Mpende au Mchukie, Mugalu ni msaada mkubwa sana Simba

Mchochezi

JF-Expert Member
Feb 29, 2012
10,413
6,569
Chris Kope Mushimba Mugalu ni straika ambaye tangu aje Simba amekuwa katika lawama na shutuma za kiwango chake, imefikia hatua hata mashabiki wake hawampendi.

Ila jamaa ni bonge la straika, anapokuwepo kwenye timu anafanya wachezaji wa timu pinzani kuanzia watatu hadi wanne wasipande mbele kwa ajili ya kumpinda yeye.

Hiyo inatoa ahueni kwa timu Simba kucheza kwa utulivu kwa kuwa wanakuwa wamepinguziwa idadibya wachezaji wanaowashambulia.

Leo amekosekana umuhimu wake umeonekana, Bocco akaishia kulikimbia eneo la 18 na kuwaacha mabeki wa Jwaneng Galaxy kupanda kadiri watakavyo, na kusababisha kupanda ushindi.

Mpende au mchukie, Mugalu ni straika mwenye msaada mkubwa san kwa Simba hasa kwenye mechi za kimataifa!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom