Mpenzi/mume/mke wako anahusika vipi na usafi wa maliwatoni..??

Mother Confessor

JF-Expert Member
Jan 7, 2016
18,596
45,225
Natumai mu wazima wa afya,.

Kama tunavyofahamu umuhimu wa maliwato kwa maisha ya binadamu,ili ubinadamu ukamilike huna budi kupata haja ndogo na kubwa na wote 'twajua usipopata hivyo vitu hata kwa siku mbili tuu nanga inavyopaa unaweza tamani kufa kwa muda...hii nikuonesha umuhimu wa kupata haja na kuwa na sehemu husika ya kwenda "kuinjooi"
Sasa basi,mimi hii sehemu buana nina ithamini sana hasa kwa kuweka mazingira yake safi,nina hakikisha kuna vifaa vyote muhimu vinavyohitajika maliwatoni kwa ajili ya usafi na dawa za kukata harufu zile za kukera kera....jamani "nyumba ni choo"....

Kwa wale wana-ndoa au wanaoishi na wapenzi wao tuu bila kuwa wameoana,je mwenza wako ana usafi kiasi gani juu ya kutunza maliwato??wengine hawana ustaarabu wakiingia unajua huko lazima ataacha alama za vasco da gama,unamsaidiaje mtu wa hivi au unamwambiaje??je jambo hilo la mwenza wako kutokuwa msafi maeneo hayo wewe unalichukuliaje??maana wengine hata wakienda ndogo tuu maji hawamwagi😫😫lol,.em tusemezane kwa wale wenye "eksipiriensi" ya kuishi na wenza wenye tabia hiyo ya kutojali usafi wa hayo maeneo huwa mnafanya nini au basi tuu mnaingia wenyewe kusafisha na kunyamaza kimya??

~MC~
 
UNAMAANISHA KUPAPASA KICHWA MJUSI KAFIRI ASAFISHE MTARO AU UNAMAANISHA NINI?
 
Nashukuru tunajielewa wote wawili maana hamna sehemu huwa nina kinyaa kama choo au bafu chafu, ila kwa atakae kuwa na mwenza wa hivo aongee nae tu kistaarabu kuhusu suala la umuhimu wa usafi wa maliwato...
Hata mm nna kinyaa sana aisee na hayo maeneo,yakiwa machafu kama ni asubuhi basi siku yangu yote inakuwa hafifu😪
 
Hii inanikumbusha miaka mingi kidogo...kuna sehemu nilienda kufanya kazi ya muda mfupi kama siku 7 hivi.Nikakaribishwa kwenye nyumba kubwa ila tunachangia choo kwa ndani.Na mle ndani kulikuwa na wazungu walikuwa wamekuja kutalii,lakini wote tulikuwa tunatumia choo kimoja.Asubuhi moja naingia huko maliwatoni,pakawa hapafai;harufu kali hakuna kuflashi wakati maji yanatoka 24hrs.Tangu siku hiyo nikaona hawa watu ni wasafi kwa nje tu ila kwa upande wa maliwatoni ni tatizo.
 
Hukumwambia akasafishe uchafu wake??😆
 
Du,hayo mambo ya kutolenga tundu kisawasawa,unakuta unakojoa pembeni halafu unaenda zako. Ndo mana sipendi kujisaidia kwenye vyoo vya jumuiya,
 
Back
Top Bottom