mpeni ushauri......ungekua wewe ungefanyaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

mpeni ushauri......ungekua wewe ungefanyaje?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by vkeisy2006, Apr 21, 2010.

 1. vkeisy2006

  vkeisy2006 JF-Expert Member

  #1
  Apr 21, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 230
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45
  Kuna kitu kinanichanganya sana, hakinihusu mimi lakini kinawahusu watu muhimu sana kwangu, nina marafiki wawili, na ni wamama wenye familia zao na nimajirani zangu, ss mmoja kati yako anatembea na mume wa mwenzie wakati wote wawili ni mashoga zangu, ila huyo anaeibiwa hajui kama huyu rafiki yangu mwingine anamchukuwa mumewe, na huwa anamchekea kabisa na kujifanya rafiki yake, wanaongea vizuri sana,  Nilishawahi kumuonya huyu rafiki yangu, kwanza ukizingatia sisi ni majirani, pili huyu akisha kuja kujuwa itaniweka mimi pabaya sana, naona bora hata asingeniweka wazi juu yahili maana linaniumiza sana, kwakuwa huyo mwanaume ameshanogewa na penzi la nje, ameshaanza kujisahau, anamtesa sana mkewe , anampiga sana, anatishia kumfukuza, kitu kidogo tu kwake linakuwa kubwa, huyo dada huwa akipigwa na kufukuzwa anakuja kwangu, akifika kwangu anajieleza sana, na kusema nahisi mume wangu ana mwanamke mwingine,

  maana mwanzo hakuwa hivi, anachowaza ni sahihi na mimi nalijuwa hilo, kinachoniuma zaidi sikumoja alipigwa sana mumewe usiku, akakimbilia kwangu, akamkuta na huyu mwizi yuko kwangu, akaanza kutueleza, nilimuhurumia sana, nikamwambia vumilia tu! lakini huy mwenzangu ambae ndie muhusika wa tukio, akawa anamshauri aondoke, aliniudhi sana na huwa namsema sana, lakini hasikii, najuta kwanini nimelijuwa hili, bora ingekuwa siri yao tu!

  sasa kumwambia kuwa chanzo ni fulani, nashindwa maana wote ni mashoga zangu, Sasa hebu nishaurini, nimwambie tu liwalo na liwe, au nitaitwa mmbea niwaache tu mwenzie huku pembeni anajifanya anampenda, inaninyima raha sana hii. ​
   
 2. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #2
  Apr 21, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  hayakuhusu mama!......
  kauka
   
 3. Akili Unazo!

  Akili Unazo! JF-Expert Member

  #3
  Apr 21, 2010
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 2,832
  Likes Received: 2,546
  Trophy Points: 280
  Kwa kweli wewe pia una tabia mbaya sana kwa nini unaendekeza tabia mbaya kama hiyo kwa nini usiwakutanishe na kuwambia tabia zao mbaya au na wewe unachukuwa mume wa mtu.

  Mfano ndo wewe unafanyiwa hivyo ungejisikiaje kama huyo mwizi hakuelewi achana naye na vunja uhusiano naye.
   
 4. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #4
  Apr 21, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,037
  Trophy Points: 280
  pole shost kwa kweli upo katika hatari kubwa sana, ukisema umwambie mwenye mume unaweza kuwa chanzo cha kuvunjika kwa ndoa ya watu, wewe cha kufanya kata mawasiliano na huyo mwizi tena ikibidi umpige marufuku kuja hapo kwako maana mwenye mume akijua atajua mko njama moja na mnamsanifu, na usitake nae mazoea tena, muachie mwenye mume ajue kwa njia nyingine ili wewe uwe safe side......ni mtihani mkubwa sana huo
   
 5. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #5
  Apr 21, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,582
  Likes Received: 545
  Trophy Points: 280
  Pole lakini huyu mwanamke mwingine mwenye kuiba mme wa mwenzie unatakiwa umfanyie cancelling aachane na mme wa mwenzie kama anaona raha iko siku atajutia
  Mbona anatabia chafu sana ..na amewezaje kuwa rafiki yako..mwambie unakereheka na tabia zake chafu utamwambia mmewe kuhusiana na hili
  Ila ingekuwa mie ningempiga stop kuja kwangu naona wewe una -mu-Entertain kwa nini????????????
   
 6. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #6
  Apr 21, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  punguza umbeay we mama............ kila siku wakikosana wanakuja kwako umejifanya hakimu wao sio?? ao we ndo mzee wa busara hapo mtaani kwenu??........... visa vingine bwana...........acha kuchonganisha nyumba za watu........... one and the only one ushauri............. achana na hao akina mama , zungumza na hilo dume la mbegu........... mwambie unajua siri yao na kama hataki kuiacha basi asimpige mkewe kwani akiendelea kuwa anampiga mkewe, utayasema yote kwa mkewe na utatoa ushahidi popote utakapotakiwa kufanya hivyo pamija na mifano hai/vielelezo kwani vyote unavyo..........

  ila achaa umbeya.................. utavunja nyumba za watu..............
   
 7. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #7
  Apr 21, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,037
  Trophy Points: 280
  kweli hata mimi nimejiuliza, coz mtu wa aina hii anaweza hata kukutoa roho
   
 8. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #8
  Apr 21, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,037
  Trophy Points: 280
  mmmhh!!
   
 9. D

  Dina JF-Expert Member

  #9
  Apr 21, 2010
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 2,824
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Mpendwa, kwani una deni kubwa na huyo 'mwizi' kiasi kwamba huwezi kuachana naye? unless hiyo tabia haikukeri. Cha msingi achana naye tena mpige marufuku kuja kwako na sababu ya kufanya hivyo uiweke wazi kabisa. Kwa sababu mateso ya ndoa sio madogo, sasa sembuse hayo ambayo chanzo chake kinajulikana, na yanafanyika kwa mtu wako wa karibu, hebu act now bwana umpe ahueni rafiki yako!
   
 10. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #10
  Apr 21, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,582
  Likes Received: 545
  Trophy Points: 280
  Ni kweli Preta sidhani kama wewe unaweza kuwa na rafiki mwenye tabia chafu kama hizo na mkadumu mommy sasa huyu mwenzetu sijui??sipati jibu
   
 11. RR

  RR JF-Expert Member

  #11
  Apr 21, 2010
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,720
  Likes Received: 206
  Trophy Points: 160
  Wewe una mme? Usishawahi kujiuliza kama hakuibii wewe pia?
  BTW: Kama mimi si mwizi siwezi kuwa na rafiki mwizi. Birds of the same feather.........
   
 12. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #12
  Apr 21, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  KUWA mkweli na utakuwa huru na kujisikia wepesi na utaondoakana na msongo wa mawazo. Pia utasaidia kumkomboa mwanamke mwenzako anayeteseka wakati wewe upo ktk nafasi nzuri ya kumsaidia. Huwezi kumfurahisha kila mtu chini ya jua. Korokwini ni chungu japo ni dawa.
   
 13. SHUPAZA

  SHUPAZA JF-Expert Member

  #13
  Apr 21, 2010
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 548
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ukweli ni kwamba mwizi ni mwizi tu kama mpango wa kumuiba mume wa shoga wako ukifeli hujue atakuibia wewe wizi ni tabia kama anayo lazima atakudhuru wewe sasa nakushauri ndugu huyo mkatae vunja ushoga nae atakuumiza na wewe
   
 14. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #14
  Apr 21, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Kwanini una linda urafiki wako na mtu mshenzi? Kuna faida yoyote unapata kutoka kwake?
   
 15. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #15
  Apr 21, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  yaani wanawake jamani tuna kuwaga na vijimamabo vya ajabu sana, sasa wewe umeolewa unamharibia mwenzio nyumba yake na zaidi unamshauri aondoke cjui kitu gani,sasa akiondoka na yeye ataacha ndoa yake aingie kwenye hiyo aliyoiharibu? hapo ndio ninapochoka unafiki wa "kike"...napendaga sana kuwashauri wanawake wenzangu kwenye ndoa zao wakipata purukushani waangalie ni nani na nani wa kumweleza, yaani ni kutafutiana uhasama tu huku, mie cjui hata nielezeje mana ingekuwa ni me cku nikijua lawama ni kwenu wote wa3...mume wangu, huyo mwizi wangu na wewe vkeisy mana wote mnani enjoy....sasa ni bora wewe vk ujitenge na huyo mharibifu mapema.
   
 16. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #16
  Apr 21, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0

  hapo sasa, na huyu dada anaeteseka sasa hivi mara ghafla akija kujua na anakumbuka alikuwa anaenda kwa huyo vk kumlalamikia na vk anajua kinachoendelea sema ni kumpooza"vumilia"...vumilia wakati unajua kinachomla/mmaliza?...bwana wanawake tuna mambo magumu mno....sasa akijua ndio utaanza kumwambia ooh rafiki yangu cjui pole cjui sorry nilishindwa kukuelezea coz kimepanda kimeshuka....ctakuelewa mana ni full" unafiki" na nitahic nawe ulikuwa unafurahia mateso yangu, haki ya nani wacheni tu, unacheka nao na wabaya ni hao hao.
   
 17. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #17
  Apr 21, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0

  hawa wote wa2 wanamu enjoy mwenzao tu, hakuna lolote hapo.
   
 18. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #18
  Apr 21, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Kama una uhakika rafiki yako ndo anasababisha hii ndoa iende mrama, ni bora umvalie uso wa mbuzi na kumwambia hadharani, ikimtishia kuwa asipoacha utamwambia shoga anaeteswa!...Vinginevyo wewe unafuga ubovu sana, na kwa hilo utahukumiwa!..Wewe ushaonyesha kuwa humpendi kabisa huyo mdada anaeteswa, na uko na yule mwizi...Vibaya sana hivyo!
   
 19. father-xmas

  father-xmas JF-Expert Member

  #19
  Apr 21, 2010
  Joined: Mar 23, 2010
  Messages: 530
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  usimchekee mwizi huyo mama wala usimuite shoga yako......,si mtu mwema kama anamtenda mwezio ujue na wewe hashindiwi kukutenda unless mnafanana tabia.....mfukuze asije kwako na umtishie utasema....sawa mrembo
   
 20. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #20
  Apr 21, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Jamani hii dunia ina kila aina ya vituko..huyu mamam hafai kabisa..yaani maeshindwa kutafuta wanaume wengine?
   
Loading...