Mpendwa Lulu: Nakutumia waraka huu kwa hayo yaliyokupata!!

Anold

JF-Expert Member
Jul 15, 2010
1,456
614
Lulu mpedwa pole kwa hayo yaliyokukuta.

Pamoja na ukweli kuwa yakujitakia hayana majuto bado nimeona nikuandikie kukupa pole. Nakupa pole kwani nafikiri hili hukuwahi kuliwaza kuwa linaweza kukupata kutokana na ukweli kuwa kwanza wewe bado ni mdogo na maisha yameanza kukunyookea ukiwa bado mdogo kiasi cha kukufanya usijue hatari na vipingamizi mbalimbali vinavyoweza kukupata katika harakati za kutafuta maisha ya baadaye, pole sana dada.

Kwakuwa kwa sasa upo mikononi mwa vyombo vya sheria ili kutoa ushirikiano kwa hilo lililotokea maana kwa kiasi kikubwa naamini unajua ukweli wa jambo hilo, mimi kubwa langu ni kukutakia kila lakheri ili ikiwezekana urudi tena uraiani na kuendelea na maisha yako ya kawaida.

Hata hivyo napenda kukushauri kuwa hili lililotokea ni funzo kubwa si kwako tu ila kwa watu wote ambao wametafakari kwa kina tukio hili kwa upana wake, mara kadhaa nimekuwa nikisoma kwenye vyombo vya habari watu wakikupinga kujihusisha na mambo ya anasa na kwa masikio yangu nimewahi kukusikia ukiwapinga na kuwaona hawakutakii mema kimsingi watu wale walikuwa wanajaribu kutoa tahadhari si kwako tu ila kwa kila mtu mwenye umri kama wako kuacha kujihusisha na mambo ya starehe za kupindukia, Kuna baadhi ya tungo za wasanii zinasema ''starehe hazina mwisho" nataka nikuhakikishie mdogo wangu kuwa starehe zina mwisho na mara nyingi mwisho wake huwa mbaya sana.

Kama utafanikiwa kutoka kwenye janga hili, nakusihi uwe balozi mwema wa kuwashawishi hata wenzako wenye umri kama wako waone faida za kuwa watulivu, na kuishi maisha ya uadilifu na kutii maonyo ya wazazi, viongozi wa dini na jamii kwa ujumla. Maisha ya mahangaiko yana hatari nyingi na balaa nyingi, watu wengi ambao wameshindwa kutulia na kuendesha maisha ya kiistaarabu wamejikuta wakijiingiza kwenye shida na majanga ambayo huenda yasingekuwa na sababu yatokee, hili ni muhimu sana ulizingatie maana ''mtoto wa tajiri akionywa mtoto wa maskini tega sikio" pia unaelewa wazi kuwa "mchuma janga hula na wakwao". Pole sana dada yangu, ningekuandikia mengi ila naona nisikuchoshe upumzike kwani hili nililokukuta kwa vyovyote litakuwa limekuvunja sana moyo na kukutia simanzi, kwa vyovyote vikao vya bunge lisilo rasmi kichwani kwako litakuwa likikuyumbisha kwa maoni na kukutaka utoe miongozo itakayosaidia kuondokana na hii dhahma, jitie moyo, inawezekana wanadamu wasitake kukuelewa ila nakuhakikishia hapo ulipo ukimwita mola wako kwa uaminifu yeye atakuelewa tu na anaweza kabisa kukuepusha na janga hili pole sana Lulu.
 
wanajf nani amepata jina la mtu maarufu aliyempigia simu lulu usiku akasababisha msiba wa kanumba?kwani nasikia eti baada ya lulu kumtaja na akammthibitishia kanumba kwali ni mpenzi wake ndo maana jembe akakasirika saana...
 
well said and presented ila believe me...hawa wasanii wetu hawa hakuna atakayebadilika. mtaniambia baadae
 
kila mtu atabeba msalaba wake, majuto mjukuu ati , vitot vya umri wake vipo vinasoma "how europe underdevelop africa " yeye navuna alichopanda.. TUJIFUNZE , TUJIFUNZE , TUJIFUNZE kutoka kwenye hili tukio JAmani
 
Kwa jinsi orodha ya walioshiriki kulimenya chenza la Lulu inavyotisha na hasa ukizingatia nyazifa wanazozitumikia huko waliko nina mashaka kama Lulu atapatikana na hatia. Hapa ni sinema tu inayoendelea subiri part 2 mahakamani
 
Uongo dhambi SK alikua anamfaidi Lulu mbhaaaya!! .........
 
Natumaini hata Lulu asipopata, the likes of LULU somehow watakuwa wamepata. Ni maneno makali sana ambayo ukiyatafakari kwa undani unajua yanatugusa wengi! Thanx pal
 
wanajf nani amepata jina la mtu maarufu aliyempigia simu lulu usiku akasababisha msiba wa kanumba?kwani nasikia eti baada ya lulu kumtaja na akammthibitishia kanumba kwali ni mpenzi wake ndo maana jembe akakasirika saana...

anaitwa papa ya kutomboka mutu ya mindombolo ya solo...
 
wanajf nani amepata jina la mtu maarufu aliyempigia simu lulu usiku akasababisha msiba wa kanumba?kwani nasikia eti baada ya lulu kumtaja na akammthibitishia kanumba kwali ni mpenzi wake ndo maana jembe akakasirika saana...

Kweli jamani tupeni jina la huyo mpenzi wa lulu aliyesababisha kifo cha lulu, kwani lulu kama lulu ahajasabibisha umauti wa kanumba bali hiyo njemba iliyopiga simu
 
Kweli jamani tupeni jina la huyo mpenzi wa lulu aliyesababisha kifo cha lulu, kwani lulu kama lulu ahajasabibisha umauti wa kanumba bali hiyo njemba iliyopiga simu
Mbona wasema kifo cha Lulu, kwani Lulu amekufa lini jamani?
 
Huyu Lulu si ndo nilisomaga kwenye magazeti ya Shigongo kuwa yuko busy anasimamia nyumba yake kimara. Na wakaendelea kusema eti anajengewa na mbunge mmoja wa CCM mwenye umbo kuubwa. Kama ni kweli basi mbio za sakafuni uishia ukingoni. Maisha si kutegemea uzuri ndo uwin mabinti zetu hawa inabidi wajue wala si dili kutegemea mwili kusafisha jina mujini.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom