Mpe alichokwambia umpe.

St. Paka Mweusi

JF-Expert Member
Sep 3, 2010
7,369
2,000
Kuna shehe mmoja alioa mtoto mwanamwali mzuri wa kuvutia.Basi kutokana na wivu aliokuwa nao kwa mkewe alikuwa hatoki ndani kila siku anamchunga mkewe.Vijana wa mtaani nao kila aliyebahatika kumuona mke wa shehe huyo aliapa kuwa lazima ajivinjari na mke wa shehe huyo,lakini hilo halikuwezekana kutokana na jamaa alivyokuwa akimchunga mkewe.Shehe alipoona jinsi vijana wanavyohangaika basi akaanza kutamba mtaani kwamba hakuna mwenye mke mzuri kama wa kwangu na hakuna anayeweza kumrubuni.Siku moja wakati shehe anakwenda kuswali akiwa keshafunga udhu na ametoka ila hayuko mbali sana na nyumbani kiatu chake kikamkatikia,kurudi nyumbani akashindwa,akaamua kumtuma kijana aliyekuwa jirani na maeneo yale akamwambia kijana naomba ukanichukulie viatu nyumbani kwangu utanikuta hapo kwenye kahawa.Kijana akatoka mbio kuwahi nyumbani kwa shehe,kufika akamkuta mke wake na kumwambia mama mmeo kanituma nije kwako tuvunje amri ya sita,yule mwanamke akaruka kwa ukali na kuanza kuporomosha matusi kwa yule jamaa.Yule jamaa kuona hivyo akatoka nje ya nyumba na kumwambia shehe kwa sauti kubwa maana hakuwa mbali sana na nyumbani,akasema mzee hataki kunipa!Shehe kusikia hivyo hasira zikampanda naye akajibu kwa sauti kubwa we mwanamke mpe huyo kijana anachokwambia umpe.Basi jamaa akajikuta ameua Tembo kwa ubua.
 

bucho

JF-Expert Member
Jul 13, 2010
4,925
2,000
duu nshasikiaga hii story long tym .umenikumbusha mbali sana .
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom