Kuna mjadala mkali wa Muundo wa Muungano wa Tanzania ambapo kuna maoni kinzani wengine wakitaja Serikali Mbili na Wengine wakitaka Tatu.
Napenda kuwakumbusha wana Sisiemu kwamba Chama chao ni Muungano wa Vyama Viwili yaani,TANU-Tanganyika na ASP –Zanzibar na Muungano huo uliofanyika mwaka 1977 ulikuwa na lengo kuimarisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliofanyika mwaka 1964 na Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964. Najiuliza maswali haya:-
1.Yapi yalikuwa Malengo ya Muungano wa TANU na ASP mwaka 1977?
2.Ziko wapi hati au Mkataba wa Muungano wa Vyama hivi Viwili vilivyokuwa na Sera tofauti kutoka katika nchi mbili Tofauti?
Napenda kutoa Wito kwa wana Sisiemmu wanaounga Mkono muundo wa Serikali Tatu wajue kwamba, nje ya Muungano wa Serikali mbili hakuna "CCM" bali kuna "TANU – Tanganyika na ASP- Zanzibar" .
Hivyo muundo wa Serikali Tatu utakisambaratisha Chama Chama hiki chenye nguvu kubwa na kilicho muhimili wa Umoja na Mshikamano wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa zaidi ya miaongo maika 50 hivi.
"Tanganyika, sio Sera ya Chama Cha Maaaapinduzi, kwakuwa CCM ni Muungano wa TANU na ASP" Ikiwa Muungano wa Serikali Tatu utakubalika basi Chama hiki itabidi kivunjike Vipande Viwili TANU- Tanganyika na ASP –Zanzibar hivyo kukisambaratisha kabisa Chama hiki Kikongwe na kilichosimamia Uchumi ,Umoja na Mshikamano wa Watanzania.
Hatuwezi kuzungumizia Muundo wa Muungano bila kuzungumzia Muundo wa muungano wa Chama hiki imara kabisa na Chenye nguvu nyingi.
Natoa wito kwa Wahafidhina wote kwamba sasa ni Wakati wa Kudai Kipande cha TANU- Tanganyika kutoka kwenye CCM,na wale wa Zanzibar wabaki na ASP yao.
Nawasilisha maoni yangu kwenye Jukwaa.