Mpenzi wa mbali ukisema hakusaliti itakuwa unajipa moyo tu

The king mswati

JF-Expert Member
Jun 20, 2020
787
820
Naandika haya kwa hisia za maumivu makali sana ila ukweli ni kwamba "Ukiwa na mpenzi wa mbali alafu ukajiaminisha kuwa hakusaliti huko aliko basi utakuwa unajipa moyo tu ila uhalisia siyo huo "

Sijui niseme nina mpenzi au nilikuwa na mpenzi (maana hata haijajulikana tumeachana au bado) ila iko hivi :

Nina mwanamke ambaye alikuwa kama mchumba ingawa hatujatambulishana kwa wazazi bado. Yeye nilimwacha Arusha na mimi nikaja kutafta riziki huku Zanzibar (kuna chaka la ajira nilipata). Hivyo nikawa mbali naye ni kama mwaka na nusu hivi.

Katika kipindi hiki tulichokuwa mbali tulikuwa na panda shuka nyingi sana katika mahusiano yetu (tumeachana na kurudiana kwa vipindi tofauti tofauti).

Mwezi Aprili mwaka huu tuliachana kimwisho mwisho tukakubaliana kila mtu achukue time yake na maisha yake. Kumbe yeye alitamka hivyo kwa hasira tu ila moyoni hakumaanisha.

Kumbe kipindi chote hiki akawa anasubiri nimtafte lakini mimi ‘nimekula buyu’. Akawaagiza watu kadhaa kuja kuniambia kuwa bado ananipenda na hawezi olewa na mwanaume mwingine and son on lakini mimi sikumtafuta wala.

Basi mwezi jana (mwezi Septemba) uvumilivu ulimshinda kanitafta akanambia “mimi bado nakupenda naomba tu turudiane and son on”. Nilimkubalia maana nikikumbuka tushapita mapito mengi sana ya panda shuka nikiwa naye.

Sasa picha linaanza juzi kati (siku 3 zilizopita) kuna binamu yangu mmoja hivi yupo huko Chuga alikuwa na shida ya dawa (Maana huyu dada anauza duka la dawa alisomeaga nursing). Ikabidi amcheki shemeji yake kuwa ana shida na dawa fulani. Akamwambia hapa dukani kwangu hamna ila njoo nije nikupeleke mahali ninaponunuaga kwenye maduka ya jumla.

Binamu akaenda kamfata na boda hadi kwake wakaenda huko kwenye maduka ya jumla. Kwa mujibu wa binamu anasema walienda kwenye phamarcy moja hivi wakamkuta daktari ambaye alikuwa mshikaji halafu huyo daktari kamwambia mpenzi wangu “hizo dawa hazipo hapa mpaka nyumbani”

Cha kushangaza ni kwamba huyo daktari alimpa mpenzi wangu funguo wakaondoka na bro hadi nyumbani kwa daktari kuchukua dawa na walipofika anadai mpenzi wangu alionekana kuwa mwenyeji humo ndani (nyumbani kwa daktari) akachukua dawa wakarudisha funguo.

Swali ninalojiuliza ni huyu mpenzi wangu amepajuaje kwa daktari mpaka akampa na funguo akachukue dawa (kitu kinachomaanisha tayari ni mwenyeji hapo) kama hawana mahusiano naye? Maana hawaishi mtaa mmoja, na hawafanyi kazi pamoja!

Nimebaki na maswali mengi sana, kwa mazingira kama hayo yananipa ushahidi kuwa yule daktari atakuwa anamla mpenzi wangu.

Kingine kinachonipa ushahidi zaidi ni kwamba baada ya kuchukua dawa walipomrudishia daktari ule funguo broo anadai daktari alimuuliza "Unanipa funguo kwani leo hulali huku?” Mpenzi wangu akajibu “Hapana leo silali nilimuaga mama kuwa nitarudi mapema”.

Inaniuma sana japo sina ushahidi wa moja kwa moja kuwa analiwa lakini kwa mazingira hayo hata kipofu ataona kuwa hapa naibiwa. Jana nimuuliza kuhusu hilo suala kawa mkali hataki kulizungumzia na anasema niache kusikiliza maneno ya watu.

Imeniuma sana na mpaka sasa nimeshindwa nimuhukumuje maana najikuta nina stress hadi nashindwa kulala wala kula. Narudia tena "Ukiwa na mpenzi wa mbali halafu unasema hakucheat basi utakuwa unajipa moyo tu"
 
Acha kujitesa mwenyewe hapo ni wazi kuwa huyo sio wako na ameshajua udhaifu wako kuwa unampenda sasa wewe endelea nae hayo maumivu uliyonayo sasa yatazidi zaidi.
Cha kufanya jitoe mhanga hata kama moyo unampenda punguza mazoea ya kumtafuta taratibu na umuache maana yeye hana cha kupoteza huyo sio wako ikiwezekana tafuta mpenzi huko znz ulipo wahenga walishasema fimbo ya mbali haiui nyoka.
 
Mtu ukishamwekaga moyon inakuwag n ngum xan kumsahau tena ashukuru niko mbali maan ningekuwa karbu nahic xaiv ningekuw polisi tiar, kuna mda nawaza cjui nipande ndege chap kmya kimya nikatue kisongo alaf nimfate kwake kimya kimya tukatambuane vzur maan dem kuni cheat alaf nikajua naumiaga xan maan hapo naanzag kujiulza nimekosea wap, madhaifu yang nn wap 😢😢
 
Mtu ukishamwekaga moyon inakuwag n ngum xan kumsahau tena ashukuru niko mbali maan ningekuwa karbu nahic xaiv ningekuw polisi tiar, kuna mda nawaza cjui nipande ndege chap kmya kimya nikatue kisongo alaf nimfate kwake kimya kimya tukatambuane vzur maan dem kuni cheat alaf nikajua naumiaga xan maan hapo naanzag kujiulza nimekosea wap, madhaifu yang nn wap

Usijifariji mkuu hayo yote hayana maana kama hayatobadilisha ukweli, huko ni kupalilia maumivu inaonesha unayapenda maumivu sana au unadhani ukiumia sana ndio atabadilika? Badilika bro you are a man act tough ona unavyoteseka ulali kwa raha na mtu yupo makilomita mengi mbali huko.
 
Kubadilika cyo kwamba nashindwa ila ni kwamba inaweza kuchukua mda xana na hakunaga mtu anaependa maumivu, hata nikiwa na dem mwingine leo hapa bado tu akili yangu itamuwaza yeye kwanza
 
Kubadilika cyo kwamba nashindwa ila ni kwamba inaweza kuchukua mda xana na hakunaga mtu anaependa maumivu, hata nikiwa na dem mwingine leo hapa bado tu akili yangu itamuwaza yeye kwanza

Move on mkuu kama unaweza badilika anza sasa.
 
Utamu wa mapenzi ya mbali bhana ni selfie tu hapo tu ndipo nayapendea Mimi,

Pole mtoa mada jikaze uachane nae 'xaxaiv' unaandika kivulana hivyo ukitegemea demu akutunzie chiu yake,, weee thubutuu mi ukiniandikia hivyo vixaxa vyako nakunjwa dakika hiyo hiyo na nakuacha mazima,
 
Kinachokuuma ni Nini Sasa hapo ? Kwani ni mkeo ,au umetoa mahari ?
Je ,unafikiri Kuna mwanamke ambae haliwi pembeni / kucheat? ,Unajua vijana mnajidanganya Sana ,as long as yy pia ni binadamu so Kama analiwa ,kazi yako ni kumrekebisha asiliwe Sasa ,

Hakuna mtu asie na mapungufu chamsingi ni kuonesha uwanaume wako kukabiliana na situation,napata mashaka pia aina gani ya mume unaenda kuwa kwake Kama ndo unalialia huku Kama watoto wa form 4 ,
 
Mtu ukishamwekaga moyon inakuwag n ngum xan kumsahau tena ashukuru niko mbali maan ningekuwa karbu nahic xaiv ningekuw polisi tiar, kuna mda nawaza cjui nipande ndege chap kmya kimya nikatue kisongo alaf nimfate kwake kimya kimya tukatambuane vzur maan dem kuni cheat alaf nikajua naumiaga xan maan hapo naanzag kujiulza nimekosea wap, madhaifu yang nn wap
Kwenye biashara ya madawa na vipodozi kuna magendo sana yaani kuna dawa hazitakiwi kuonwa na wakaguzi ila wateja wanazihitaji sana kwa hiyo fanya kama alienda tu stoo ya siri.
Unakosea kujiuliza ulikosea wapi,itakuumiza zaidi we Fanya ni umalaya wake na nyege mshindo ndio vimesababisha.
 
Hilo najua na hizo dawa zilikuwa za magendo kweli (Za abortion) ndo maana ziliachwa maskani, lakini Je huyu demu imekuwaje akaenda yeye kwenye geto la mwanaume kama hilo alafu akaonekana ni mwenyeji si mara ya kwanza ? Alafu ilikuwaje wakati anarudisha funguo jamaa anamuuliza kwani leo hulali huku mbona unarudisha funguo ? hapo tu ndo wasi wasi wangu mkubwa sana kwamba nachapiwa😥
 
Back
Top Bottom