Mpango wa kuvunja Jiji la Dar waingia dosari; mvutano kati ya Serikali Kuu na uongozi wa jiji la Dar

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Saturday, 01 October 2011 21:34

Claud Mshana na Fidelis Butahe


MPANGO wa kulivunja Jiji la Dar es Salaam na kuunda majiji matatu
(Metropolitan city), umeingia dosari baada ya kuibuka mvutano kati ya Serikali Kuu na uongozi wa jiji hilo.Jiji la Dar es Salaam lipo katika mpango wa kuvunjwa na kugawanywa ili kuwe na majiji matatu; City Centre, Kigamboni na Bunju. Habari zilizolifikia Mwananchi Jumapili zinaeleza kuwa mpango huo uliokuwa uanze kutekelezwa mwaka huu, utashindikana kutokana na viongozi wa juu serikalini kupingana.

Kwa mujibu wa habari hizo, wapo viongozi wanaoafiki mpango huo wakieleza kuwa utalifanya Jiji la Dar es Salaam kuwa la kisasa na wale wanaoupinga wanaeleza kuwa muundo wa sasa wa jiji hilo, ni wa kihistoria na unapaswa kuenziwa. Hata hivyo, viongozi husika wa jiji la Dar es Salaam na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) wanatupiana mpira kuzungumzia suala hilo la mgongano huo.


Waziri wa Tamisemi, George Mkuchika, jana alisita kuzungumzia suala hilo akieleza kuwa linapaswa kutolewa ufafanuzi na uongozi wa Jiji la Dar es Salaam. “Umesikia (mwandishi), zungumza na uongozi wa jiji hili ni suala lao wenyewe,” alisema Mkuchika na kukata simu. Meya wa Jiji la Dar es Salaama, Didas Masaburi pamoja na mambo mengine, alisema, suala la mfumo mpya wa Jiji la Dar es Salaam, unatakiwa kutolewa ufafanuzi na Serikali Kuu (Tamisemi).

“Hilo ni suala la Serikali Kuu. Ninavyojua mimi Serikali Kuu ndio inatakiwa kulizungumzia suala hilo, sawa? Naomba uwasiliane nao,” alisema Masaburi. Masaburi alikata simu, mara baada ya kutakiwa kueleza mapendekezo ya tume kuhusu mfumo huo mpya wa Jiji la Dar es Salaam.


Hata hivyo, taarifa zilizolifikia gazeti hili zimeeleza kuwa ripoti ya tume iliyoundwa kutazama muundo wa Jiji la Dar es Salaam na kutoa mapendekezo, imebaini upungufu mkubwa wa kiutawala, siasa na mipango.

Ripoti hiyo ambayo Mwanachi Jumapili imefanikiwa kuiona, imeeleza kuwa tume hiyo iliundwa na watu watano chini ya Makatibu Wakuu wa Wizara Wastaafu Deotrephes Mmari (Mwenyekiti) na Rose Lugembe. Wajumbe wengine katika tume hiyo ni Mkuu wa Mkoa Mstaafu, Kanali Nsa Kaisi, Charles Igogo na Habraham Shamumoyo (Katibu wa Kamati).


Kwa mujibu wa ripoti hiyo, baadhi ya upungufu wa kimfumo katika Jiji la Dar es Salaam unaopaswa kurekebishwa ni uwepo wa halmashauri za manispaa tatu ambazo zimeshindwa kufanya kazi kwa ufanisi.

"Kazi zinazofanywa na Halmashauri ya Jiji, ndizo zinazofanywa pia katika manispaa zote tatu hivyo kuwa na mgongano katika utekelezaji wake," imesema ripoti hiyo. Tume imesema mfumo wa Halmashauri ya Jiji unawatenga wakurugenzi wa manispaa kushiriki katika vikao vya madiwani. Hali hiyo ni kinyume na sheria kwa sababu wakurugenzi wa manispaa, ndiyo wanaopaswa kusimamia mapendekezo ya Baraza la Madiwani.

Tatizo lingine lililoanishwa katika taarifa hiyo ni idadi kubwa ya watu wanaoingia Dar es Salaam kila siku. Tume imesema idadi hiyo ni kubwa kuliko uwezo wa miundombinu hivyo kusababisha kuwepo kwa shughuli nyingi zisizo rasmi. “Udhaifu mwingine uko katika mgawanyo wa madaraka. Wakurugenzi wa manispaa hawahusiani na mkurugenzi wa jiji.


Hakuna utaratibu unaoweza kuwakutanisha pamoja kujadili masuala muhimu ya kuboresha huduma za jiji kwa wananchi,” inasema ripoti hiyo. Ripoti hiyo imeeleza kuwa manispaa za za Ilala, Temeka na Kinondoni zimepewa mamlaka ya kupanga na kupitisha bajeti zao na pia kuidhinisha sheria ndogo bila kuhusisha Halmashauri ya Jiji, jambo ambalo pia lina kasoro. Baadhi ya kasoro hizo ni kutokuwapo ushirikiano au makubaliano katika baadhi ya miradi inayotekelezwa na Jiji na manispaa zake.

“Kwa mfano, jiji lilijenga dampo la Pugu Kinyamwezi, lakini halitumiki ipasavyo kwa sababu manispaa hazikukubaliana na mradi huo," inaendelea kueleza ripoti hiyo. "Pia ujenzi wa jengo la Machinga Complex haukupata kuungwa mkono na viongozi wa manispaa ambao walikuwa wakali walipotakiwa kuchangia kwa sababu mradi huo ulikuwa ukisimamiwa na jiji.”

Uchaguzi wa Meya wa Jiji Kwa mujibu wa kifungu cha 20 cha Sheria Namba 8 ya mwaka 1982 ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) na iliyofanyiwa marekebisho mwaka 1999, Meya wa Jiji anapaswa kuchaguliwa na madiwani wa mamlaka ya miji ndani ya mipaka ya halmashauri ya Jiji. Ripoti hiyo inafafanua kuwa mfumo wa kuchagua meya miongoni mwa madiwani waliochaguliwa, una udhaifu mkubwa. Inaeleza kuwa mfumo huo, unalipa Baraza la Madiwani mamlaka yote ya kisheria na kiutendaji ndani ya jiji.

Mapendekezo Baada ya kubaini upungufu huo, Kamati imependekeza kuwe na mfumo mpya utakaokuwa na Jiji Kuu la Dar es Salaam ambalo litakuwa na muundo wake wa kisiasa, sheria na utawala, vitakavyosaidia utendaji mzuri wa shughuli za maendeleo. Mfumo huo mpya unapendekeza kuwe na Baraza Kuu la Jiji chini ya Meya atakayechaguliwa na wananchi wa jiji na meya huyo atakuwa mtendaji.

Chini ya Baraza Kuu la Jiji la Dar es Salaam, kutakuwa na Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na Mameya wengine wawili; Meya wa Halmashauri ya Jiji la Kigamboni na Meya wa Halmashauri ya Jiji la Bunju. Tume hiyo pia imependekeza kuongeza kiwango cha chini cha elimu kwa watu wanaotaka kugombea nafasi za uongozi wa umma, hasa madiwani.


“Hivi sasa vigezo vya elimu vinavyotumika ni kujua kusoma na kuandika na uwezo wa kuongea Kiswahili na Kiingereza tu. Hivyo kamati inapendekeza kiwango cha chini kiwe ni Kidato cha Sita ili madiwani wawe na uwezo wa kusoma, kuelewa na kutathimini bajeti zinazipitishwa.”

Katika kutatua tatizo la wingi wa wahamiaji katika jiji la Dar es Salaam, Kamati imependekeza kuwepo kwa mikakati dhabiti ya kuwawezesha vijana wanaoingia jijini kufanya kazi. Miradi hiyo inapaswa kuanzishwa na kuendelezwa katika majiji yote. “Serikali Kuu na Serikali za Mitaa zinatakiwa kufanya kazi kwa pamoja kuhakikisha kuna mfumo wa kisheria wenye nguvu ili kuhimiza uwazi na wajibikaji.


Kwa sababu kamati imegundua udhaifu mkubwa katika siasa, utawala na sheria kwa watu kushiriki katika shughuli mbalimbali.”

 
Walivunje tu, mie sipendi kabisa lilivyokaa, yaani muundo wake umekaa kaa kama nchi maskini za kiarabu (Yemeni n.k), yaani ovyo kweli!!
 
Hakika yale yale ya zamani,ni sawa na kama wakati watu waliopaswa kutumia tekinolojia ya digital karne hii watu wanashinikiza kubaki kwenye analogy system,ili waendeleze umbumbu wao.Kwa kuligawa jiji ili ingechochea maendeleo ya kikanda katika majiji ndani ya Metropolitan city.Ukiuliza idadi ya washirki wa kupoinga mchakoto huo umri wao ni miaka mingapi si ajabu kusikia wana miaka kuanzia 55-80.

Aibu kubwa kwao wapinga mpango huo mpya ni kipimo cha wizi mkubwa wa kimfumo kwa kujua ujio wa mfumo mpya utachangia mabadiliko ya ulaji uliozoeleka,wa kama kawaida.

Hakika muda utasema atapatikana kionozi mwenye busara na kuusimamia ufanikiwe awa waliopa ni walewale wanywa uji wa mgonjwa.Hawana cha kupoteza kwa zaidi ya kugain kutokana na mfumo uliopo wa kushadadia wizi na mipango ya kifisadi na kuendeleza mifumo ya conservative
 
Hivi mpango wa kuhamishia Makao Makuu ya Nchi mjini Dodoma ndiyo umezikwa kabisa?

Kugawanya MJI (siyo jiji kwa maana halisi ya jiji) wa Dar es Salaam kwenye MIJI mitatu ni uendawazimu!
 
nadharia hiyo wakiitia vitendoni watazua mgogoro mkubwa kuliko wanaouona sasa. naona kuna msukumo wa kisiasa zaidi kuliko kitaaluma. ukitaka kugundua hilo angalia wajumbe wa kamati inayotajwa, tutenganishe siasa na taaluma hili ndilo tatizo la tanzania achilia mbali dar-es-salaam.
 
Tume iliyotumika haiwezi kuja na mambo ya kitalam maana imejaa wanasiasa tu. Wataalam wa mipango miji mbona hawakuwepo kwenye tume. Hapa kuna mvutano wa kisiasa zaidi. Na sasahivi wanapoona wapinzani wamekaa mkao wa kula wanapata wasiwasi ni muundo gani utawasaidia wao waendeleze mambo yao.

Imefika wakati watu hata hawpendi kitu chochote kinachofanywa na utawala huu hata kama ni kizuri kwa sababu kila kitu kinatawaliwa na kutengeneza mfumo wa kutoleta mabadiliko.

Tuwaache waboronge tutatengeneza watakapokuwa wameondoka. Inatia aibu sana kwa kuwa na jiji lenye muundo unaokanyagana kama huu wa dar.
 
CCM na ajira mpya 5000.... ubunifu haupo inabaki kuunda Wilaya na mikoa mipya na sasa kugawanya jiji... Ujinga mtupu!
 
Back
Top Bottom