Mpenzi wangu aombwa rushwa ya ngono ili apate kazi.

Alikua anatafuta kazi wa ualimu, ya polisi au ya Jeshi? Ni kazi ya serikalini au private sector?
 
Jamani Tanzania hali si nzuri hata kidogo.
Mpenzi wangu yupo katika wakati mgumu wa kutafuta ajira,jamaa amemuahidi kazi ipo ila awe tayari kumtolea nguo za ndani.
Nimemshauri aachane nae na kuangalia utaratibu mwingine.

Mue makini dada zangu kwa hili.

Vile vile kumbuka angekuwa anasifa kama zako wangemalizana juu kwa juu
 
Pole sana, jipeni moyo. Huo ni mtego.akinasa atakuwa mtumwa daima kwa hilo fataki. Mbweha huru japo mnyonge kuliko mbwa aliye kwa bwana lkn ana booonge la mnyororo shingoni. Askate tamaa ajarib kusoma magazet kama ana sifa,atakutana na ofis zenye watu makini
 
Kama mama ntilie anahonga k asikamatwe na city huyo mpenzi wako ameshindwa kasababu jamaa hana mvuto
 
Jamani Tanzania hali si nzuri hata kidogo.
Mpenzi wangu yupo katika wakati mgumu wa kutafuta ajira,jamaa amemuahidi kazi ipo ila awe tayari kumtolea nguo za ndani.
Nimemshauri aachane nae na kuangalia utaratibu mwingine.

Mue makini dada zangu kwa hili.

Mh aendelee tu kutafuta atapata kwa njia salama. tz kumevunda haswa yan cku iz wakaka wanaambia wahonge pesa ndio wapate job. wadada ndio rushwa ngono. inasikitisha kwel yan. smtin need to b done 4 ril. watu fulan fulan wanatakiwawawajibishwe, ila ndio ivo tena vilio vyetu kama samaki vinaishia kwenda na maji. duh. 9t ppo.
 
Vitendo vya unyanyasaji katika kutafuta ajira havitakoma kama kila anayetakiwa kufanya mapenzi kabla ya kupata kazi anaishia ama kukubali au kukataa hiyo kazi na kuacha watanzania wenzake wakinaswa na mtego wa hao mafataki. Mimi naamini ni wajibu wa mtu anayeombwa rushwa ya ngono kuchukua hatua kwani kama hayuko tayari kutoa hiyo rushwa hana cha kupoteza kama ataripoti katika taasisi zinazohusika. Najua wengi watasema hata hizo taasisi nazo haziaminiki, lakini kuna makundi ya wanaharakati ambayo wanaweza kutoa msaada mkubwa hasa kwa akina dada wanaokutana na adhaa hii. Mojawapo ni TAMWA.

Tuwatie moyo ndugu/jamaa zetu wanaokutana na matatizo haya kuchukua hatua sahihi badala ya kukwepa kwa kutafuta kazi sehemu nyingine.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom