Mpenzi anitaki tena...nifanyeje... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mpenzi anitaki tena...nifanyeje...

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by BabaTina, Mar 15, 2010.

 1. BabaTina

  BabaTina JF-Expert Member

  #1
  Mar 15, 2010
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 362
  Likes Received: 372
  Trophy Points: 80
  jamani habari za siku, mie mtanzania mwenzenu nina masaibu ya mahusiano yaliyonifika na ambayo kwa namna moja ama nyingine nimeona ni vizuri niyaweke hapa ili mradi nipate mawaidha yatakayoupoza moyo wangu.....!
  kuna binti nimekaa nae katika mahusiano kwa muda wa miaka miwili na miezi kadhaa sasa. binti huyu tulianza mahusiano kama mzaha na mwisho wake tukashibana hasaa..! kabla mie sijaanza nae mahusiano alikuwa katika mahusiano na jamaa mmoja ambaye anadahi kwamba jamaa huyo alikuwa ni mlevi kupindukia na eti maumbile ya huyo jamaa yalimshinda sana hivyo basi akaadhamia kuachana nae na kuja kwangu.
  mwanzoni mie nilikuwa sipo yatari kuwa nae katika sehemu ya maisha yangu kwani nakumbuka niliwahi kusitisha mahusiano na yeye kama mara 3 hivi katika vipindi tofauti tofauti lakini binti huyu alikuwa na moyo wa ajabu aliendelea kuwa positive kwangu hata ikanibidi nitafakari hatua yangu mpya katika maamuzi niliyoyachukua na siku moja akanisihi turudiane + takafakari zangu na wema aliokuwa akinionesha sikuona vyema kumchukua kama mpenzi wangu kwa ajili ya maisha.
  Safari ya maisha ya mahusiano yaliyoshiba ikaanza huku mie nikiwa nimemuahidi kutomwacha tena...! kusema kweli mahusiano yalikuwa mazuri sana kwani nilweza kumjua vizuri huyu binti, ni mpole , mnyenyekevu na mwenye msaada mkubwa sana wa kimawazo na material pia.
  lakini bahati mbaya ilikuwa kwangu kwani sie mahusiano yetu yalianzia chuoni then tulipoingia mtaani tukaanza mahusiano serious huku tukipena ahadi kadhaaa ikiwemo ya kuwa kitu kimoja(ndoa).
  kwa bahati mbaya ndugu zangu mie nilipopata kazi nilijikuta ni kichwa cha treni ambacho ni lazima kilitakiwa kivute mabehewa mengine....!
  nilijikuta nimezungukwa na wadogo zangu ambao kutokana na hali ngumu ya uchumi nyumbani kwetu ilibidi nitoe msaada japokuwa nilikuwa napata kipato kidogo sanaaa...
  kutokana na hali hiyo ya kutoa msaada kwa ndugu zangu nilikuwa nikiishiwa pesa yangu nyingi na hivyo kushindwa kuweka hakiba hata kidogo hivyo kabla mwisho w mwezi haujafika mie tayari nakuwa sina pesa mfukoni....!
  so, binti huyu ndiye aliyekuwa karibu yangu na nilimpa kila taarifa ya hesabu yangu niliyokuwa natumia kwangu na ndugu zangu.
  hivo basi kimbilio langu lilikuwa kwake, nilikuwa namuoba pesa kidogo nasongesha maisha na wakati mwingine ananikopa then narudisha. lakini kadri siku zilivyosonga hali yangu kiuchumi ilizidi kubana mpaka sasa naongea hali nii tait sanaaa...!
  sikujua kama hali hii ilimsononesha sana mwenzangu moyoni mie nilitambua kitu kimoja tu 'pendo la dhati..!
  jitihada nyingi nimezifanya ili kuongeza kipato lakini mtu mzima situation imegoma.....!
  Sasa siku za hivi karibuni hali ilianza kubadilika, mwenzangu alikuwa hanitumii tena msgs za kunitakia siku njema kama ilivyokuwa awali, ( Good mornig dear...nice day, Good Afternoon sweet have a nice lunch, Gud evening dear, jioni hii utakula nini..? gud 9t nice dreams n.k) zote zilitoweka ghafla...!
  nikijaribu kuumuliza kwa sms i didn't get positive reactions, so nikamwomba appointment tuonane...! akawa so bussy na kazi yake and i said ok fine.
  So one day alikuwa ananidai kiasi cha sh, laki moja akiomba nimrejeshee nikamwita shemu fulani maeneo ya ATM moja ili nitoe fedha benki nimpatia, alipokuja hakuwa na mwonekano wa kunifurahia uso kaunja na kama aliyekuwa anakwepa kunitazama machoni....!
  nikampa pesa na kumwambia kuwa mbona kanibadilikia hivyo , akanijibu kwa kuniambia kuwa atanitafuta aniambie ukweli.....! aliposema hivyo nikamwacha aende zake..nami nikabaki nimesimama lakini kabla hajafika mbali nilmfuata na kumsihi aniambie pale pale kama huu ndio mwisho wa penzi ama lah...! akasema hawezi kuzungumza pale...ok nikamwacha aondoke zake...!
  wiki ikasonga na mawazo mengi sanaaaa....then baadae akanitumia sms kunitaarifu kuwa meeting yetu itakuwa jumamosi but then the next day akasema hatutoweza kuonana nae jumamosi kwani anavikao katika hekalu analoabudu ambako huku ni kiongozi..
  nikamsihi akakataaa...! therefore ikanibidi nlazimishe nikamwambia nitakwenda kwao jioni ya siku ya jumamosi tarehe 13/03....akanisihi sana nisiende lakini nikalazimisha snaa, nikamwambia nitakwenda nitamsubiri hata pale atakapomaliza kikao chake ili anipe hatma ya mahusiano yetu.
  alinipigia simu mara 2 akiniomba nisiende home, lakini mie ilipofika jioni nilienda maeneo jirani na home kwao nikamsubiri hata ilipofika saa 2 usiku akawa maeshindwa kutoka kwao ikabidi nisogee maeneo ya karibu na kwao.....
  thanks God akaja tukaanza kuongea nikamuuliza mbona hivyo mwenzangu umebadilika sanaaaa....hakutaka kuniambia mwanzoni lakini baadae ikabidi aseme na aliniambia maneno haya........KUSEMA KWELI ....(anataja jina langu)...MIE SIKU HIZI MAPENZI YANGU KWAKO YAMEPUNGUA SANA'
  Kisha akataja sababu zifuatazo kama chanzo cha mapenzi kupungua

  1. Lifestlye yangu si nzuri ( ..yaani kila nipatapo kipato changu pesa yote uigawa kwa ndugu na kusahau kuwa mie mwenyewe nahitaji kuishi..)
  2. Dini.....( mie na yeye tu dini tofauti)
  3. frastuation life toka katika familia yake( kuna migogoro ambayo hakuitaja)
  hizo ndizo sababu alizozitaja hasa....!

  1. niliumia kwa sasbabu kuishiwa kipato sikufanya kusudi siku zote kwani hao wadogo zangu naowapatia nawashuhudi mbele yenu kuwa walichangia kunisome elimu yangu ya kidato cha tano na sita na baadae chuo. sasa wao wanasoma je niwatose....! kwangu si uungwana kabisa ndio maana nilikuwa natoa kila nilichonacho kwa ajili ya wema walinionifanyia
  2. Dini zetu kweli ni tofauti lakini mapenzi yangu ya dhati yamenifanya nisione dini kama kikwazo cha mie kuwa nayeye.....kwani nashuhudia kuwa baba na mama yangu leo hii wana maiaka 33 ndani ya nyumba wakiwa na dini tofauti kabisa, then my father katugeia uhuru wa kuchagua dini tunayoitaka na tunamwabudu mungu katika misingi ya sheria zake...!
  3. kuhusu familia yake siwezi sema lolote kwani sijui kinachoendelea huko......
  Sasas ndugu zangu naomba ushauri wenu nifanyeje kwani dada huyu amesema mapenzi yamepungua na ni kweli hatuna tena mawasiliano ya sms kama mwanzo
  lakini ukweli ni kwamba nampenda sanaaa, pili ndugu na jamaa ambao tayari walikuwa wanamfahamu hawatanielewa mie kwani walikuwa wanamuamini sana kwa tabia yake nzuri...
  Je, nifanyeje..? ninao ushahidi wa mazungumzo yangu na yake ambayo wakati tunaongea nilikuwa narekodi lakini yeye alikuwa hafahamu kama nafanya hivyo itakapo bidi nitayaweka hapa japokuwa yanasikika kwa mbali kutoka na sababu kuwa eneo tulilokuwepo kulikuwa na genereta mabayo ilikuwa ikinguruma sanaaaa....
  endapo itabidi nitaipost hiyo saund clip hapa siku ya kesho... tafadhalini nishaurini nifanyeje binti huyu nampenda...sana
   
 2. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #2
  Mar 15, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Pole sana!

  Kama kweli anakupenda ; hizi sio sababu za kuyaua mapenzi yenu!

  Hilo suala la ndugu si mgeni nalo na lazima atambue kuwa wewe unawajibika kwa jamaa yako na kiukweli ndio maisha ya familia nyingi sana za kiafrika! basi angekuja na njia mbadala yakutatua labda kuanzisha mradi wa pamoja utakawaowasaidia kuendesha maisha na kutoa msaada maana vitu kama elimu haviwezi kusubiri ni kama mlo!

  na suala la dini ndio kabisaaaaaaaaaa; halina mashiko kwenye mapenzi; wife mie alibadili pasipo hata kumwambia wala kushinikizwa nami nilikuwa nimeafiki tubaki na dini tofauti mapaka wakati muafaka ; kwani nilikuwa nimetendwa sana na hao niliokuwa nao dini moja kabla yake yeye! Hivyo si kikwazo kwa watu wenye nia moja na thabiti!

  Mie nikupongeze kwa kujitolea kwako kuwasaidia nduguzo; kwa uwezo ulionao! Unastahili kuigwa na vija wa kileo amabo wanaishia kutanua mijini wakisahau kabisa ndugu zao; na unaposaidia elimu unaendeleza taifa letu hivyo wewe ni mtanzania wa kuigwa!

  wala usione aibu kuishiwa na usiingie tamaa ya kujiongezea kipato isivyo halali; karibu kule kwa wajasiriliamali utapata mbinu nyingi tu!

  Huyu mpenzi wako mweleze jinsi ulivyoumizwa na umwache yeye aamue; usimshinikize na umshukuru mungu kwa lolote atakaloamua!
   
 3. m

  mungiki2 Member

  #3
  Mar 15, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani mi sifikiri kama ni sahihi kumhukumu huyo dada. Kulingana na maelezo aliyotoa inawezekana kweli swala la dini ni tatizo kwa familia yake si kwake tu.Na katika hali kama hiyo afanye nini kama wazazi wameonyesha kutokubali?
   
 4. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #4
  Mar 15, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  maskini BabaTina nitakuja baadae hapa!
   
 5. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #5
  Mar 15, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  summary bana
   
 6. BabaTina

  BabaTina JF-Expert Member

  #6
  Mar 15, 2010
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 362
  Likes Received: 372
  Trophy Points: 80
  Thanks everybody @ maskini jeuri wapi hapo wanapotoa elimu ya ujasiriamali nami nijiunge
   
 7. Sydney

  Sydney Senior Member

  #7
  Mar 15, 2010
  Joined: Nov 10, 2009
  Messages: 154
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Du, jamani pole sana baba Tina, lakini haya yote ndio maisha. Na wanaposema maisha ni safari ni kweli, na safari ina kila aina ya kashi kashi, raha, karaha, n.k Mimi kwa matazamo wangu naona ni vizuri ukichukua maamuzi ya busara, maana shida na raha ni sehemu za maisha, mpe muda kama kweli ana yanayomsibu basi kuna siku atakujia na mtaweka mambo yenu sawa, kama kweli anakupenda. Na kwa upande wa ndugu zako waeleze ukweli tuu, na waombe wakupe muda, nina hakika mtafikia mahali pazuri mlikokuwa manaelekea awali. Pole sana, imenisikitisha!
   
 8. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #8
  Mar 15, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,263
  Likes Received: 21,996
  Trophy Points: 280


  You are intelligent, and know what's right. You like to make things go your way, which can sometimes cause trouble for not thinking about other people's feelings. But you be patient when it comes to love.. Once you get a hold of the right person, it's hard for you to find a better love.

  __________________
  There is a drop of Greatness in every Man!!

  Last edited by Kimey; Today at 01:23 PM..


  [​IMG]
  Kimey
  JF Senior Expert Member
  [​IMG][​IMG][​IMG][​IMG] [​IMG] [​IMG]
  Join Date: Wed Mar 2009
  Posts: 584
  Thanks: 160
  Thanked 171 Times in 126 Posts


  [​IMG] Report Post [​IMG] Subscription [​IMG] Show Printable Version [​IMG] Email this Page [​IMG] Add to Kimey's Reputation
   
Loading...