Mpendazoe azidi kuwaandama mafisadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mpendazoe azidi kuwaandama mafisadi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kilbark, Nov 15, 2010.

 1. Kilbark

  Kilbark JF-Expert Member

  #1
  Nov 15, 2010
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 558
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Geofrey Nyangóro
  MWANACHAMA wa Chadema aliyekuwa akiwania Ubunge katika Jimbo la Segerea, jijini Dar es Salaam, Fred Mpendazoe, amelitabiria taifa kuingia katika utumwa kama kikundi cha watu wa chache kitaendelea kuwapangia watu viongozi wa kuwaongoza.

  Mpendazoe ambaye tayari ameshafungua kesi mahakamani kupinga ushindi wa Mbunge wa jimbo hilo, katika uchaguzi wa mwaka huu Dk Makongoro Mahanga wa CCM, aliyasema hayo jana katika mkutano wa wa kuwashukuru wakazi wa jimbo hilo kwa kukiunga mkono chama chake katika uchaguzi.

  "Kama watu wachache wanakaa na kuwaamulia watu nani awe diwani wao, mbunge, rais na hata Spika bila ridhaa ya wananchi, taifa linaelekea kubaya na huo ni utumwa,"alisema Mpendazoe.

  Katika mkutano huo, Mpendazoe aliwataka Watanzania kuunganisha nguvu zao katika kudai haki kwa kuwa ndio msingi wa maendeleo.
  Alisema bila haki, hakuna maendeleo yanayoweza kupatikana na kwamba vitendo vya ukiukwaji wa haki za msingi za bidanamu, unaofanywa na watu wachache unalitia aibu tauifa nzima.

  "Nidhahiri kuwa hali ilipofikia Watanzani wanataka mabadiliko na hiyo ndiyo sababu wamekuwa wakiunga mkono Chadema,naviomba vyombo vya dola, polisi, Usalama wa Taifa na wapenda maendeleo, kuunganisha nguvu zao katika kutetea haki, ili kuleta maendeleo ya kweli katika taifa,"alisema Mpendazoe.

  Alisema kamwe taifa haliwezi kuendelea kama viongozi wake, wataendelea kuwekwa na kikundi cha watu wa chache mafisadi na kusisitiza kuwa katika msingi huo, demokrasia ya kweli hapa itakoma kwa kuwa maamuzi yatafanywa kili ulinda maslahi ya watu wenye fedha.

  Akizungumza kesi iliyoko mahakamani ya kupinga matokea alisema tayari wanachama wake wameshatoa mchango wa Sh5 milioni, kugharimia uendeshaji na kuwataka wanachi kuchangia ili kuhakiksha haki inapatikana.

  MWANANCHI
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Nov 15, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,315
  Likes Received: 19,477
  Trophy Points: 280
  hapa hadi kieleweke
   
 3. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #3
  Nov 15, 2010
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Huyu ndio ishakula kwake kigeugeu...aende akakuze CCJ..lol
   
 4. dwight

  dwight JF-Expert Member

  #4
  Nov 15, 2010
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 437
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Poor Mpendazote uchu wa madaraka ulimzidi
   
Loading...