Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 75,227
- 157,421
Kama uko kwenye mahusiano ambayo yana kimoja kati ya haya, haraka sana jitoe, okoa muda wako na upendo wako unaopoteza:
1.Kama uko kwenye mahusiano na mwenzio anataka umvulie nguo ndio atajua kuwa unampenda! Hapa hakuna upendo bali tamaa mbaya, mtu wa aina hii hana malengo na wewe, anautaka tu mwili wako, akishakujua atakuacha na machozi yako!
2. Kama uko kwenye mahusiano, halafu ukimwangalia mwenzio mipango yako na yake ya kesho (future) hamwendani; yaani wewe unakwenda kulia na yeye anakwenda kushoto, hapa hakuna umoja, haitawezekana kuwa pamoja, kila mtu ana chake hakikisha mtu uliyenaye mnakwenda njia moja "watu wawili hawawezi kwenda njia moja wasipopatana"
3. Kama uko kwenye mahusiano kwa kumwonea mwenzio huruma, lakini si kwakuwa unampenda na unaona picha ya wazi kuwa pamoja milele, achana naye mapema! Ndoa haijengwi kwenye huruma bali upendo na upendo si ujinga/ upofu.