Mpango wa kuwawekwa kizuizini Viongozi CHADEMA waiva? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mpango wa kuwawekwa kizuizini Viongozi CHADEMA waiva?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Mar 19, 2013.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Mar 19, 2013
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,893
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  [​IMG]CCM vs CHADEMA [​IMG]

  Inakuja sasa mpango mpya wa kutolea kafara watu ili kujenga hoja ya kubambikiza kesi za kijasusi sheria ambayo haiwapi dhamana wala kuwatoa vifungoni hadi uchaguzi Mkuu upite, wakati tukijua sheria za kugombea vyeo kisiasa aliyekwisha onja kifungo cha muda uliowekwa kisheria haruhusiwi kugombea nafasi za uwakilishi na ukuu wa nchi. Mbaya zaidi vyombo vya dola vinapojenga mfumo wa kuegemea upande mmoja kiutendaji badala ya mfumo wa kutofungamana upande wo wote ili kutendea haki wananchi wote maana dola na vyombo vyake ni mali ya wananchi katu kisheria si miliki ya chama fulani.

  Katika kile kilichoelezwa na Wasira hadharani kwamba Chadema itasambaratika katika mwaka huu, dalili za wazi zimeanza kujionyesha kwa suala la Rwekatare. Hoja za Chadema zinaonekana kuwa nzito na za kueleweka na kwa lugha inayoeleweka kwa wananchi. CCM kujenga ushawishi kwa wananchi inaelekea kugonga mwamba kwa sababu hoja zao hazionyeshi uwezo wa kuzipiku zile za Chadema. Wananchi wanapokea hoja za upende wa upinzani kutokana na hali halisi ilivyo nchini kwa sasa. Kwa mantiki hiyo CCM kinachoendelea ni kujaribu kutumia zaidi nguvu ili kuendelea kushika dola kwa nguvu badala ya ridhaa ya kidemokrasia.
  Hivi wajibu wa Wasira katika wizara yake sera na taratibu ni kuratibu sera na taratibu za kuangamiza demokrasia nchini?

  Tangazo la Chadema la kujiimarisha kikanda linaonekana kutibua nyongo za CCM, maana kwa mfumo huo ni dhahiri mtandao wa Chadema utakuwa na nguvu ya ziada kanda zote na kuwa na nafasi ya kupenya kotekote mikoani hadi vijijini ambako CCM inajivunia kuwa hazina ya ushindi wake. CCM ilibweteka kwa hoja kwamba vyama vya upinzani ni vya msimu na havikubaliki vijijini ambako kuna wapiga kura asilimia 80. Leo mambo yamegeuka ni sera ndiyo yenye kuteka wapiga kura badala ya mazoea ya rangi ya chama.

  [​IMG]
  Kauli ya Kikwete Mkutano Mkuu CCM Dodoma ni ya uchochezi?
  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mkutano wa CCM mjini Dodoma alitoa kauli kwamba atahakikisha kwa njia ye yote anaukabidhi urais kwa CCM si chama cha Upinzani.

  Rais ni wa wananchi wote wa Tanzania bila kujali itikadi akisha shika kiti cha Ikulu ni wa wote. Waliomchagua ni watanzania wote wakiwemo CCM na vyama vingine vya siasa hali kadhalika wasio wanachama wa chama cho chote. Kauli ile kimantiki si sahihi kwa Kiongozi wa nchi, maana kwa kauli ile kwa mamlaka aliyo nayo anaweza akayatumia vibaya madaraka yake kwa sababu tu ametamka wazi kwamba atafanya kila liwezekanalo kuhakikisha urais anamwanchi mwanachama wa CCM. Kauli ile ielewekaje?​

  Polisi kutotenda haki usawa kwa vyama vyote vya siasa
  [​IMG]
  Kashfa ya Mwigulu Mchemba Dola kutochukulia hatua stahiki


  • [*=1]Kashfa alizonazo Mwigulu Mchemba kuhusika kutuma gari lililojaa vijana kwenda kuvuruga mkutano wa Chadema na kusababisha kifo cha mtu mmoja huko mkoani Singida, polisi kutoa ushuhuda huo mahakamani, lakini Mwigulu Mchemba hajaitwa kutoa maelezo polisi na alitakiwa akamatwe kuunganishwa katika kesi hiyo.
   [*=1]Mwigulu Mchemba katika uchochezi kwamba anazo kanda za video za Chadema kupanga mauaji hajaitwa na vyombo vya dola kutoa ufafanuzi and to release kanda hizo kama ushahidi ili vyombo vya dola vifanyie kazi.

  Zuio la mikutano ya hadhara dola huthibiti upinzani tu
  Wakati wa zuio la mikuano ya hadhara, CCM ruksa kufanya mikutano ya hadhara na hawabughudhiwi na vyombo vya dola lakini vyama vya upinzani wakati wa zuio hata mikutano ya ndani husambaratishwa hadi kusababisha majeruhi na mauaji.​

  Tuko la kuuawa mwanahabari wa Chanel Ten huko Iringa ni mfano dhahiri ambapo zuio la mikutano ya hadhara kwa sababu ya zoezi la kuhesabu watu wakati Chadama walikuwa na mkuano wa ndani wakati huo huo CCM ikifanya mkutano mkuwa wa hadhara huko kisiwani Unguja na mkutano mkubwa mwingine wa tamasha kwenye uwanja mojawapo huku bara lakini hawakuguswa na sheria hiyo.​

  Pamoja na mengi ambayo yanaelekea Chadema kushikishwa adabu kwa sheria zilezile zinazovunjwa na CCM kutoshikishwa adabu inatia shaka katika vyombo vya dola kutendea haki watanzania, vyama vya siasa ambavyo vyote vina haki sawa kikatiba na wananchi kwa ujumla. Vyama vyote vinawakilisha wananchi walewale walio chini ya dhamana ya kulindwa na vyombo vile vile vya dola.

  [​IMG] [​IMG]
  Ushindani wa kweli ni hoja, sera na pengine hata utani
  Ushindani wa kisiasa si vita, bali hoja na sera
  Tujifunze kuendesha siasa za ustaarabu kwa kutumia hoja na kuuza sera kwa wananchi kwa nguvu ya hoja badala ya kuendesha siasa kwa kutumia mfumo wa hoja ya nguvu. Mambo yakielekea kukukalia vibaya bora kutulia na kuangalia wapi umeteleza, jipange upya na mkakati mpya ili kuanza kujenga ushawishi wenye kuwakuna wananchi. Chama kinachoshika dola kina nafsi zaidi ya kuonyesha utendaji wake ili kuwavutia wananchi kuliko chama ambacho kisicho shika dola kwa vile kinanadi sera bila utekelezaji. Kitanzi kwa chama chenye kushika dola ni pale kinapohangaika majukwaani kunadi sera wakati ndio watekelezaji wa sera walizozinadi kipindi cha uchaguzi.

  Wapigania haki si Wanachadema bali wapenda mabadiliko ya kweli
  Wapigania haki tulio wengi si wanachama wa chama fulani ila ni wapenda maendeleo na mabadiliko ya kweli kwa manufaa ya nchi bila kujali chama gani kifanikishe kuibadili Tanzania ya leo iwe tuitakavyo.

  Sera ambazo zinatukuna wapigania haki na wananchi ndizo zinazofanya tupende sera hizo si chama. Ushindani wa kimaendeleo ni pale miamba miwili inaposhindana katika kujenga nchi badala ya mmoja asiye na upinzania hatakuwa na ushindani wa kweli bali kuongoza nchi kwa mazoea. Hiyo ndiyo njia nzuri ya kukuza uongozi unaojengeka kwa misingi ya kidemokrasia kwa kupinduana kwenye masanduku ya kura.

   
 2. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #2
  Mar 19, 2013
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,300
  Likes Received: 2,400
  Trophy Points: 280
  Watanzania wanataka Mabadiliko Bila kujali hayo Mabadiliko yataasaidia nini au bila kujali waleta mabadiiko ni watu wa aina gani, so hata wangefungua kesi ngapi hazitasaidia kitu chochote
   
 3. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #3
  Mar 19, 2013
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,383
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Makaburu wamezaa ngozi nyeusi. Ngoja tuone. Ila wachunge saana amani.
   
 4. f

  fakisi Member

  #4
  Mar 19, 2013
  Joined: Sep 4, 2012
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ningependa Rais Kikwete avunje vyama vyote ibaki CCM tu, maana hakuna maana ya kuwa na vyama vingi ikiwa dola, mahakama n.k. havitoa haki sawa kwa vyama vingine! Dola ishaona usipokuwa mwanaCCM basi wewe ni gaidi, jasusi n.k. Tunapoteza pesa na muda tu, ibaki CCM wafanye watakalo au vinginevyo tutapitia the hard way ambacho sio kitu kizuri
   
 5. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #5
  Mar 19, 2013
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,738
  Trophy Points: 280
  kwa mpango huu wa kutumia vyombo vya dola kama walivyotumia makaburu Afrika Kusini sasa natoa rai kwa upinzani tutumie mbinu zile zile walizotumia ANC kukabiliana na udhalimu huu.Tuna base support ya kutosha,tupo na umma.Tusikubali kurudi nyuma.

  Na sisi tuwaonyeshe rangi halisi ya wanamageuzi baada ya wao kutuonyesha rangi halisi ya ukoloni na ukandamizaji

  Tukiwaonyesha woga wetu, itakua silaha imara zaidi kwao kutumaliza
   
 6. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #6
  Mar 19, 2013
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,977
  Likes Received: 6,672
  Trophy Points: 280
  BLACKEYED PEAS FT. JUSTIN TIMBERLAKE

  "Where Is The Love?"

  What's wrong with the world, mama
  People livin' like they ain't got no mamas
  I think the whole world addicted to the drama
  Only attracted to things that'll bring you trauma

  Overseas, yeah, we try to stop terrorism
  But we still got terrorists here livin'
  In the USA, the big CIA
  The Bloods and The Crips and the KKK

  But if you only have love for your own race
  Then you only leave space to discriminate
  And to discriminate only generates hate
  And when you hate then you're bound to get irate, yeah

  Madness is what you demonstrate
  And that's exactly how anger works and operates
  Man, you gotta have love just to set it straight
  Take control of your mind and meditate
  Let your soul gravitate to the love, y'all, y'all

  People killin', people dyin'
  Children hurt and you hear them cryin'
  Can you practice what you preach
  And would you turn the other cheek

  Father, Father, Father help us
  Send some guidance from above
  'Cause people got me, got me questionin'
  Where is the love (Love)

  Where is the love (The love)
  Where is the love (The love)
  Where is the love, the love, the love

  It just ain't the same, always unchanged
  New days are strange, is the world insane
  If love and peace are so strong
  Why are there pieces of love that don't belong

  Nations droppin' bombs
  Chemical gasses fillin' lungs of little ones
  With ongoin' sufferin' as the youth die young
  So ask yourself is the lovin' really gone

  So I could ask myself really what is goin' wrong
  In this world that we livin' in people keep on givin' in
  Makin' wrong decisions, only visions of them dividends
  Not respectin' each other, deny thy brother
  A war is goin' on but the reason's undercover

  The truth is kept secret, it's swept under the rug
  If you never know truth then you never know love
  Where's the love, y'all, come on (I don't know)
  Where's the truth, y'all, come on (I don't know)
  Where's the love, y'all

  People killin', people dyin'
  Children hurt and you hear them cryin'
  Can you practice what you preach
  And would you turn the other cheek

  Father, Father, Father help us
  Send some guidance from above
  'Cause people got me, got me questionin'
  Where is the love (Love)

  Where is the love (The love)?
  Where is the love (The love)?
  Where is the love, the love, the love?

  I feel the weight of the world on my shoulder
  As I'm gettin' older, y'all, people gets colder
  Most of us only care about money makin'
  Selfishness got us followin' our wrong direction

  Wrong information always shown by the media
  Negative images is the main criteria
  Infecting the young minds faster than bacteria
  Kids wanna act like what they see in the cinema

  Yo', whatever happened to the values of humanity
  Whatever happened to the fairness in equality
  Instead of spreading love we're spreading animosity
  Lack of understanding, leading us away from unity

  That's the reason why sometimes I'm feelin' under
  That's the reason why sometimes I'm feelin' down
  There's no wonder why sometimes I'm feelin' under
  Gotta keep my faith alive till love is found
  Now ask yourself

  Where is the love?
  Where is the love?
  Where is the love?
  Where is the love?

  Father, Father, Father, help us
  Send some guidance from above
  'Cause people got me, got me questionin'
  Where is the love?

  Sing with me y'all:
  One world, one world (We only got)
  One world, one world (That's all we got)
  One world, one world
  And something's wrong with it (Yeah)
  Something's wrong with it (Yeah)
  Something's wrong with the wo-wo-world, yeah
  We only got
  (One world, one world)
  That's all we got
  (One world, one world)
   
 7. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #7
  Mar 19, 2013
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,383
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Like Serafina kike Ben, I like that. If they want to take our right from us by force, they loose legitimacy of being faithful to the constitution so they shall be without.
   
 8. F

  FUSO JF-Expert Member

  #8
  Mar 19, 2013
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 12,685
  Likes Received: 3,050
  Trophy Points: 280
  CDM cha kufanya ni kujikita zaidi uelimisha umma wa watazania hasa wa vijijini juu ya umuhimu wa mabadiliko, kwa nini tunahitaji mabadiliko na kwa manufaa ya nani hasa?

  Ukiwa na umma wa watanzania nyuma yako your safe, umma wa watanzania ndiyo backbone yenu, CCM wafanya wafanyavyo kwa sasa lakini mbele ya safari mambo ya kupika huwa yanadunda. utafunga wangapi/ utafungulia kesi wangapi kama umma mzima upo tayari kwa mabadiliko?

  Wao wana dola nyie mna watu, na huo ndiyo mtaji mkubwa sana mlionao kwa sasa, move on CDM.
   
 9. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #9
  Mar 19, 2013
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,827
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  TATIZO NIKWAMBA WANACCM WANASOMA BAONI MAZURI YA WANANCHI LAKINI WANAONA KAMA KELELE ZA MRANGO AMBAZO HAZIMNYIMI MWENYE NYUMBA uSINGIZI
   
 10. m

  mob JF-Expert Member

  #10
  Mar 19, 2013
  Joined: Dec 4, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 571
  Trophy Points: 280
  ndo maana napendaga sana huu wimbo wa bob marley.

  Old pirates, yes, they rob I;
  Sold I to the merchant ships,
  Minutes after they took I
  From the bottomless pit.
  But my hand was made strong
  By the 'and of the Almighty.
  We forward in this generation
  Triumphantly.
  Won't you help to sing
  This songs of freedom
  'Cause all I ever have:
  Redemption songs;
  Redemption songs.

  Emancipate yourselves from mental slavery;
  None but ourselves can free our minds.
  Have no fear for atomic energy,
  'Cause none of them can stop the time.
  How long shall they kill our prophets,
  While we stand aside and look? Ooh!
  Some say it's just a part of it:
  We've got to fullfil the book.

  Won't you help to sing
  This songs of freedom-
  'Cause all I ever have:
  Redemption songs;
  Redemption songs;
  Redemption songs.
  ---
  /Guitar break/
  ---
  Emancipate yourselves from mental slavery;
  None but ourselves can free our mind.
  Wo! Have no fear for atomic energy,
  'Cause none of them-a can-a stop-a the time.
  How long shall they kill our prophets,
  While we stand aside and look?
  Yes, some say it's just a part of it:
  We've got to fullfil the book.
  Won't you have to sing
  This songs of freedom? -
  'Cause all I ever had:
  Redemption songs -
  All I ever had:
  Redemption songs:
  These songs of freedom,
  Songs of freedom.
   
 11. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #11
  Mar 19, 2013
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,893
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Mdharau mwiba mguu huotea tende. Yale yale vyama vya upinzani ni vya msimu, leo vinatutoa kamasi hadi kuchukua majambia.
   
 12. N

  Ngandema Bwila JF-Expert Member

  #12
  Mar 19, 2013
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 999
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  HAKUNA MAHALI UDHALIMU ULISHIDA , THOSE ARE QUICK FIX SOLUTIONS, VITISHO, PROPAGANDA, AHADI HEWA, MAKATAZO, UBABE na MAGUVU ni mbinu za watu wasio UNA MBALI, Wasio soma historia, wavivu, waoga na wenyepupa na wasiotunza kumbukumbu ya hata mambo yaliyotokea siku mbili nyuma. NDIO MAANA UTAMSIKIA MTU ANAULIZA ELIMU YA MTU WAKATI YEYE MWENYEWE ALIPATA ZIRO.
   
 13. m

  majebere JF-Expert Member

  #13
  Mar 19, 2013
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 591
  Trophy Points: 280
  Wewe subiri ukajieleze ule unga uliutoa wapi na nani alikutuma ukamuue Zitto.
   
 14. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #14
  Mar 19, 2013
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Serikali hii isipoangalia itaifanya nchi hii isitawalike. Watz wa sasa siyo wale wa mwaka 1947 wanaotishwa wakatishika, wanadanganywa wakadanganyika, na wanaolishwa propaganda wakaziamini. Not this time any more.
   
 15. master peace

  master peace JF-Expert Member

  #15
  Mar 19, 2013
  Joined: Dec 19, 2012
  Messages: 1,451
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Muishiwa dhaifu hana hiyo jeuri; Chezea the Hegue weyee...
   
 16. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #16
  Mar 19, 2013
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,827
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  DHAIFU SANa
   
 17. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #17
  Mar 19, 2013
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Lazima watz wataamka na ccm itaaibika na proganda zake soon.
   
 18. Kocha

  Kocha JF-Expert Member

  #18
  Mar 19, 2013
  Joined: Mar 2, 2008
  Messages: 375
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Kwa hali ilivyo sasa hivi mpango wao ni kutoachia madaraka na ikibidi watu kwa maelfu wata uawa ili mradi wao waendelee kukaa madarakani
   
 19. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #19
  Mar 19, 2013
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,827
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  DHAIFU SANa
   
 20. m

  majebere JF-Expert Member

  #20
  Mar 19, 2013
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 591
  Trophy Points: 280
  Nyie ndio nia yenu hiyo, hata viongozi wenu wanataka nchi isitawalike, hii ni TANZANIA ndugu yangu, sheria ziko za kuwaweka sawa.
   
Loading...