Mpendazoe azidi kuwaandama mafisadi

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,427
154,271
MWANACHAMA wa Chadema aliyekuwa akiwania Ubunge katika Jimbo la Segerea, jijini Dar es Salaam, Fred Mpendazoe, amelitabiria taifa kuingia katika utumwa kama kikundi cha watu wa chache kitaendelea kuwapangia watu viongozi wa kuwaongoza.

Mpendazoe ambaye tayari ameshafungua kesi mahakamani kupinga ushindi wa Mbunge wa jimbo hilo, katika uchaguzi wa mwaka huu Dk Makongoro Mahanga wa CCM, aliyasema hayo jana katika mkutano wa wa kuwashukuru wakazi wa jimbo hilo kwa kukiunga mkono chama chake katika uchaguzi.


"Kama watu wachache wanakaa na kuwaamulia watu nani awe diwani wao, mbunge, rais na hata Spika bila ridhaa ya wananchi, taifa linaelekea kubaya na huo ni utumwa,"alisema Mpendazoe.


Katika mkutano huo, Mpendazoe aliwataka Watanzania kuunganisha nguvu zao katika kudai haki kwa kuwa ndio msingi wa maendeleo.


Alisema bila haki, hakuna maendeleo yanayoweza kupatikana na kwamba vitendo vya ukiukwaji wa haki za msingi za bidanamu, unaofanywa na watu wachache unalitia aibu tauifa nzima.

"Nidhahiri kuwa hali ilipofikia Watanzani wanataka mabadiliko na hiyo ndiyo sababu wamekuwa wakiunga mkono Chadema,naviomba vyombo vya dola, polisi, Usalama wa Taifa na wapenda maendeleo, kuunganisha nguvu zao katika kutetea haki, ili kuleta maendeleo ya kweli katika taifa,"alisema Mpendazoe.

Alisema kamwe taifa haliwezi kuendelea kama viongozi wake, wataendelea kuwekwa na kikundi cha watu wa chache mafisadi na kusisitiza kuwa katika msingi huo, demokrasia ya kweli hapa itakoma kwa kuwa maamuzi yatafanywa ili kulinda maslahi ya watu wenye fedha.


Akizungumza kesi iliyoko mahakamani ya kupinga matokea alisema tayari wanachama wake wameshatoa mchango wa Sh5 milioni, kugharimia uendeshaji na kuwataka wanachi kuchangia ili kuhakikisha haki inapatikana.
 
Kiukweli tunahitaji utashi kutoka ccm apatikane mtu anayeitaji Tanganyika!!ilikuikomboa Tanzania!vinginevyo tutakuwa watumwa wawachache walipo kwenye madaraka!kwani tunaona hata vyama vya upinzani kuna ufisadi hapotutegemee nini??kama sikurudishana nyuma!!??
 
Kila mtu aliye safi ajifanyie screening kama kweli ana nia ya dhati ya kulifikisha taifa letu kwenye ngazi nyingine ya kimaendeleo.

Maneno mazuri na matendo ya hovyo vitaturudisha nyuma daima
 
Kila mtu aliye safi ajifanyie screening kama kweli ana nia ya dhati ya kulifikisha taifa letu kwenye ngazi nyingine ya kimaendeleo.

Maneno mazuri na matendo ya hovyo vitaturudisha nyuma daima


maana yake nini? eleweka.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom