Mpenzi/Mke akisema "naondoka" mwanamme afanye nini?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,460
39,927
Imefika mahali mwanamke anasema "I'm leaving you" au "Naondoka" na anaweza hata kuanza kufunga virago na hata kukata tiketi. Je ina maana gani? Je mwanamme afanye nini? Je anatingisha kiberiti tu au ni hasira? Au mwanamme amwambie tu "nenda kwani nani kakukataza?". Hivi dada zetu wanaposema hivi huwa wanamaanisha kweli? Je mwanamme akionekana hajali kama ataondoka au la ni sahihi au ndio kutegeana...?
 
yaani mwanamke akisema anaondoka na anaanza kufungasha yaani namshaidia hata kufungasha vitu na nauli nampa maana atakuwa amenipunguzia mzigo.. wengi hujaribu kutumia njia hiyo kama kupima imani ya mwenzake ikoje kwake lakini hawaelewi wanatengeneza ufa na mwanaume anakuwa na imani kwamba iko siku mwanamke ataondoka hivyo anakuwa na utayari wa mapokeo
 
Sasa kama kakata tkt huyo anamaanisha kuwa umemchosha pengine ameshauri mpaka basi unatakiwa ubembeleze mtu mzima
 
wapo wa aina 2 kuna wanaotingisha kibiriti kwa kujua kwamba ataombwa msamaha na ndio walio wengi............wapo ambao kweli ana maanisha kutoknaa na kero anazokuwa amezipata kwa muda mrefu amevumilia lakini hakuna mabadiliko mwisho wa siku anaamua kuondoka................hapo inabidi wote kuangalia nini chanzo cha mke kutaka kuondoka
 
Mara nyingi huwa haimanishi kuondoka kweli inakuwa ni kupima upepo kama jamaa anaona umuhimu wa uwepo wako pale au laa, au anakupenda bado au hata ukiondoka poa tu!ila anakuwa bado anakupenda na hamaanishi kuondoka!
 
Mwache aende,,kama anazuga atabaki lakini kama anamaanisha kweli ataondoka!ANGALIZO:kumnyenyekea na kumbembeleza mwanamke kuna kiwango na mipaka yake.
 
Nimejifunza kitu hapa! Ngoja niendelee kurudi kila mara kwenye hii thread. Thanx MMJJ.
 
Mara nyingi huwa haimanishi kuondoka kweli inakuwa ni kupima upepo kama jamaa anaona umuhimu wa uwepo wako pale au laa, au anakupenda bado au hata ukiondoka poa tu!ila anakuwa bado anakupenda na hamaanishi kuondoka!

sasa jamaa akikuruhusu na ukaona hakuzuii wala kujali utachukua hatua gani??? huoni kama unajiweka kwenye nafasi ya kutokuaminika??
 
Inategemea kama amekuta una kila kitu lakini kama mlianza wote alifu na mna watoto na kinachosababisha yeye kutamani kuondoka na matatizo ya kawaida basi wewe ukishaona dalili hizo unapaki wa kwanza unawahi mlangoni unamwachia watoto then unamwambia na wewe unakwenda kwenu unamuachia vitu vyote kama ana akili timamu atacheka na kujirudisha ndani polepole.
 
Sisemi kwa wanaume kwani ni mara chache mwanamume husema "Naondoka" hasa katika tamaduni zetu. Lakini wapo wale wanaoishi katika nyumba ya mke, wanaweza kusema hivyo. Au wale ambao kwa kuwa hawataki mwanamke au watoto wao wataabike, wanaweza kusema "Naondoka" na wakaondoka.
Lakini hapa hasa kauli hiyo hutolewa na wanawake, na mwanamke haamki na kusema naondoka bila sababu yoyote. Kwa kawaida, huwa wamechoshwa na visa vya mume; wachache husema hivyo ikiwa wamepata wanayemhisi bora kuliko walionao. Kwa upande wangu kama mwanamume, kwanza nimejifunza kuheshimu NO/HAPANA ya mwanamke. Mwanamke akiniambia HAPANA, ninaheshimu neno lake.

Mwanamke ananiambia naondoka, ikiwa nimemkosea nitamwomba samahani kwa kosa langu na kuhakikisha ninajirekebisha, lakini katu sitomzuwia kuchukua maamuzi yake. Na ikiwa sioni kama nimemkosea, nitakachokahikisha ni kuwa hasau chochote chake ndani ili asije akajidai kurudi eti "nilisahau upawa wangu". Anaondoka na kuchuka mpaka sindano yake; kubwa nitakalohakikisha ni kumsindikiza mpaka pale nilipokwenda kumchukua. Ikiwa ni kwa wazazi/jamaa zake, nitahakikisha ninawakabidhi mikononi.
 
sasa jamaa akikuruhusu na ukaona hakuzuii wala kujali utachukua hatua gani??? huoni kama unajiweka kwenye nafasi ya kutokuaminika??
Najijua huwa sikurupuki kufanya jambo kama hili,inamaana nikifika hapo nimeshatumia njia zote na kufail na najua nikifika hapo lzm kwa mwanaume makini na anayenipenda kiukweli atashituka na kamwe hataniruhusu kuondoka badala yake atanitaka tuyaongee na kufikia muafaka!ila kama hajafanya hivyo ameniruhusu niondoke naondoka hata kama nampenda nikajifikrie upya kuhusu hiyo relation!
 
je kutumia kitisho ndo unaamini ni njia sahihi ya wewe kukuita na kukaa chini kuongea tatizo??? ina maana wewe huwezi kumwambia mwanaume ukae nae kwa ajili ya kuongea tatizo???
 
Sisemi kwa wanaume kwani ni mara chache mwanamume husema "Naondoka" hasa katika tamaduni zetu. Lakini wapo wale wanaoishi katika nyumba ya mke, wanaweza kusema hivyo. Au wale ambao kwa kuwa hawataki mwanamke au watoto wao wataabike, wanaweza kusema "Naondoka" na wakaondoka.
Lakini hapa hasa kauli hiyo hutolewa na wanawake, na mwanamke haamki na kusema naondoka bila sababu yoyote. Kwa kawaida, huwa wamechoshwa na visa vya mume; wachache husema hivyo ikiwa wamepata wanayemhisi bora kuliko waliyenao. Kwa upande wangu kama mwanamume, kwanza nimejifunza kuheshimu NO/HAPANA ya mwanamke. Mwanamke akiniambia HAPANA, ninaheshimu neno lake.

Mwanamke ananiambia naondoka, ikiwa nimemkosea nitamwomba samahani kwa kosa langu na kuhakikisha ninajirekebisha, lakini katu sitomzuwia kuchukua maamuzi yake. Na ikiwa sioni kama nimemkosea, nitakachokahikisha ni kuwa hasau chochote chake ndani ili asije akajidai kurudi eti "nilisahau upawa wangu". Anaondoka na kuchuka mpaka sindano yake; kubwa nitakalohakikisha ni kumsindikiza mpaka pale nilipokwenda kumchukua. Ikiwa ni kwa wazazi/jamaa zake, nitahakikisha ninawakabidhi mikononi.

ina maana hadi atishie kuondoka ndo utambue kosa lako na kuomba msamaha???
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom