Mpendazoe ni Mrithi wa Mrema? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mpendazoe ni Mrithi wa Mrema?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Elli, Jul 18, 2010.

 1. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #1
  Jul 18, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,816
  Likes Received: 10,106
  Trophy Points: 280
  Ni jumapili nimetoka ibadani, nipo hapa nyumbani, limenijia wazo hili ambalo linanisumbua kichwa changu, Hivi kweli Mpendazoe sio Mrithi wa Mrema? Urithi ninaozungumzia hapa ni ule wa kazim, kutokana na ukweli kwamba sasa Mrema anaelekea kurudi CCM baada ya kuvidhoofisha kabisa vyama vya upinzani. Je kuna uwezekano kuwa CCM wameamua kumtafuta mrithi wa Mrema ili kuendeleza jahazi??

  Juzi kakimbilia CCJ, leo kakimbilia CHADEMA! Kesho haijulikani ni wapi, labda ni sehemu itakayoonekana inaleta upinzani wa kweli? Nisaidieni jamani, hivi kweli Mpendazoe sio Mrithi wa Mrema CCM? Kujibu swala hili linganisha kazi za Mrema na anazofanya Mpendazoe sasa...

  Jumapili njema
   
 2. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #2
  Jul 18, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,047
  Likes Received: 3,954
  Trophy Points: 280
  Kwani Mpendazoe ametokea usalama wa Taifa?
   
 3. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #3
  Jul 18, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,816
  Likes Received: 10,106
  Trophy Points: 280
  Mhh, kisiasa hasa!!!
   
 4. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #4
  Jul 18, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Tumpe muda kwanza ndo tufanye hukumu. Ni mapema mno kusema ni mrithi wa mzee mrema. Kama ni mrithi atajipambanua tu.
   
 5. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #5
  Jul 18, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  I dont think so,
  Kwanza stail aliyotoka nayo Mpendazoe si sawa naya Mrema iliyokuwa ya majigambo,
  Pili Mpendazoe hajulikani kama alivyokuwa Mrema enzi hizo kwa hiyo hata kama ametumwa hataweza kuleta impact kubwa kwenye maamuzi yake.
  Tatu Mrema alitoa masharti ya kuachiwa Uenyekiti kabla ya kuingia NCCR kitu ambacho sidhani kama kiko kwenye mawazo ya Mpendazoe.
  Nne vyama vilisha umwa na nyoka vitakuwa vimejifunza mengi kutoka kwa Mrema kwa hiyo sidhani kama watakuwa wajinga kiasi hicho kwa mara ya pili.
  Tano kuna vyama na vyama vya kuingilika kirahisi vingine huwa vinasimamia misingi yake kama hutaki vinakuonyesha mlango wa kutokea.
   
 6. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #6
  Jul 18, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0


  Unalazimisha premature conclusion kwani bila shaka una lengo lako. Lakini ukweli ni kwamba si wote wanaohama vyama huishia kama Mrema – hutegemea resolve ya huyo mhamaji. Kwa maana nyingine si kila mtu anayo weak resolve kama ile ya Mrema.

  Bila shaka unaelewa fika jinsi serikali ya CCM ilivyokuwa "inamshughulikia" Mrema wakati akiwa tishio kweli kwa chama tawala. Kila akitaka kufunga goli, wao huhamisha nguzo. Walimlainisha hadi akalainika na sasa wanamchangia hata hela za fomu.

  Huamini bado kama CCM huogopa wapinzani wa kweli? Wanakufanyia kila hila kwanza kukutest, na ukiwa weak, basi finito! Kwa nini CCM wameshindwa kufanya hivyo kwa Dr Slaa, Ndesamburo na Maalim Seif? It all depends on the individual concerned.

  Too early to say that on Mpendazoe – just too early, my dear! Ni mara ya kwanza serikali ya CCM kumhamishia nguzo Fred (kukinyima chama chake usajili – kwa sababu yoyote ile). Kwa sasa hivi mimi nasema Fred ni very courageous politician, kuliko wengi wale waliokuwa wanapiga tarumbeta kuhusu ufisadi, lakini when it came for the real deciscion to take, they just chickened out.

  Wameogopa ile mbaya. Kama unaam ini unachokisimamia, ni unafiki tu kuonyesha woga wa utoto.

  Big Up -- Mpendazoe!!!!
   
 7. dengeru

  dengeru Member

  #7
  Jul 18, 2010
  Joined: Oct 1, 2009
  Messages: 52
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ukimwangalia mpendazoe huyu anaehama vyama sasa ndo unaweza kuwa na huo wasiwasi kuwa labda yupo kama mrema,ila kama unamfahamu mpendazoe na misimamo yake toka akiwa bungeni ndo unaweza kujudge vizuri,kama uliwahi kufuatiliahoja zake na michango yake bungeni wala huweiz kuna na hofu naye kabisa,huyu ni mwanamapinduzi wa kweli na amekuwa akisimamia kile alichokuwa akikiamini,alikuwa mwiba kwa CCM.na pia sababu alizozitoa kuhusu kuhama kwake zipo wazi,CCJ hakijapata usajiri wa kudumu hivyo kumfanya asiweze kugombea ubunge mwaka huu,itakuwa ni hasara kwa wanamapinduzi kukosa hoja na busara zake huyu mzee kwa kipindi cha miaka kumi...kumbua huyu ndo amesababisha mgodi wa kiwira uliochukuliwa na mkapa kurudi serikalini...ni afadahali kuwa na mpendazoe 1 kuliko kuwa na akina kingunge 200..mungu ibariki tanzania,mungu mmbariki mpendazoe..
   
 8. babu M

  babu M JF-Expert Member

  #8
  Jul 19, 2010
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 3,992
  Likes Received: 990
  Trophy Points: 280
  Wabunge wa ccm ni kama 86pc ya wabunge wote,Kwa upeo wangu sioni ccm kujaribu kumpandikisha Mpendazoe kwenye 14pc.CCM wanaogopana wao kwa wao na sio upinzani
   
 9. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #9
  Jul 19, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  hajatumwa lakini anachofanya hata CCM wanakifurahia.
   
 10. minda

  minda JF-Expert Member

  #10
  Jul 19, 2010
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 1,070
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  huyu jamaa wala hajatumwa ila kajitoa mhanga kwa ajili ya taifa hili. kumbuka aliachia ubunge na mafao kibao akijitetea kwamba mafao kwake si muhimu kuliko mustakabali wa watanzania.
  mrema alifukuzwa kazi kwa kuvunja dhana ya uwajibikaji wa pamoja ndani ya baraza la mawaziri ambalo yeye alikuwa mjumbe; mpendazoe aliondoka mwenyewe ccm kwa kuchoshwa na kila alichokiita chama hicho kutetea ufisadi na wanaofanya ufisadi.
   
 11. S

  Shelute Mamu Member

  #11
  Jul 19, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Subiri matokeo. Lisemwalo lipo kama halipo laaaaaaaaaaaaaaja!
   
 12. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #12
  Jul 19, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Tutawaona hakuna wakijijini wala wa mjini hapo!huyo ndiye mpenda-ozo,mtamtambua mwanawane!
   
 13. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #13
  Jul 19, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,689
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Acha upuuzi ameacha mafao gani?
   
 14. b

  balenyaguje Member

  #14
  Jul 19, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  naona yuko kwenye kazi maalumu kwa manufaa ya nchi.
  Tumpe muda tuone.
   
 15. kaburunye

  kaburunye JF-Expert Member

  #15
  Jul 19, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 675
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Acha matusi. Toa hoja usitoe matusi. Kuwa mstaarabu hata unapokuwa hukubaliani na mawazo ya wengine.
   
 16. OFFORO

  OFFORO Member

  #16
  Jul 19, 2010
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Bongo hakuna siasa! Ni kelele tu za watu wanaotaka kula ruzuku za serikali!
  Kwa mfano angalia jinsi tlp walivyokuwa wanaendesha kikao chao cha mwisho ambacho kilimpata mgombea urais!
  Porojo na majungu mengi

  mungu ibariki bongo, wahuni wasiongoze nchi hii
   
 17. K

  Kashishi JF-Expert Member

  #17
  Jul 20, 2010
  Joined: Apr 11, 2010
  Messages: 1,101
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Udhanivyo ndivyo wala SIVYO ndugu yangu. Imagine wewe leo ungekuwa mwanachama CCJ ungefanyaje na Uchaguzi huu umeshakaribia na serikali ndio imeshaamua kwa kutumia ubabe na mitulinga yake kuvunga milango ya demokrasia kama katika mazinga yanayoikabili CCJ kwa sasa?

  Na nakuhakikishia si Mpendazoe pekee atayeenda Chadema, wengi wako njiani kwenda Chadema mwaka huu...Stay tuned.
   
 18. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #18
  Jul 20, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,816
  Likes Received: 10,106
  Trophy Points: 280
  Kashishi nimeisoma kwa makini, kweli nimeamua kukubaliana na mawazo yako
   
Loading...