Mpango wowote wa TRA kukamata wasiodai risiti hautofanikiwa hadi pale Wamachinga watakapoondolewa

Kuna siku nilikuwa naenda Sumbawanga from Mbeya. Sasa kufika Tunduma nikaona abiria wengi tuu wananunua sukari from Zambia ambazo wamachinga wanauza openly hapo Tunduma. Tulipofika huko mbele wakaingia TRA na kutaka eti kukamata abiria walionunua sukari, which was 2 to 3 kgs kwa walio wengi. Bwana wee watu wakachachamaa kwamba how come hawaendi kuwakamata wauzaji pale Tunduma? Wengine wakasema wamenunua Mbeya kwenye maduka, yaani ilikuwa balaa, mwishowe ilibidi waondoke tuu.
hahahaha watu wengi wanaokwepa ussue za kodi wanawatumua machinga....mtu anaduka lake ila bidhaa asilimia 40 zinatembezwa nje na machinga......

mkuu ila hiyo sukari nitaifuata nione kama inaquality nzuri. ...vipi upande wa Flat screen Tunduma bei ni nzuri au sawa na mbeya mjini?
 
Naunga mkono hoja yako ni kweli kabisa kuwa ni vigumu kuwa kamata watu ambao watakutwa na bidhaa zisizo na lisiti kwani wafanya biashara wanawatumia wamachinga kukwepa kodi huo ndio ukweli
 
Usinilishe maneno , kwani wamachinga mnaowapa vitambulisho hawana biashara zao wenyewe , na je mliwapa mashine za EFD ?
 
Ni vigumu sana kujua nani kanunua bidhaa zake wapi, hii ni kwa sababu Wamachinga wanauza kila kitu kinachouzwa madukani tena bila kikwazo chochote.

Wamachinga wanauza nguo, simu, vifaa vya simu, vifaa vya mahospitalini, vifaa vya shule, TV , vifaa vya majumbani na maofisini, ikiwa ni pamoja na dawa za binadamu, dawa za meno na dawa za magonjwa mengine zinapangwa barabarani kuanzia Kariakoo, Manzese hadi Mbagala huku zikipigwa jua kutwa nzima.

Wamachinga hawana machine za EFD na wala hawabughuziwi kwenye hilo huku wakifanya biashara kubwa kuliko wenye maduka na taarifa za sasa za Kariakoo zinaonyesha kwamba Wamachinga ni almost 70% ya wafanyabiashara wote, sasa kwa hali hii unawezaje kumuuliza mtu risiti ya alichonunua?

Labda TRA iseme kwamba imelenga kuwakomoa wauzaji wa jumla ambao ndio unaweza kuwatofautisha na wengine, Vinginevyo TRA yaweza kushitakiwa mahakamani kwa kumkamata aliyenunua kwa wamachinga ambao wanauza kila kitu kuliko hata maduka halali, maana hakuna duka lolote la halali linaloweza kuuza kandambili, chupi za watoto na humo humo likauza na dawa za binadamu pamoja na sumu za panya.

Ikumbukwe pia kwamba Watanzania hawajui lolote kuhusu sheria za uuzaji wa baadhi ya bidhaa , wanachoangalia ni bei rahisi pekee , kwahiyo kumkamata huku akiwa kanunua kihalali kwa muuzaji aliyevaa kitambulisho halali cha Mmachinga utakuwa uonevu wa kutisha.
TRA wangekuwa wanaweza kuelewa uhalisia Basi ningewashauri waachane na hivyo vimashine. Toka vianzishwe zimepelekea kwa asilimia nyingi kuyumbisha biashara. Muuzaji akisema kiukweli kabisa kabisa akitumie Kama TRA walivyomeza Basi hiyo Kodi yake hawezi kuilipa na akiilipa Basi ujue amechota hadi kwenye mtaji, kwahiyo badala ya biashara kukua inaendelea kudhoofika.

Biashara hasa ya duka badala ya kukua believe me litaendelea kupwaya na hatimae kufa, ambalo kimsingi halipaswi kuwa lengo.
TRA wanavyomkomalia mtu mwenye kaduka at the same time wanatakiwa kutambua kodi zote anazolipa huyo mwenye kaduka zinazotoka humo humo ambapo na yeye anategemea kakue aendeshe pia maisha mengine
Mfano

TRA
Lesen
Service Levy
Ulinzi
Usafi
Fire
Afya
Frem

Hawa wote wanafika mlangoni kudai pesa. Haya mazingira kiuhalisia yana dhoofisha msingi na hatimae biashara kufa.

TRA ningewashauri waachane na mfumo wa kusema wanakadiria Kodi kutokana na Mauzo. Huo mfumo si sahihi na hauna uhalisia wa faida anayopata mwenye kaduka.

Biashara ya duka iwe jumla au rejareja ni biashara ambayo faida huwekwa ndogo Sana
Mfano hai let say mie nauza maji kwa jumla
Katoni moja naiuza 2500 hapo faida ni 100.

Kwa siku ikitokea nipo sehem ninayoweza uza katoni 100 kwa siku ina maana faida yangu kwa siku Ni elf10 tu. Na hapo TRA yeye kunikadiria kodi atauliza mauzo /day which means kwa mauzo ya katoni 100 niliyopata elf10 tu Kama faida yeye atapigia kwa 250000

250000x28x12 =84M then atakokotoa Kodi toka hapo wakati kiuhalisia wewe mtaji wako ni laki 2 na elf40 na ulikuwa unapata faida elf 10 Kila ambapo kwa mwezi Ni laki3 kwa mwaka Ni 3.6M
Sasa cheki hiyo difference wewe.

Sasa fahsm kwa kaduka kavinywa ambako unaweza uza katoni 100 /day ujue upo center mno na Kodi ya frem lazima iwe laki2 and above kwa mwezi ikiwa laki2 tu tayari frem unalipia 2.4 M
Sasa endelea kutoa hayo malipo unayotakiwa kulipia then ona Kama hiyo biashara Kama inaweza kuwa.
 
Hiv TRA uwa wanajaribu kuwahusisha wafanya biashara wanapotaka kufanya maamuzi yao kwel? Ama ndio ile sisi ni wasomi tunauwezo wa kufanya maamuzi na mamlaka tunayo.
 
Hao ni wasomi waliotukuka , wanawezaje kuwasikiliza wengine ?
 
Katika jambo la hovyo serikali imejipiga ngwala ni kuruhusu machinga kila sehemu ...

Watu wanafunga maduka yao anatafuta vijana anawapa mizigo wanakuwa machinga na hawalipi Kodi ...

Serikali nawaomba acheni kuingiza siasa kwenye kila kitu, hapo TRA Wu weenda shule acheni watumie elimu zao kukusanya kodi. Mambo mengi hapo TRA yanafanywa na wanasiasa.
 
Watu wakipigwa faini wataacha kununua vitu barabarani na badala yake kuingia madukani na kununua humo. Huu msako ukifanywa kwa weledi utawaondoa Wamachinga wote wanauza vitu vya madukani barabarani na hivyo kuongeza pata la Taifa.
Yaani ninunue kitu kwa machinga we ti ara ei uje unipige faini? Haki yamungu nakufa na wewe, Hilo timbwili lake, mpaka jamii itashangaa,wawape basi risiti chinga.vinginevyo hao ti ara ei wakajifunze upya
 
Ni vigumu sana kujua nani kanunua bidhaa zake wapi, hii ni kwa sababu Wamachinga wanauza kila kitu kinachouzwa madukani tena bila kikwazo chochote.

Wamachinga wanauza nguo, simu, vifaa vya simu, vifaa vya mahospitalini, vifaa vya shule, TV , vifaa vya majumbani na maofisini, ikiwa ni pamoja na dawa za binadamu, dawa za meno na dawa za magonjwa mengine zinapangwa barabarani kuanzia Kariakoo, Manzese hadi Mbagala huku zikipigwa jua kutwa nzima.

Wamachinga hawana machine za EFD na wala hawabughuziwi kwenye hilo huku wakifanya biashara kubwa kuliko wenye maduka na taarifa za sasa za Kariakoo zinaonyesha kwamba Wamachinga ni almost 70% ya wafanyabiashara wote, sasa kwa hali hii unawezaje kumuuliza mtu risiti ya alichonunua?

Labda TRA iseme kwamba imelenga kuwakomoa wauzaji wa jumla ambao ndio unaweza kuwatofautisha na wengine, Vinginevyo TRA yaweza kushitakiwa mahakamani kwa kumkamata aliyenunua kwa wamachinga ambao wanauza kila kitu kuliko hata maduka halali, maana hakuna duka lolote la halali linaloweza kuuza kandambili, chupi za watoto na humo humo likauza na dawa za binadamu pamoja na sumu za panya.

Ikumbukwe pia kwamba Watanzania hawajui lolote kuhusu sheria za uuzaji wa baadhi ya bidhaa , wanachoangalia ni bei rahisi pekee , kwahiyo kumkamata huku akiwa kanunua kihalali kwa muuzaji aliyevaa kitambulisho halali cha Mmachinga utakuwa uonevu wa kutisha.
Umeandika kitu cha kweli kabisa.nimeenda pale karume ,nikakuta mabegi yametundikwa,nikapiga haraka haraka hesabu ,nikagundua yule jamaa mtaji wake ni zaidi ya chinga wa kawaida ,nikajichekea mwenyewe kwamba muuzaji anatumia kitambulisho cha mmachinga
 
Kwamba wamachinga wako exempt kutoa risiti za mauzo? kama mdau hapo juu alivyosema ,wangewatafutia tuu kidigital flan hivi simple,pos machine kama zile wanazolipia parking za magari.ili watoe reciept.

serikali iingie gharama ya kuwakopesha
 
Ni vigumu sana kujua nani kanunua bidhaa zake wapi, hii ni kwa sababu Wamachinga wanauza kila kitu kinachouzwa madukani tena bila kikwazo chochote.

Wamachinga wanauza nguo, simu, vifaa vya simu, vifaa vya mahospitalini, vifaa vya shule, TV , vifaa vya majumbani na maofisini, ikiwa ni pamoja na dawa za binadamu, dawa za meno na dawa za magonjwa mengine zinapangwa barabarani kuanzia Kariakoo, Manzese hadi Mbagala huku zikipigwa jua kutwa nzima.

Wamachinga hawana machine za EFD na wala hawabughuziwi kwenye hilo huku wakifanya biashara kubwa kuliko wenye maduka na taarifa za sasa za Kariakoo zinaonyesha kwamba Wamachinga ni almost 70% ya wafanyabiashara wote, sasa kwa hali hii unawezaje kumuuliza mtu risiti ya alichonunua?

Labda TRA iseme kwamba imelenga kuwakomoa wauzaji wa jumla ambao ndio unaweza kuwatofautisha na wengine, Vinginevyo TRA yaweza kushitakiwa mahakamani kwa kumkamata aliyenunua kwa wamachinga ambao wanauza kila kitu kuliko hata maduka halali, maana hakuna duka lolote la halali linaloweza kuuza kandambili, chupi za watoto na humo humo likauza na dawa za binadamu pamoja na sumu za panya.

Ikumbukwe pia kwamba Watanzania hawajui lolote kuhusu sheria za uuzaji wa baadhi ya bidhaa , wanachoangalia ni bei rahisi pekee , kwahiyo kumkamata huku akiwa kanunua kihalali kwa muuzaji aliyevaa kitambulisho halali cha Mmachinga utakuwa uonevu wa kutisha.

I agree with you 100%.
 
Back
Top Bottom