Mpenzi wako bado anahifadhi Picha ya Mpenzi Wake wa Zamani

Status
Not open for further replies.

Regia Mtema

R I P
Nov 21, 2009
2,970
863
Kuna rafiki yangu mmoja, analalamika na kuhuzunika kuwa mume wake bado anamiliki picha,maua,kadi na hata mashairi ya mapenzi aliyokuwa akitumiwa na mpenzi wake wa zamani.Huyu binti yuko kwenye ndoa kwa mwaka wa tatu sasa. Hivi vitu ni vya mpenzi wake wa zamani ambaye waliachana kabla ya kuwa na huyu rafiki yangu.Rafiki yangu huyu roho inamuuma kwani anahisi mumewe huenda akawa bado anampenda huyu mnyange wake wa zamani,anasema amevumilia sana.Mbaya zaidi mumewe na huyu mpenzi wake wa zamani wanafanya kazi ofisi moja hivyo hukutana karibu kila siku.

Hivi hii imekaaje,je huyu jamaa ni kweli bado anampemnda huyu mpenzi wake wa zamani?je binti avichome moto hivi vitu?
 
huyo jamaa hamtendei haki kabisa mkewe...hakuna kitu kinawauma wanawake kama hicho....mshauri rafiki yako ateketeze kila kitu kinachomuhusu huyo ex wa mume wake
 
huyo jamaa hamtendei haki kabisa mkewe...hakuna kitu kinawauma wanawake kama hicho....mshauri rafiki yako ateketeze kila kitu kinachomuhusu huyo ex wa mume wake

kwa hiyo na mimi utanilazimisha niziteketeze picha za ex wangu? Wee Preta wewe
 
Anaweza kuteketeza kila siku lakini sio moto wa mapenzi ulio moyoni mwake.
Anaweza akawa na picha na kadi lakini asiwe na issue yoyote na huyo demu.

Na mkewe akileta kisirani tu, jamaa atamwambia ex wake na watalianzisha kikweli.
 
labda ndie wakwanza kwake ndio maana anamkumbuka kwa hizo picha chakufanya jitahidi mambo atajaribu kusahau lakini hapo pole hiyo ni lazima we achaa tu one remember fat joe song is one not 2 or 3
 
Anaweza kuteketeza kila siku lakini sio moto wa mapenzi ulio moyoni mwake.
Anaweza akawa na picha na kadi lakini asiwe na issue yoyote na huyo demu.

Na mkewe akileta kisirani tu, jamaa atamwambia ex wake na watalianzisha kikweli.
Sasa anahifadhi hizi picha za nini?
 
huyo jamaa hamtendei haki kabisa mkewe...hakuna kitu kinawauma wanawake kama hicho....mshauri rafiki yako ateketeze kila kitu kinachomuhusu huyo ex wa mume wake
Yaani asithubutu kuteketeza bila ridhaa ya mumewe. cha kufanya ni kwamba aongee na mumewe kwa upole na ustaarabu, amwambie wazi kabisa machungu anayoyapata akikumbuka hizo picha na kila kitu anavyotunza. Wababa ni kama watoto tu, ukimwendea kwa upole anakuelewa vizuri kuliko ukimjia kwa ukali, tena atasababisha ahamishie mawazo yote kwa huyo x wake
 
Simple. The first cut is the deepest.... Inawezekana hata yeye mwenyewe anahifadhi picha unconsiously. Human beings have been made with one weakness - of attachment, to things, people, memories etc
 
Leo nimegundua kuwa ww ni bibie. Kuhusu somo, inauma lakini yale mapenzi ya kwanza yana mengi sana ya kukumbukwa. Ukiona mtu hachomi usimlaumu, cha msingi usimchokonoe
 
Simple. The first cut is the deepest.... Inawezekana hata yeye mwenyewe anahifadhi picha unconsiously. Human beings have been made with one weakness - of attachment, to things, people, memories etc

l like your comments,
most of your comments says something
about how smart and knowledgeable you are.
 
contentious issue...but whether or not one has physical memorabilia of their past lovers......whats in the heart can never be erased. mwmabie hata zikichomwa yaliyo moyoni mwa huyo bwana hawezi kuyafuta... ndio ukubwa huo. i still have memories that send shivers down my spine and others that make me smile!
 
Mhhh! Shishi...it seems that he was very very special to you. Binadamu tunatofautiana wengine hawaoni tatizo ya kuendelea kuziweka na wengine hawataki kabisa ziendelee kuwepo. Namjua jamaa aliyeomba zihamishwe nyumbani kwa binti badala ya kwao maana binti alikataa kuzichoma.
 
Asivichome,avumilie angempenda zaidi office mate wake si wangeoana?
 
Jamani watu kama hawako tayari kuoa si waache? iweje umtese mkeo kwa vipicha tu kama kweli unampenda? i dont get it, sasa kama moto wa mapenzi hauzimwi kwa kuchoma memories hizo si asingefunga ndoa? hii ndo inafanya niamini kuna ndoa nyingi hufungwa kwa conviniences but not love. May be unaolewa au unaoa huyu kwa ajili ya pesa, status, etc but unaempenda mwingine.
 
Leo nimegundua kuwa ww ni bibie. Kuhusu somo, inauma lakini yale mapenzi ya kwanza yana mengi sana ya kukumbukwa. Ukiona mtu hachomi usimlaumu, cha msingi usimchokonoe

Sijakupata hapa.Kwanini unasema hivyo na kwanini unataka kujua jinsia yangu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom