Mpasuko Wainyemelea KKKT | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mpasuko Wainyemelea KKKT

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by X-PASTER, Nov 27, 2010.

 1. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #1
  Nov 27, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  *Askofu Malasusa atakiwa kujiuzulu
  *Waumini wengine walikimbia kanisa

  Wakizungumza na gazeti hili, baadhi ya waumini wa makanisa mbalimbali yaliyo chini ya kanisa hilo wamesema hivi sasa kanisa hilo limeingiwa na shetani aliyesababisha mgawanyiko wa makundi mawili, jambo ambalo halimpendezi Mungu na ni hatari katika maadili ya kiroho.

  “Kiongozi mzuri hapaswi kulalamikiwa kama maandiko matakatifu yanayosema. 1 Timotheo 3:2-7 inamuelekeza askofu mkuu anavyotakiwa kuwa," amedai muumini mmoja ambaye hakutaka kutaja jina lake.

  Muumini huyo amesema hivi sasa waumini katika sharika mbalimbali wamekuwa wakimlalamikia Malasusa kutokana na utendaji wake mbaya hali ambayo imewafanya wengi wao kukimbilia kwenye madhehebu mengine.

  “Tuna idadi kamili ya waumini waliohamia madhehebu mbalimbali ambao wote wanadai kuwa hawaridhiki na utendaji wa Malasusa kutokana na mapungufu yake,” amedai muumini huyo.

  Ameongeza kuwa kitendo cha Askofu Malasusa kumfukuza mchungaji Enock Mlyuka na Mtheologia wa Kibiti kukataa kubarikiwa na askofu huyo kuwa mchungaji ni dhahiri kuwa anajua mengi juu ya Malasusa ambayo yanamkwaza na kumfanya aone kuwa hapaswi kumuongoza kwenye njia ipasayo.

  Ameendelea kudai kuwa katika Usharika wa Azania Front kumekuwa na malalamiko ya watumishi juu ya ucheleweshaji wa mishahara, huku kukiwa na matumizi mabaya ya fedha na watumishi wengine wakijilipa mishahara mikubwa kila mwezi.

  “Kitendo cha matumizi mabaya ya fedha kinaweza kuchangia kanisa kuingia kwenye machafuko wakati wahitaji wengi kama yatima wakiendelea kuteseka kwa kukosa misaada inayotolewa na wafadhili wetu,” amesema muumini huyo.

  Kutokana na malalamiko hayo, waumini hao wamemuomba Askofu Malasusa kukaa kando ili uchunguzi ufanyike na kupata kiini cha matatizo ndani ya kanisa hilo.

  Katika waraka wao ambao gazeti hili limeupata, wamemuomba Naibu Katibu Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani (DMP), Ernest Kadiva, kulionea huruma kanisa hilo huku wakizingatia kuwa mishahara wanayojilipa ni sadaka kwa wajane, wazee, watoto na wengi wasio na uwezo.

  Akizungumza na gazeti hili kuhusu malalamiko hayo, Msaidizi wa Askofu, Mchungaji George Fupe, amesema ni kweli kuna malalamiko kutoka kwa waumini na tayari yameanza kufanyiwa kazi.

  Askofu huyo amesema si jambo la busara kwa waumini hao kukimbilia kwenye vyombo vya habari kutoa malalamiko yao na badala yake amewaomba kufika Makao Makuu ya kanisa hilo.

  Hata hivyo, mchungaji huyo ameahidi kutoa taarifa kamili kuhusu malalamiko hayo.

  Hata hivyo, wakati gazeti hili linakwenda mitamboni kulikuwa na taarifa ambazo si rasmi kuwa wachungaji wa kanisa hilo wamepewa waraka wa taarifa mbalimbali zinazolikumba kanisa hilo na kutakiwa kuwaelimisha waumini kuhusu askofu huyo.


  DarLeo
   
 2. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #2
  Nov 27, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,784
  Likes Received: 1,970
  Trophy Points: 280
  haya masakata ya ubadhirifu katika makanisa ni ya kuangaliwa kwa umakini vinginevyo yatakatisha tamaa waumini.
   
 3. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #3
  Nov 27, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,437
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Fedha ndio inasababisha yote haya!
   
 4. M

  Mountainmover Member

  #4
  Nov 27, 2010
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 46
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Malasusa na Kadiva jueni ya kwamba KKKT si kampuni bali ni kanisa la Mungu. Pamoja na mambo mengine yalichochea kuchepuka kwa kanisa la kilutheri kutoka kanisa la kirumi ni ubadhirifu wa fedha uliofanywa na mapapa wa enzi hizo. Iweje leo msaliti misingi ya muasisi wenu Martin Luther? Tunaomba mjirekebishe.
   
 5. K

  Kimambo Member

  #5
  Nov 27, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 76
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Lisemwalo lipo this needs immediate action, wnahitajika kukaa makini kuona kama kuna jambo la kutengeza, kila siku malalamiko kibao and by/the way this is a dioces with everthing but not better for any thing, diocs haina benki wamashindwa hata na kilimanjaro hakuna shule xa maana, hakuna shospitali za maan what ismalasusa is failure
   
 6. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #6
  Nov 27, 2010
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Malasusa angalia fedha ya CCM inavyokuharibia kanisa lako, watu wamepewa kidogo kitu ili tu wakuharibie kwani ulipiga vita sana ya mafisadi yasichaguliwe katika uchaguzi sasa wanakuundia zengwe chinichini wakiwa na nia ya kukumaliza...kaa chonjo kwani wana mbinu nyingi na zote ni chafu
   
 7. Kishongo

  Kishongo JF-Expert Member

  #7
  Nov 27, 2010
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Malasusa anavuna alichopanda kutokana na kumpigia debe Dr Slaa.

  Alijionesha waziwazi kumshabikia Slaa na hata kumwita 'Jiwe Kuuu la Pembeni"

  Ukivuna dhambi utavuna dhambi, huwezi kukataa chaguo la mungu JK.

  Sasa inakula kwake.
   
 8. Simba Mangu

  Simba Mangu JF-Expert Member

  #8
  Nov 27, 2010
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 351
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Kishogo ala samahani kishongo jk hawazi kamwe kuwa chaguo la mungu kwani chaguo la mungu huwa halijikwezi hivyo tafakari na utubie kumshirikisha mungu ktk upuuzi
   
 9. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #9
  Apr 17, 2016
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,515
  Likes Received: 1,685
  Trophy Points: 280
  Mlyuka amefukuzwa KKKT??? Huyu Mchungaji anasifika na anatambulika kwa misimamo mikali isiyoyumba. Alinibariki (kipaimara) usharika wa Bagamoyo. Ni brain chache sana ambazo KKKT DMP waliwahi kuwa Nazo. Nimeambiwa sasa hivi ni Dokta(PhD). Daah makanisa yetu yana mambo! Ndo maana Mimi sitoi sadaka kanisani
   
 10. R

  Recae JF-Expert Member

  #10
  Apr 17, 2016
  Joined: Jul 9, 2015
  Messages: 238
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 60
  Post ya zaman tangu 2010
   
 11. P

  Pohamba JF-Expert Member

  #11
  Apr 17, 2016
  Joined: Jun 2, 2015
  Messages: 14,393
  Likes Received: 21,333
  Trophy Points: 280
  Mwacheni Malasusa acheni chokochoko!
   
 12. k

  kabombe JF-Expert Member

  #12
  Apr 17, 2016
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 15,566
  Likes Received: 8,509
  Trophy Points: 280
  DMP kuna matatizo ya ukabila hasa naeneo ya uzaramo
  Kuna wachaga wanaona kama wao ndio wenye hati miliki ya kanisa kwa ukaskazini wao.
  Tatizo hili liliwahi kutokea miaka ya nyuma askofu na msaidizi wake kama sikosei mchungaji kombo wakawekwa pembeni watu wa mungu,leo yamerudi tena
   
 13. All TRUTH

  All TRUTH JF-Expert Member

  #13
  Apr 17, 2016
  Joined: Nov 20, 2011
  Messages: 3,275
  Likes Received: 983
  Trophy Points: 280
  Dhambi ya ubaguzi huwa haiachani na mbaguzi
   
 14. All TRUTH

  All TRUTH JF-Expert Member

  #14
  Apr 17, 2016
  Joined: Nov 20, 2011
  Messages: 3,275
  Likes Received: 983
  Trophy Points: 280
  Wewe wivu ndo unakumaliza kwani Dr slaa ni kiongozi shujaa Sana
   
 15. C

  Chief wa kibena JF-Expert Member

  #15
  Apr 17, 2016
  Joined: Mar 13, 2016
  Messages: 690
  Likes Received: 390
  Trophy Points: 80
  sasa mgogoro umehamia dayosis ya kusini, dayosis hii cjui inaelekea wapi? wajuv wa pande hizo tuambien tatizo nini?? me niko mbal na home?
   
Loading...