Mpendazoe atupwa nje kura za Wagombea Ubunge CHADEMA

RRONDO

JF-Expert Member
Jan 3, 2010
51,719
107,834

.

1.Wajumbe
2.Rachel Mashishanga
3.Freddy Mpendazoe.

Aliyekuwa Mbunge wa Kishapu CCM na baadae kukihama chama hicho na kuhamia Chama mfu CCJ na kuhama tena CCJ kwenda CHADEMA, Freddy Mpendazoe leo hii amebwagwa vibaya katika kura za maoni kuomba ridhaa ya wajumbe ya kugombea ubunge jimbo la Segerea.Katika uchaguzi uliofanyika ukumbi wa baa ya Seper Karatu Ukonga na kukamilika jioni hii Mpendazoe ameangushwa vibaya na Mwanamama Rachel Mashishanga kwa zaidi ya kura 20, Rachel Mashishanga amepata kura 48, ikiwa Fred Mpendazoe akiambulia kura 28 tu. Kwa matokeo hayo Rachel Mashishanga ndiye Mgombea ubunge jimbo la Segerea jijini Dar es Salaam kwa Tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)

kwa hisani ya:MJENGWA BLOG.
 
i was expecting that ...............nothing suprising there.
 
:behindsofa:kwani ilikuwaje hakurudi kwenye jimbo lake? Au chama hakipo huko?
 
huyu mama RACHEL MASHISHANGA ni nani?naomba wanaomfahamu wanipe wasifu wake kidogo...........
 
si aende kulitetea jimbo la kishapu kule kama alishinda kwa njia safi na kawatumikia vizuri mwanzo? sidhani kama wananchi kule watamtosa kwa vile anagombea kwa ticket ya chadema.

kama alishinda kishapu kwa njia chafu basi labda ndio maana kakimbia kwani ushindi wa njia chafu unatumiwa na chama kimoja tu.
 
si aende kulitetea jimbo la kishapu kule kama alishinda kwa njia safi na kawatumikia vizuri mwanzo? sidhani kama wananchi kule watamtosa kwa vile anagombea kwa ticket ya chadema.
tatizo leo ndo ilikuwa siku ya nominations within the party yaani Chadema na CCM! sasa kama alibugi step namna hii sidhani kama anaweza rudi Kishapu! cha kufanya asubiri tu nathani ana umuhimu mkubwa wa kurudi Bungeni hata kama through party nomination! Pole sana mkuu tupo pamoja
 
Daah, wengi watamkumbuka Mtikila na sheria ya mgombea binafsi!
 
Daah, wengi watamkumbuka Mtikila na sheria ya mgombea binafsi!
umenena, ila unafikiri ingekuwa rahisi kushinda kama yeye? Watanzania haswa wa jimbo wangeweka imani kweli kwenye hilo?
 
mwanzo mbaya sana kwa wapambanaji.ni mwanzo mbaya pia kwa chadema pia natuombe mungu hali hii isiendelee inakera sana
 
Mpendazoe kajimaliza mwenyewe! Alikosea mahesabu sana pale alipoamua kuihama CCM kwa mbwembwe na kwenda CCJ huku akijua kwamba chama anachokwenda hakina hata usajili. Right angeota aende CHADEMA moja kwa moja si ajabu angekuwa amepata hata akili nzuri juu ya jimbo gani agombee. Lakini bado hajachelewa, sasa hivi afanye kazi ya kumsupport Slaa, naamini CHADEMA watampa nafasi za kuteuliwa kama zipo.
 
Pole zake hata hivyo alitanga tanga mno mzee mzima. Yawezekana kalaaniwa na wapiga kura wake.
 
1.Wajumbe
2.Rachel Mashishanga
3.Freddy Mpendazoe.

IMG_0795.jpg
Aliyekuwa Mbunge wa Kishapu CCM na baadae kukihama chama hicho na kuhamia Chama mfu CCJ na kuhama tena CCJ kwenda CHADEMA, Freddy Mpendazoe leo hii amebwagwa vibaya katika kura za maoni kuomba ridhaa ya wajumbe ya kugombea ubunge jimbo la Segerea.Katika uchaguzi uliofanyika ukumbi wa baa ya Seper Karatu Ukonga na kukamilika jioni hii Mpendazoe ameangushwa vibaya na Mwanamama Rachel Mashishanga kwa zaidi ya kura 20, Rachel Mashishanga amepata kura 48, ikiwa Fred Mpendazoe akiambulia kura 28 tu. Kwa matokeo hayo Rachel Mashishanga ndiye Mgombea ubunge jimbo la Segerea jijini Dar es Salaam kwa Tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)

Aliyekuwa Mbunge wa Kishapu CCM na baadae kukihama chama hicho na kuhamia Chama mfu CCJ na kuhama tena CCJ kwenda CHADEMA, Freddy Mpendazoe leo hii amebwagwa vibaya katika kura za maoni kuomba ridhaa ya wajumbe ya kugombea ubunge jimbo la Segerea.Katika uchaguzi uliofanyika ukumbi wa baa ya Seper Karatu Ukonga na kukamilika jioni hii Mpendazoe ameangushwa vibaya na Mwanamama Rachel Mashishanga kwa zaidi ya kura 20, Rachel Mashishanga amepata kura 48, ikiwa Fred Mpendazoe akiambulia kura 28 tu. Kwa matokeo hayo Rachel Mashishanga ndiye Mgombea ubunge jimbo la Segerea jijini Dar es Salaam kwa Tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)

Source: Mjengwa blog
 
mwanzo mbaya sana kwa wapambanaji.ni mwanzo mbaya pia kwa chadema pia natuombe mungu hali hii isiendelee inakera sana
Wewe una akili timamu kweli yaani kushindwa kwa Mpendazoe na mwanachama wa Chadema ni mwanzo mbaya wa chadema kivipi au zako zimetune upande mmoja, au hujui maana ya kura za maoni umevamia jukwaa si lako hili.
 
Nilishangaa sana kwa Mpendazoe kukimbia jimbo alilokuwa akiwakilisha, ndipo nikagundua kuwa huenda alikuwa na walakini fulani katika ushindi uliompeleka bungeni, na uwakilishi wake katika kipindi hicho alichokuwa bungeni. Inawezekana kabisa kuwa ushindi uliompeleka bungeni ulikuwa wa kuiba kwa kutumia vyombo vya CCM na hivyo asingeweza kuupata ushindi huo tena baada ya kukosana na vyombo hivyo vya CCM. Kuamua kugombea Dar ambapo CHADEMA ilikuwa na watu wake wa siku nyingi ilikuwa ni kutoona mambo kwa kina, at least angetafuta jimbo ambalo CHADEMA haikuwa na wawakilishi wa kutosha; huyu dada Mashishanga ni wa siku nyingi sana ndani ya CHADEMA, na amekuwa mwenyeji wa huko Segerea kwa siku nyingi ambako alikuwa kiongozi wa tawi mojawapo la CHADEMA.

Hata hivyo sijui strengths za huyu Rachel Mashishanga kwani amefanya mtihani wa form four mwaka jana tu na kupata division four:

RACHEL STEPHEN MASHISHANGA: (pts 27) (Division: IV ) - Subject Scores: CIV-D, HIST-D, GEO-D, KISW-D, ENGL-C, BIO-F, B/MATH-F, COMM-F, B/KEEPING-C,
 
Rachal Mashishanga ni mtoto wa Mzee Steven Mashishanga. Nadhani CHADEMA wametupa kete yao vibaya sana; kwani Rachel hajulikani, hayuko vocal kisiasa kiasi cha kumshinda Mpendazoe. hayuko well kiuchumi kumshinda Mpendazoe. Hana umaarufu kumshinda Mpendazoe. Nasikitika sana, kwani Rachel anagombea Ubunge siyo kushinda Jimbo bali kupata fursa ya kupeta viti maalum.

Nadhani Kamati Kuu ya CHADEMA imwombe Rache ampishe Mpendazoe.
Tusubirini.
 
Nilishawahi kusema kuwa Chadema iko makini ina watu makini kuanzia majimboni hadi taifa, hawachagui mtu kwa vile tu katoka chama tawala. Kuna watu walianza kusema Mpendazoe na Marando wametumwa kuisambaratisha Chadema kitu ambacho itakuwa ngumu sana kwa hali ninavyoijua Chadema kimuundo.

Najua kuna wanaCCM wengi watajiunga Chadema baada ya kutemwa na chama chao, kama kweli wana moyo wa dhati wa kuwatumikia wananchi wanakaribishwa, kwa vile utumishi kwa umma si lazima uwe ndani ya chama tawala, ila wasitegemee mteremko wa haraka katika uongozi kaa kwa muda onyesha umahili wako kama alivyofanya Lwakatare then umahili na uwezo wako ndio utakaokupatia uongozi.

Ushauri wangu kwa Mpendazoe na wengine watakaoingia Chadema ambacho ni chama kikuu cha upinzani kwa sasa, wasitegemee kupata vyeo kwa muda mfupi kama alivyopewa Mrema waje wakae wasome katiba na sera zinasemaje baadaye wakijenge chama. Lakini vilevile kuna exceptional figures kama alivyo Marando unaweza ukaombwa usaidie mapambano Day One unapoingia kwenye chama hata kugombea ubunge kutokana na rekodi yako.

GO Slaa GO.
 
Back
Top Bottom