maramia
JF-Expert Member
- Jul 17, 2015
- 2,030
- 1,345
Ni jambo jema serikali kuhakikisha inakusanya kodi kutoka kila chanzo halali kadri inavyowezekana lakini kuna vyanzo vingine inatakiwa iwe makini sana katika kuvianzisha na kuvisimamia.
Mara nyingi masuala yahusuyo nyumba huwa ni magumu sana katika kuyasimamia, kumbukeni hata huko Marekani ndiyo yaliyoiletea nchi hiyo mdororo wa uchumi miaka michache iliyopita pale serikali ilipojaribu kuingilia ujenzi na bei ya mauzo ya nyumba mpya zilizokuwa zinajengwa.
Hata hapa kwetu serikali kwa kushindwa kuzisimamia na kuziendesha nyumba zake ndiyo maana yenyewe iliamua kuziuza na kuwaacha watumishi na wafanyakazi wake wakiishia kupanga nyumba za watu binafsi.
Kwa hiyo tukubaliane kwamba kitendo chochote cha serikali kuwapangia wenye nyumba kiasi cha pango watakachopangisha na wakati huo huo kuwalipisha kodi fedha watakayopata kwa kupangisha itasababisha athari mbili kubwa:
1. Wapangaji ndio watakaobebeshwa mzigo wa ongezeko lolote litakaloletwa na serikali.
2. Watumishi na wafanyakazi wengi wataondolewa kwenye nyumba kwa visingizio tofauti tofauti.
Binafsi ningeshauri kabla serikali haijaingia katika migogoro na wenye nyumba, ijiandae kwa kujenga nyumba za watumishi wake na nyingine za kupangisha kama ilivyokuwa siku za nyuma badala ya kukomalia nyumba zilizojengwa na watu binafsi, wengine kwa kujinyima na adha kubwa.