara tu baada ya kumaliza chuo. Matokeo yake mtu anatafuta kazi kama miezi 8 hivi bila mafanikio, wakati mwingine miezi inakatika bila hata ya kuitwa angalau kwenye usaili.

Hapo ndipo dada zetu wenye roho nyepesi na wapenda mteremko wa sekenke wanapoanza kutafuta njia za mkato. Njia za mkato sio suluhisho maana hata hao "mabosi njaa" wanajua kwamba ajira ni ngumu na mara nyingi wanakuwa hawana hata mamlaka ya kumuunganishia mtu kazi, leta alone kupendekeza jina lako ili uitwe kwenye interview. Kuna hatari kubwa ya kuliwa kitumbua na kazi usipate.

Pia siku hizi wamejitokeza wajasiriamali wa ajira. NGO inaweka tangazo la kazi na baadaye kukutumia email uende kwenye ofisi zao ambako watakwambia uchangie gharama za kuendesha interview ndipo uitwe kwenye interview. Ikifikia hatua hii, kimbia-hawa ni wajasiriamali tu! Kila la kheri vijana mnaosaka ajira!
 
mwambie 2 atoe kama anataka kazi,,then wewe kama unamwonea uruma masaidie utowe wewe kwa naaba yake
 
Wizara ya elimu.

Wizara ya Elimu makao makuu? Kama makuu ni idara ipi? Utumishi, Sera na Mipango,Ukaguzi,Elimu ya Msingi, Elimu ya Sekondari,Vyuo vya Ualimu, Ufundi, Elimu ya juu? Funguka Mkuu tujue pakuanzia.

Ninachoshngaa ni hiki, Siku hizi wanaajiri kupitia Tume ya ajira inakuwaje Mpenzi wako anadanganywa kwamba kuna ajira wakati wanaotangaza ajira na kusaili ni Tume ya Ajira
 
Yaani jamaa amekuja fungua thread huku badala ya kwenda PCB..............angalia usije kula nyasi.
 
Hata humu wengi ni wahanga na wanamaisha mazuri, semina za hapa na pale, trip za ndani na nje ya nchi, na hawaonyeshi ku-regret. Unategemea watakushauri nn?
 
Jamani Tanzania hali si nzuri hata kidogo.
Mpenzi wangu yupo katika wakati mgumu wa kutafuta ajira,jamaa amemuahidi kazi ipo ila awe tayari kumtolea nguo za ndani.
Nimemshauri aachane nae na kuangalia utaratibu mwingine.

Mue makini dada zangu kwa hili.
Believe me huo uamuzi uliomwambia auchukue utakutesa sana wewe siku za usoni, kama bado utakuwa hapa utanambia..........EXPERIENCE
 
Sasa huyo jamaa mnataka mumuachie hivi hivi apete si mumuekee mtego apate funzo? Kwani mumuachie dhalimu hivi hivi? Mtegeni ili akome tabia hiyo na wengine wapate salama
 
Usiamini sana wanawake inawezekana ka fail interview ndo kaja na sababu hizo-afu wewe unadhani wakivua nguo za ndani huwa wanasema....wakisema ujuwe wanakasoro za kiakili tu.
 
Vipi ikitokea akipata kazi kihalali,yaani bila kutoa ngono wewe utajisikiaje?
 
usiamini sana wanawake inawezekana ka fail interview ndo kaja na sababu hizo-afu wewe unadhani wakivua nguo za ndani huwa wanasema....wakisema ujuwe wanakasoro za kiakili tu.
precisely!
 
Back
Top Bottom