Regia Mtema
R I P
- Nov 21, 2009
- 2,970
- 864
Kuna rafiki yangu mmoja, analalamika na kuhuzunika kuwa mume wake bado anamiliki picha,maua,kadi na hata mashairi ya mapenzi aliyokuwa akitumiwa na mpenzi wake wa zamani.Huyu binti yuko kwenye ndoa kwa mwaka wa tatu sasa. Hivi vitu ni vya mpenzi wake wa zamani ambaye waliachana kabla ya kuwa na huyu rafiki yangu.Rafiki yangu huyu roho inamuuma kwani anahisi mumewe huenda akawa bado anampenda huyu mnyange wake wa zamani,anasema amevumilia sana.Mbaya zaidi mumewe na huyu mpenzi wake wa zamani wanafanya kazi ofisi moja hivyo hukutana karibu kila siku.
Hivi hii imekaaje,je huyu jamaa ni kweli bado anampemnda huyu mpenzi wake wa zamani?je binti avichome moto hivi vitu?
Hivi hii imekaaje,je huyu jamaa ni kweli bado anampemnda huyu mpenzi wake wa zamani?je binti avichome moto hivi vitu?