Mpango wa kuwakabidhi Makaburu Ngorongoro ulivyozimwa na Vita 1 ya Dunia!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,786
Kwa wasiofahamu Bonde la Ngorongoro ambalo leo nii ni hifadhi imekuwa hivyo tangia mwaka 1959 tu, lkn kabla ya hapo lilikuwa ni Mali binafsi ya Settler wa Kijerumani aliyejulikana kama Adolf Siedentopf ambaye mwaka 1904 aliomba Kibali kutoka kwa Serikali ya Kikoloni ya Kijerumani ili aweze kufugia mifugo yake!

Kabla ya hapo Bonde hilo lilikuwa likikaliwa na Wamasai ambapo baada ya settler kupewa kibali na Serikali ya Kijerumani, mwaka 1907 Wamasai walifukuzwa na kupigwa marufuku kukanyaga kwenye eneo hilo na walihamishiwa sehemu ya kusini mwa Mlima Kilimanjaro!

Sasa lengo Kuu la Wazungu lilikuwa ni kuwaleta Makaburu kutoka AK kama settlers na kuwakabithi eneo hilo kwa ajili ya ufugaji na kilimo, lkn mpango uliingiliwa na Vita ya kwanza ya Dunia ambapo baada ya Wajerumani kushindwa, Vita Waingereza walikabidhiwa nchi yetu na kuligeuza eneo hilo lililokuwa Mali ya mtu binafsi kuwa Hifadhi kama tuijuavyo leo hii, hivyo kama isingekuwa ni Vita ya Dunia leo hii Tanzania tungekuwa na Makaburu kama AK au Namibia na apartheid pia!

Lkn hakuna kilichobadilika mpaka leo hii Wamsai bado wamepigwa marufuku wao na mifugo yao kukanyaga eneo hilo ingawaje ni mali yao na waliporwa na Muzungu, hakuna jipya tangia mwaka 1904 ambapo walifukuzwa na settler wa Kijerumani na kugeuza eneo sehemu ya kufugia mifugo yake ya kizungu, ...

Bonde la Ngorongoro ambalo lilikuwa ni shamba binafsi la settler wa Kijerumani ambaye alitaka kuleta Makaburu ktk AK kusettle na kulima!

1280px-NgorongoroCrater_Wegmann2012.jpg


Kaburi la Mjerumani Bonde la ngorongoro!

1280px-Grab_von_Michael_und_Bernhard_Grizmek.jpg
 
Back
Top Bottom