The Donchop
JF-Expert Member
- Jan 10, 2014
- 294
- 378
Habari wanajamii,
Nimekuja tena kwenu kuomba ushauri na ninaomba msaada wenu.
Mpenzi wangu ambaye tumekaa nae kwa miaka mitatu sasa, juzi tulipishana kiswahili.
Labda niwaeleze jinsi tulivyoishi mwanzo. Kusema ukweli, miaka miwili nyuma, mpenzi wangu huyu alinipenda hata mimi nilijua wazi bila hata yeye kunitamkia hivyo mara kwa mara. Alinijali, alinishirikisha kwenye kila jambo na hata kunitambulisha kwao.
Baada ya miaka miwili kupita, ugomvi ulianzia kipindi wamekorofishana na kaka yangu mkubwa kwa mambo yasiyonihusu mimi. Wakagombana wao kwa wao. Na kosa lenyewe ni mtu wa tatu kuwachonganisha. Binafsi naliona ni la kawaida sana.
Baada ya ugomvi huu, tulikaa chini na nikamuuliza nini hatma yetu. Akajibu kuwa hayo ni ya kawaida nisiwe na wasiwasi. Tukaendelea kuwa pamoja ingawa yeye akaanza kubadilika. Nilijaribu kumwelewesha lakini hakukuleta mabadiliko.
Siku moja alinipigia simu pasipo na ugomvi na kuniambia mimi na yeye basi sababu hana tena amani kutokana na ugomvi wa yeye na shemeji yake. Nililia sana. Kwa mara ya kwanza nilikunywa pombe siku hiyo nikidhani zitanisaidia kulala. Mwisho wake niliishia kumpigia simu na kuendelea kugombana.
Kufupisha tu ni kuwa, tunarudiana na tunakaa kama miez mitano tunaachana hata kwa wiki, hayo ndiyo maisha yetu.
Imekua hata kawaida kwangu akiniambia tunaachana. Wala silii tena wala kumsumbua kuomba msamaha. Leo tena amenipigia simu na kuniambia hana tena upendo kama uliokuwepo zamani. Lakini nilipoongea nae tena tukakubaliana kurudiana ingawa inachukua kama wiki mpaka kuwa kwenye hali ya utulivu kabisa.
Ndugu zangu nimekuja kuomba ushauri, sielewi kama mtu huyu ananipenda au anamaanisha anachokisema. Hana mwanamke yeyote na wala hataki kabisa. Muda wowote naweza kwenda kwake na cm yake nikaisach. Lakini kinachonip mashaka ni yeye yuko upande gani? Ananipenda au hanipendi? Ukizingatia juzi tu kabla ya ugomvi ametoka kunipigia cm na kuniambia jinsi anavyonipenda. Mimi nampenda ingawa kama itashindikana kutafuta suluhu niko radhi kuachana naye moja kwa moja. Je kuna njia yoyote ya kumfanya mpenzi huyu awe na amani na kumfanya asiwe na hasira na kusimamia kile anachomaanisha?