Mpendazoe akamatwa...

Sokomoko

JF-Expert Member
Mar 29, 2008
1,915
127
Sadick Mtulya
ALIYEKUWA mgombea ubunge wa Jimbo la Segerea kwa tiketi ya Chadema, Fred Mpendazoe janaalipatwa na msukosuko wakati alipokamatwa na askari wa Jeshi la Polisi ambao walidai kuwa alikuwa anamiliki na kutumia gari la wizi, tukio ambalo amelielezea kuwa lilipangwa kwa lengo la kumchafua.

Mpendazoe, ambaye alishindwa kwenye uchaguzi huo wa ubunge kwa njia ambayo ameielezea kuwa ilijaa ukiukwaji wa sheria, alihojiwa na polisi kwenye kituo cha Buguruni kwa takriban saa mbili kabla ya kuachiwa bila ya masharti.Mpendazoe, mmoja wa wabunge waliokuwa mstari wa mbele kwenye vita dhidi ya ufisadi, alikamatwa jana majira ya saa 3:30 asubuhi eneo la Uwanja Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere akiwa na diwani wa Chadema wa Kata ya Segerea, Azuri Mwamboji pamoja na Buhari Mgonyezi ambaye aligombea udiwani wa Kata ya Kinyerezi.
Hata hivyo, Mpendazoe, ambaye alihama CCM mapema mwaka huu wakati akiwa mbunge wa Jimbo la Kishapu na kujiunga katika Chama cha Jamii (CCJ) na baadaye Chadema, aliachiwa majira ya saa 5:44 asubuhi na maafisa upelelezi wakamueleza kuwa wataendelea na uchunguzi.

"Kwa kuwa namba zako za simu umetuachia, wewe nenda. Sisi tutatimiza wajibu wetu wa kuendelea na uchunguzi. Hatua tutakayofikia tutakufahamisha,'' alisema afisa upelelezi mmoja.
Mpendazoe amefungua kesi Mahakama Kuu kupinga matokeo ya ushindi wa Dk Makongoro Mahanga kwenye Jimbo la Segerea, baada ya zoezi la kuhesabu kura kuingiwa na dosari kubwa zilizocheleweshwa kutangazwa kwa matokeo.
Hata hivyo, Dk Makongoro ameshateuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa Naibu Waziri wa Kazi na Ajira.
Mpendazoe anatuhumiwa kumiliki na kutumia gari la wizi aina ya Toyota Corona, lenye rangi nyeupe ambalo inadaiwa liliripotiwa kuibwa tangu Juni mosi, 2010.
Lakini mbunge huyo wa zamani wa Kishapu aliiambia Mwananchi jana kuwa tuhuma hizo zimelenga kumchafua na kwamba ni hujuma.

"Askari walinikamata kwa nguvu kubwa, hadi kufikia hatua ya kutishia kutumia silaha endapo ningeendelea na msimamo wangu wa kutaka kujieleza... sisi ni raia na katika mazingira haya inabidi tusaidiwe,'' alisema Mpendazoe ambaye aliruhusiwa kuondoka na gari hilo.
Alifafanua kuwa tukio hilo lilipangwa kwa makusudi na kusisitiza kuwa gari hilo ni lake na amekuwa akilimiliki tangu mwaka 2007.

"Hadi sasa polisi hawajaniambia ni mtu gani aliyefungua mashtaka haya (ya kudai kuibiwa gari hilo). Hii ni hujuma kutoka kwa watu ambao hawanitakii mema pamoja na dola kuendelea kunikandamiza. Gari nimelitumia katika kipindi chote cha kampeni zilizopita za uchaguzi mkuu,'' alisema.
"Jana (juzi) tu, nilikuwa nalo kituo cha polisi cha Sitakishari, Ukonga nilipokuwa nimekwenda kuomba kibali cha kufanya mkutano wa harambee ili kuwaomba wananchi kunichangia fedha kwa ajili ya kuendeshea kesi niliyofungua kupinga matokeo yaliyompa ushindi Dk Makongoro.''
Hata hivyo, Mpendazoe alisema kuwa polisi walimnyima kibali hicho na kulalama kuwa eneo alilokuwa amekusudia kufanya mkutano ndilo aliloruhisiwa Dk Mahanga wiki iliyopita kufanya mkutano wa kuwashukuru wakazi wa Segerea kwa kumchagua.

Mpendazoe pia alidai kuwa wiki iliyopita alitumia gari hilo kwenda kituo kikuu cha kati cha polisi kuomba kibali cha kufanya mkutano wa hadhara.
"Ajabu nyingine gari hili hili, wiki iliyopita nilikuwa nalo... mbona hawakunikamata,'' alihoji Mpendazoe.
Alikwenda mbali na kusema: " Kulingana na mazingira haya, hisia zangu ni kwamba hizi ni hujuma na demokrasia inaaza kukandamizwa.''

Kamanda wa Polisi Ilala, Faustine Shilogile hakutaka kuzunghumzia suala hilo kwa maelezo kuwa hakuwa ofisini.
"Nitafute baadaye; kwa sasa sina taarifa kamili na muda huu ( saa 6:30 mchana) nipo njiani natoka uwanja wa ndege.... naenda hapo kituoni,'' alisema.
Alipopigiwa simu baadaye, hakupokea.
 

sulphadoxine

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
2,257
641
CCM Wameanza kazi yao ya kipuuzi ili kumvunja nguvu mpiganaji mpendazoe,hiiii nchi ina watu wa ajabu sana,wakiwemo polisi,ambao awafuati maadili ya kazi yao.
 

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
48,033
66,488
Baado hawataweza daima!! sasa anaogopa nini kupokea simu?
 

sulphadoxine

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
2,257
641
Nadhani atakuwa amejua kuwa ni zengwe ndio maana ataki kupokea simu,ila waache mambo ya ajabu hawa watu ccm na askari wao ambao awafuati sheria na taratibu za jeshi la polisi,Tatizo polisi wa bongo awaoni kazi kumpachikia mtu kesi.
 

Nyunyu

JF-Expert Member
Mar 9, 2009
4,354
1,005
Kama wa polisi Faustin ni mtu ninayemjua, ni msomi na muelewa; ni hatari kusikia kuwa na yeye anatumiwa na wakubwa kutimiza haja zao!!!
 

tumpale

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
200
35
kuna haja ya kuangalia sheria upya maana hawa wanaobambikia kesi raia wema wao wanafanywa nini baada yakubainika kuwa wamewabambikia watu kwa makusudi,tuwe na utaratibu wa kuwashitaki kwa kubambikia watu kesi, kwa stahili hii mchezo huu utakwisha, wanabambikia watu kesi afu wanajisifu and nothing is done to them, what a hell is that.
 

mpingomkavu

Member
Nov 26, 2010
94
0
:party:Mi binafsi siwalaamu polisi wetu nalaumu mfumo, kwani mwanasiasa akisema kama fulani basi hawa jamaa ni kama mbwa kukimbia na kukamata tu,ukienda kinyume wewe utapelekwa makao makuu kusoma magazeti, angalieni vizuri uhamisho wa makamanda wa polisi wa hivi akaribuni mtapata jibu
:whoo::whoo::whoo:
 

Somoche

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
5,561
4,927
shame on you polisi njaa. majambazi na vibaka yanawatoa jasho kila siku na hamyawezi. eti gari la wizi baadae mnaliachia xibit mahakamani kiktakua nini?!!! wajinga sana polisi njaa nyie mnatumiwa na makongoro.
 

Njowepo

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
9,618
2,123
Sasa mtu ana gari toka 2007 alafu manakuja sema gari imeibiwa mwaka 2010 sasa kabla ya uchaguzi why wasingemkamata?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom