Idugunde
JF-Expert Member
- May 21, 2020
- 6,273
- 6,637
Mpasuko mkubwa umeukumba uongozi wa Chadema Mbeya mjini na hii ni dalili kuwa hawako kwenye good terms. Sijui lini watafika mbali
===========
Mchungaji Msigwa: Tumeuvunja uongozi wa jimbo la Mbeya mjini na tunawapa mkoa siku tatu kwa mujibu wa katiba kama nilivyosema kuunda timu(Task force) ambayo itasimamia shughuli za chama na tunaipa siku 60 iunganishe wanachama, iandae uchaguzi wa jimbo la Myeya mjini tupate viongozi walio halali
Wale wote tuliowatoa kwa mamlaka ya kanda(Kanda ya Nyasa) tuliyonayo, kuanzia sasa hawatakiwi kufanya shughuli za chama, wakiendelea kufanya shughuli za chama ni utovu wa nidhamu, hii ni mamlaka ambayo ipo kwenye kanda ila wanayo haki ya ukata rufaa, mlango uko wazi.
Mwenyekiti aliyeondolewa: Msigwa hana mamlaka na wenzake hawa watatu kuniondolea nafasi yangu mimi ya uenyekiti wa Mbeya mjini. Kwa mnaonisikiliza Mbeya mjini, viongozi wangu ninaowaongoza, relax. Kwasababu kamati ya kanda ina wajumbe kumi, wao wanaofanya maamuzi ya kihuni wako wanne.
Nimwambie tu Msigwa, haya ni maisha.. aache stress, sio kila kasa analiwa. Kwangu mimi ninajitambua, labda akasimamishe pembeni kwa wenyeviti ambao hawajitambui, hawasomi katiba.
Mimi nina miaka sasa 15 nachaguliwa kila msimu Mbeya kwahiyo constitution ya chama naijua, hata ukiniamsha usingizini naijua kuisoma katiba ya CHADEMA.
Mimi sio mwenyekiti wa... wanaowababaisha babaisha, mimi ni mwenyekiti wa mjini kwenye jiji, asiniletee mambo ya Iringa ambayo anawafukuza fukuza wenzake