Mpenzi wangu amepigwa Risasi 3 Jana asubh...Hali yake ni mbaya.!

Supervisor

JF-Expert Member
Oct 29, 2010
559
207
Wana jf wenzangu.!
Jana ilikuwa siku mbaya mno kwangu baada ya Mpenz wangu kunipigia cm kuwa wamevamiwa na majambazi huku akilia akisema anakufa..! Nilichomwambia ni kwamba azime simu na aifiche, naona alifanya hvyo. Lakn kwa vile alikuwa amekaa seat ya dirishan alipigwa risasi 3, mguun, tumbon na mkonon. Hivi jana yeye na majeruhi wengne serious wamepelekwa Bugando hospital mwanza. Jaman naomba Mungu ili aweze kupona. Walivamiwa wilaya ya kibondo mkoan Kigoma na m2 1 alikufa hapohapo. Nalia mie jaman...
 
pole sana ndugu.
Tumwombe mungu aweze kupona ili muendelee kufurahia maisha.
Vyombo vya ulinzi na usalama fanyeni kazi zenu vyema.
Tumechoka kusikia mauaji ya raia wasio na hatia na hata kupata ulemavu wa kudumu.
 
Duh pole Mkuu. Mungu amponye mapema shemeji, na kuwapeni nguvu kwa pamoja. kaza moyo.
 
Pole mkuu. Mungu ya mwema atasikia sala na maombi yetu kwajili ya majeruhi wote. Shimbo,Mwema,UWT na Tossi mnafanya nini? Au ndo mpaka kuchakachua tu?
 
Tunawaombea wote kwa Mungu awajalie kupona haraka. Nanyi ndugu na marafiki mguswe kujitoa kwa hali na mali kuwasaidia wenzetu waliojewruhiwa au na kuathirika kwa namna moja au nyingine na kadhia hiyo ya ujambazi.
 
pole mkuu hii ni habari ya kusikitisha sana, tutazidi kumuombea apone haraka
 
Pole sana ndugu Mungu awapiganie na awaponye majeruhi wote
 
Pole sana Supervisor, tunamwombea kwa mwenyezi Mungu ili apone haraka..:redfaces:
 
Nakumbuka jana musa aliomba msaada hapa jf na tulishilikiana kutoa namba za polisi na wengine walidhani ni utani kumbe ni ya kweli. Pole sana mkuu mungu yupo nawe ni mategemeo yetu kuwa atapona kwani ktk heri mungu huweka heri pia


eee mungu bariki mwana jf mwenzetu uwa lake la moyo lipate nafuuu mapema

mapinduziiiiiii daimaaaaaaaaaa
 
Hakika ni suala la kumshukuru Mungu kwa kuwa bado yuko hai. Tuko pamoja kimaombezi. Hope those involved will recover soon. Tumtangulize Mungu mbele ndo muweza wa yote.
 
POle sana Mkuu. wakati tukimuombea shemeji apone haraka, nadhani ni wakati pia mamlaka husika zikazidi kuchukua hatua madhubutii kukabiliana na ujambazi huu wa utekaji magari ambao unaonekana kutaka kurejea tena
 
pole sana muheshimiwa....
Sala zetu ziko naye na wengine waliokubwa na huu mkasa...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom