Mpasuko Chadema waibukia mkutanoni

Luteni

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Messages
2,274
Likes
10
Points
0

Luteni

JF-Expert Member
Joined Jan 9, 2010
2,274 10 0
Imeandikwa na Na Gloria Tesha;
Tarehe: 9th January 2010

MGOGORO unaofukuta ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) umechukua sura mpya jana baada ya Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe kutofautiana kauli na mama wa Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe, Shida Salumu kuhusu fukuto hilo linalohusisha uongozi wa kitaifa wa chama hicho.

Wakati Mbowe huku akijiamini aliwaeleza vijana wasomi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kuwa hakuna mgogoro kabisa ndani ya chama, mama wa Zitto, Salumu alitoa kauli tofauti ya kuutaka uongozi wa chama kumuita mwanawe ili ahojiwe kuhusu kauli zake anazozitoa zinazoashiria kuwepo kwa mgogoro.

Kauli ya Mbowe na mama mzazi wa Zitto, walizitoa kwa nyakati tofauti katika Kongamano la Vijana lililoandaliwa na chama hicho walipokuwa wakijibu maswali ya wanafunzi walioshiriki mara baada ya kumaliza kuwasilisha mada mbalimbali kuhusu sera za chama hicho za majimbo kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao, unaotarajiwa kufanyika Oktoba 31 mwaka huu.

“Ndani ya Chadema hakuna mgogoro, zipo propaganda zinazoenezwa na watu nje ya chama ili kuonesha kwamba ndani hatuelewani, zinatengenezwa kujenga mazingira ya kuhalalisha uwongo kuwa ukweli na ukweli kuwa uwongo,” alisema Mbowe kujibu moja ya maswali ya vijana hao wa chuo kikuu.

“Haiwezekani mgogoro kuwepo usiipasue Halmashauri Kuu ya chama, kilichopo ni uhuru wa kuzungumza unaozingatia demokrasia,” Mbowe aliendelea kutoa ufafanuzi kukana kabisa mgogoro huo.

Baada ya kauli hiyo, mwanafunzi aliyejitambulisha kwa jina la Steven Owawa, ambaye aliposimama kuuliza swali alishangiliwa na wenzake, alimtaka mama mzazi wa Zitto, Salumu asimame na aeleze ana msimamo gani kuhusu kauli za mwanawe kwa kuzingatia kuwa yeye ndiye mzazi wake.

Owawa aliendelea kujenga hoja yake ili kuchokonoa kinachoendelea ndani ya chama hicho na kumtaka Salumu afafanue kuhusu kauli moja aliyoitoa Zitto kwamba, atamuunga mkono mgombea wa Ubunge wa NCCR-Mageuzi, David Kafulila, atakayegombea Kigoma Kusini badala ya mgombea wa Chadema na kuhoji kama hiyo si ishara ya mgogoro ndani ya chama.

Salumu alisema anaamini Chadema ni chama imara chenye viongozi madhubuti na kuutaka uongozi wa chama umuite Zitto, uzungumze naye ili aeleze kauli zake zinamaanisha nini.

Alisema Zitto ni mtu mzima mwenye umri zaidi ya miaka 18, na anauwezo wa kujieleza kwa hivyo hawezi kumsemea. “Niliingia Chadema mwaka 1992 na yeye (Zitto) mwaka mmoja baadaye (1993), nimemzaa ndiyo, lakini sasa yeye ni mtu mzima, umri wake ni zaidi ya miaka 18, anauwezo wa kujieleza, viongozi wamuite, wazungumze naye ajieleze,” alifafanua mama huyo huku akishangiliwa na wanafunzi hao.

Baada ya kusema hayo, Salumu aliwatoa wasiwasi vijana hao wa chuo kikuu na kuweka msimamo wake unaopingana na msimamo wa Zitto kwamba yeye Salumu atampigia kura mgombea yeyote atakayesimamishwa na Chadema katika jimbo la Kigoma Kusini hata kama Zitto atamuunga mkono mgombea wa NCCR-Mageuzi.

“Mimi binafsi sitamuunga mkono mgombea anayemsema Zitto, nitamuunga wa Chadema, ila siwezi kumsemea Zitto,” alisisitiza.

Awali kwa nyakati tofauti wanafunzi hao walimlalamikia Zitto kuwa amewagawa vijana, si ndani ya chama pekee bali hata nje kwa kile walichoeleza kuwa alikuwa mstari wa mbele kushawishi vijana waingie katika chama hicho lakini sasa anawavunja moyo kwa kauli zake kupitia vyombo vya habari.

Mwishoni mwa mwaka jana, kwa nyakati tofauti katika vyombo vya habari, Zitto ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, alinukuliwa akitoa kauli mbalimbali zilizoonesha kuwa kuna mpasuko na mgogoro mkubwa ndani ya chama lakini hata madai hayo yalipingwa vikali na viongozi wengine wa chama hicho akiwemo Mwenyekiti (Mbowe) na Katibu Mkuu, Dk. Wilbroad Slaa kuwa hakuna mgogoro bali uhuru wa kujieleza.

Maelezo hayo ya Zitto yaliunganishwa na wachambuzi wa mambo na matukio ya uchaguzi mkuu wa Chadema ambao Zitto alijitokeza kugombea nafasi ya uenyekiti wa chama hicho, kukabiliana na mwenyekiti aliyekuweko wakati huo, Mbowe.

Kujitokeza huko hata hivyo kulizua mtafaruku kwamba kiongozi huyo kijana alikuwa akikigawa chama. Hata hivyo, kabla ya kufanyika uchaguzi huo, Zitto aliyeonekana kuwa na msimamo wa kutaka kuwa Mwenyekiti mpya wa Chadema, aliitwa na Kamati ya Wazee wa chama hicho ikiongozwa na muasisi wa chama hicho, Mzee Edwin Mtei na baada ya kikao chake na wazee hao, alitoa barua ya kujitoa katika kinyang’anyiro hicho na hivyo Mbowe akagombea bila kuwa na mpinzani.

Baada ya uchaguzi huo, mgawanyiko huo ulidaiwa kujitokeza katika uchaguzi wa mabaraza ya vijana, wazee na wanawake ambapo baadhi ya chaguzi hizo ziliahirishwa kutokana na vurugu.

Baadaye waliokuwa wagombea wa baadhi ya nafasi katika chaguzi hizo, akiwemo Kafulila aliyekuwa ofisa habari wa chama, walijitoa Chadema baada ya kuondolewa nyadhifa zao katika chama hicho.

Awali kabla ya kujitokeza kwa kauli hizo zilizoonesha mgawanyiko huo, Mbowe aliwataka wanafunzi hao wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pamoja na kutoipigia kura CCM katika Uchaguzi Mkuu ujao, wahakikishe kuwa wanamrejesha chuoni aliyekuwa Mhadhiri wa Chuo hicho, Profesa Mwesiga Baregu ambaye mkataba wake uliisha na hakurejeshwa tena kazini ingawa yeye alikuwa tayari.

Alimtaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Kaimu Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Rwekaza Mukandala, kuhakikisha kuwa Prof. Baregu anarejeshwa chuoni hapo kwa kuwa bado utaalamu wake unahitajika kwa manufaa ya taifa hili na kueleza kuwa anaamini watu wenye chuki binafsi na Chadema ndiyo wamezuia ajira ya Prof. Baregu.

Nia ya kongamano hilo pamoja na mambo mengine ilikuwa kufafanua sera za chama hicho ambapo Mbowe alizungumzia mabadiliko ya mfumo wa utawala kupitia sera ya majimbo, unaolenga kumpunguzia Rais madaraka na kutoa ridhaa ya kuwapata viongozi kwa njia ya uchaguzi badala ya uteuzi.

“Sasa hivi Rais ana madaraka makubwa, kutoka Mungu ni yeye, hii sisi hatukubaliani nayo, endapo mkitupa ridhaa, Chadema inaamini katika mfumo wa utawala unaolenga kiongozi kuchaguliwa na wananchi, viongozi hao ni pamoja na Mkuu wa Wilaya, Mkuu wa Mkoa, wakurugenzi wa halmashauri, mameya, wabunge, madiwani na viongozi wa Serikali za Mitaa, ili wote wawajibike kwa wananchi badala ya ilivyo sasa kwa baadhi kuwajibika kwa Rais moja kwa moja,” alisema Mbowe.

Akizungumza wakati wa kutoa mada, Prof. Baregu bila kuonesha kuwa anataka kurudi chuoni hapo au la, alisema kuwa ilidaiwa moja ya mambo yaliyosababisha asipewe mkataba mwingine ni pamoja na kuwa na misimamo iliyowafanya wanafunzi aliowafundisha kuwa kama yeye japo mwenyewe haelewi ni misimamo gani.

“Binafsi sijui ni nini, lakini ninachoamini mimi kazi yangu kama Profesa ni kusisimua wanafunzi ili wajue kuchambua mambo na si kesho waniandikie insha ya kile nilichosema bali waboreshe nilichosema, naamini mwanafunzi bila kuasi si mwanafunzi, kuasi huko ni katika mitazamo, yaani usikubali kila kitu lazima uibue mjadala lakini sasa serikali inawajengea hofu kuogopa kujadili na kusema ukweli,” alisema Prof. Baregu.

Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa Chama hicho, John Mnyika akifafanua kuhusu sera ya majimbo, alisema, “wapo watu wanaeneza propaganda kwamba tunataka kuleta ukabila, hakuna kitu kama hicho, lengo ni kuinua hali ya dhamana na uchumi wa wananchi wa sehemu husika, mfano jimbo linalounganisha mikoa kama Mwanza, Mara, Bukoba na Shinyanga, litakuwa Jimbo la Ziwa, kuna ukabila gani hapo, tunataka madini yawanufaishe kwanza wakazi wake kabla ya Serikali Kuu.”

Akifafanua kuhusu hilo, Mbowe alisema CCM imeshindwa kupeleka huduma kwa wananchi ingawa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere pamoja na uadilifu wake na sera nzuri ya Ujamaa, alishindwa kuitekeleza kutokana na mfumo wa kikoloni uliokuwepo ambao upo mpaka leo na kwa kutumia sera ya Chadema, rasilimali za nchi zitawanufaisha wananchi.

Naye Mwanasheria Mkuu wa Chama hicho, Tundu Lisu katika mada yake, aliwataka vijana kuupinga Muswada wa Sheria ya Matumizi ya Uchaguzi usipitishwe kuwa sheria kwa kuwa una lengo la kuvimaliza vyama vya siasa vya upinzani ambavyo ruzuku yao ni kidogo ukilinganisha na CCM kwani unazuia mgombea kutumia fedha zake katika kampeni, wala kutumiwa kutoka nje ya nchi na wahisani au Watanzania walioko huko lengo likiwa ni kuzuia fedha haramu.

Source: Gazeti la Habari Leo
 
Wacha1

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2009
Messages
12,765
Likes
1,028
Points
280

Wacha1

JF-Expert Member
Joined Dec 21, 2009
12,765 1,028 280
Vipi wanagombea fweza za ruzuku? Lazima Chama Cha Majambazi wamewamwagia pesa za ruzuku hapo sio bure.
 
Papa Sam

Senior Member
Joined
Jan 10, 2008
Messages
102
Likes
0
Points
0

Papa Sam

Senior Member
Joined Jan 10, 2008
102 0 0
CHADEMA NI CHAMA IMARA, Zito ni Naibu Katibu Mkuu , mimi sioni kama kuna tatizo ziiito kama ambavyo mleta hoja anavyotaka kutuaminisha. mafisadi tu mnaweweseka, CHADEMA ipo Imara sana.
 
Tumain

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2009
Messages
3,158
Likes
11
Points
0

Tumain

JF-Expert Member
Joined Jun 28, 2009
3,158 11 0
CHADEMA NI CHAMA IMARA, Zito ni Naibu Katibu Mkuu , mimi sioni kama kuna tatizo ziiito kama ambavyo mleta hoja anavyotaka kutuaminisha. mafisadi tu mnaweweseka, CHADEMA ipo Imara sana.
Wishful thinking..keep on dreaming!

Chama imara chama imara? chadema imara hapa JF tu lakini kwenye ground hali yake ni mbaya subiri matokeo 2010.

Resources walizotumia na matokeo yake ni vitu viwili tofauti kabisa, ugomvi wake baada ya uchaguzi utakuwa maradufu...
 
Papa Sam

Senior Member
Joined
Jan 10, 2008
Messages
102
Likes
0
Points
0

Papa Sam

Senior Member
Joined Jan 10, 2008
102 0 0
Wishful thinking..keep on dreaming!

Chama imara chama imara? chadema imara hapa JF tu lakini kwenye ground hali yake ni mbaya subiri matokeo 2010.

Resources walizotumia na matokeo yake ni vitu viwili tofauti kabisa, ugomvi wake baada ya uchaguzi utakuwa maradufu...
Tumaini unaweza kuwa kweli lakini si kila tabiri huwa kweli mengine ni dua tu. ZINGINE NI TABIRI NA MAONO KAMA yA shehe Yahya Husein.
Kuiombea CHADEMA iPARANGANYIKE HUJAANZA WEWE , WALA mafisadi, Mrema bali imeanza na kina Mabere Marando na NCCR YAO MIAKA HIYO, KINYUME WAKAANGUKA WAO chadema IKO iMARA JAPO KUNA MATATIZO ya hapa na pale, CCM Inahatari zaidi ya kugawanyika kuliko CHADEMA .
 
Luteni

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Messages
2,274
Likes
10
Points
0

Luteni

JF-Expert Member
Joined Jan 9, 2010
2,274 10 0
Nimeanza kukubali kweli Chadema kipo imara na kipo serious, mwandishi anataka kulazimisha kuwa kuna mpasuko lakini mimi siuoni. Kauli ya mama Zitto ni ya kawaida kabisa kwamba yeye hawezi kumsemea mwanae kwanza ni mtu mzima aitwe mwenyewe afafanue kauli zake.

Hakuna mpasuko hapo ni mgongano wa mawazo tofauti tu, wala sijaona walichotofautiana na Mbowe. Kwa hiyo ni sisi wapokea habari kuzichuja na kuwa makini na waandishi wa aina hii kwa vile na wao pia wana interests zao.
 
Luteni

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Messages
2,274
Likes
10
Points
0

Luteni

JF-Expert Member
Joined Jan 9, 2010
2,274 10 0
Wishful thinking..keep on dreaming!

Chama imara chama imara? chadema imara hapa JF tu lakini kwenye ground hali yake ni mbaya subiri matokeo 2010.

Resources walizotumia na matokeo yake ni vitu viwili tofauti kabisa, ugomvi wake baada ya uchaguzi utakuwa maradufu...

You also keep on dreaming kuwa siku moja Chadema itagawanyika utasubiri sana kama fisi anavyofuatilia binadamu akifikiri mikono itadondoka achukue.

Baada ya uchaguzi wa 2000 watu walitabiri ndio mwisho wa Chadema bado ipo, wakasema Mbowe atajimaliza mwenyewe akigombea 2005 bado yupo, wakasema vile vile Chadema itasambaratika baada ya uchaguzi 2005 now is getting even stronger than ever.

Chadema sasa kimekomaa si cha kusambaratishwa na mtu mmoja tu. Chairman has been tested and Chadema as party it has been tested too. Kimepitia changamoto nyingi sana kimeshinda, chukulia mfano wa NCCR ya Mrema mgogoro mmoja tu kikagawanyika. NCCR walimalizwa na ruzuku Chadema waliliona hilo wakajiandaa nalo, pia naona Chadema inajitahidi sana kukabiliana na mamluki kitu ambacho NCCR ya Mrema ilishindwa.

Angalia hizi kauli za Zitto na uangalie jinsi viongozi wanavyo li-handle wametulia hawajibizani hovyo kwenye magazeti wako kimya ni sisi tu huku ndo tunapapatika, kama wasingekuwa makini kwa hili wangekimaliza chama mimi kweli nawapa credit wanazidi kukomaa.
 
All the best JF chadema fun/member or whetever..

2010 kwani mbali itakuwa nzuri mkiweza kupata wabunge watano wote mlio nao sasa ...

challenge ni kuongeza hata moja walau wawe sitta..tusubiri
 
Facts1

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2009
Messages
308
Likes
5
Points
0

Facts1

JF-Expert Member
Joined Dec 23, 2009
308 5 0
All the best JF chadema fun/member or whetever..

2010 kwani mbali itakuwa nzuri mkiweza kupata wabunge watano wote mlio nao sasa ...

challenge ni kuongeza hata moja walau wawe sitta..tusubiri
Kwani tatizo ni nini, kama wewe siyo Chadema fun au member waache Chadema na wabunge wao watano na wewe chukuwa hao wabunge 300 wa CCM uwapeleke nyumbani, naona JF tunataka kuwa kama watoto sasa kugombania sale sale maua, hapa leta hoja siyo ku swear subirini tuone.

I dont see any problem mtu kuwa mpenzi wa chama tofauti na chako sasa unataka wote tuwe CCM basi anza kampeni ubadili tena katiba iwe ya chama kimoja.
 
Ng'wanza Madaso

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2008
Messages
2,278
Likes
100
Points
145

Ng'wanza Madaso

JF-Expert Member
Joined Oct 21, 2008
2,278 100 145
All the best JF chadema fun/member or whetever..

2010 kwani mbali itakuwa nzuri mkiweza kupata wabunge watano wote mlio nao sasa ...

challenge ni kuongeza hata moja walau wawe sitta..tusubiri
Sasa hao wabunge mamia kadhaa wa ccm wamekusaidia nini zaidi ya kukutafuna mpaka sasa unavaa suruali ya kilaka, tunachomba ni wabunge wengi wa upinzani kuongezeka na kufuta hii kauli ya ndio mzee ya ccm,na kila kitu au muswada utakao pelekwa bungeni upite kwa uhalali si kwamba kwa sababu tuna wabunge wengi hata tukisema Watanzania wale nyasi wabunge wote watasema ndio mzee kwa sababu ya wingi wao.

Kwa hiyo tunachokitaka ni kupunguza huu utwana na umamuluki wa ccm na kulifanya Bunge lichangamke kwa hoja na vitendo.Waikosoe Serikali na serikali ikubali kukosolewa. Lakini kwa mfumo wa sasa kama hakutaongezeka wabunge wengi wa upinzani tutaendelea na umangimeza wa ccm wa ndio mzee kwa sababu ya wingi wao bungeni.
 
Ndusty

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2009
Messages
378
Likes
65
Points
45

Ndusty

JF-Expert Member
Joined Apr 27, 2009
378 65 45
We mtoa khabari ni mnafiki tu.kichwa chako cha khabari na habari uliyotoa haviendani.sioni mpasuko wowote ambao umetokea kutokana na maelezo ya mbowe na mama zitto.JF tuko kujadili mambo yanayojiri tanzania kwa kutumia common sense na bila unafiki au kutumwa na watu fulani.kama wewe ni wakutumwa basi this is not the right place..jaribu kwenda kuchangia mada zako kwenye magazeti ya udaku..hapa wachangia mada ni wasomi na watu wenye ku-reason sio wafuata upepo.Mlaaniwe nyie wote mnaopotosha watu kwasababu ya faida zenu pekee.Burn in hell!!!!!
 
Tumain

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2009
Messages
3,158
Likes
11
Points
0

Tumain

JF-Expert Member
Joined Jun 28, 2009
3,158 11 0
Sasa hao wabunge mamia kadhaa wa ccm wamekusaidia nini zaidi ya kukutafuna mpaka sasa unavaa suruali ya kilaka, tunachomba ni wabunge wengi wa upinzani kuongezeka na kufuta hii kauli ya ndio mzee ya ccm,na kila kitu au muswada utakao pelekwa bungeni upite kwa uhalali si kwamba kwa sababu tuna wabunge wengi hata tukisema Watanzania wale nyasi wabunge wote watasema ndio mzee kwa sababu ya wingi wao.

Kwa hiyo tunachokitaka ni kupunguza huu utwana na umamuluki wa ccm na kulifanya Bunge lichangamke kwa hoja na vitendo.Waikosoe Serikali na serikali ikubali kukosolewa. Lakini kwa mfumo wa sasa kama hakutaongezeka wabunge wengi wa upinzani tutaendelea na umangimeza wa ccm wa ndio mzee kwa sababu ya wingi wao bungeni.
hao wa chadema wananisaidia nini? jisaidie mwenyewe...
 
Majasho

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2009
Messages
341
Likes
8
Points
35

Majasho

JF-Expert Member
Joined Aug 4, 2009
341 8 35
CHADEMA ni chama binafsi, na huo mpasuko upo, tena mk sana, sema huyo mchungaji wao Dkt Slaa anamuogopa Zitto, kauli za Zitto ni za kinafiki maana huwezi kusema eti utamuunga mkono mgombea mwingine hata kama CHADEMA wakisimamisha mgombea. Inamaanisha ataenda kumnadi Kafulila huko Kgoma, na uongozi wa CHADEMA huko Kigoma nao watamuunga mkono nani..mgombea wao au wa Zitto. CHADEMA humu ndani mmejaa na mtaongea chochote tu kuitetea, kama Zitto angeamua kumuunga mkono Mrema huko Vunjo wote mngekuja juu wana CHADEMa.

ukweli ni kwamba uongozi unamuogopa Zitto na ndicho kinachompa kiburi, na uhakukka hata Slaa anajuta kwanini alimvua Kafulila uongozi wake, hakutegemea kama hii tamthilia ingekuwa na twist and turns, wao wanakausha tu kwasababu CHADEMA inajipanga towards the election in october. Zitto kashaleta mpasuko in and out CHADEMA na wakimuendeleza atakipasua CHADEMA kati kati. na mama yake Zitto atamuunga mwanae mkono so asituletee unafiki hapa JF, maana nauhakika yeye hua anmshauri Zitto mara kwa mara.

Zitto anataka uenyekiti, mama yake katibu mkuu, MBOWE NA MCHUNGAJI SLAA hawaelewI
 
Kigogo

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2007
Messages
20,559
Likes
1,561
Points
280

Kigogo

JF-Expert Member
Joined Dec 14, 2007
20,559 1,561 280
Wishful thinking..keep on dreaming!

Chama imara chama imara? chadema imara hapa JF tu lakini kwenye ground hali yake ni mbaya subiri matokeo 2010.

Resources walizotumia na matokeo yake ni vitu viwili tofauti kabisa, ugomvi wake baada ya uchaguzi utakuwa maradufu...
wewe ndio sifuri kabisa..kwani babako alivokulea na resources alizotumia kukufikisha hapo ulipo ni sawa na jinsi ulivyo sasa..Mawazo ya kimakengeza kabisa hayo..
Toka lini JF ni jukwaa la kuimarisha vyama na kuvipima katika mizani ya uimara?
 
Forum statistics

Threads 1,190,580
Members 451,229
Posts 27,675,890