Mpango wa kura ya maoni katika 'Mzalendo' wazimwa na CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mpango wa kura ya maoni katika 'Mzalendo' wazimwa na CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Oct 4, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Oct 4, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  He, hii kali nimeipata leo! Swahiba wangu aliye katika gazeti dada la Uhuru – Mzalendo la kila wiki, kanieleza kuwa kulikuwa na mpango, takriban wiki mbili zilizopita, wa kuanzisha kura ya maoni kuhusu wagombea wa urais ambayo ingeendeshwa katika mtandao wa gazeti hilo. Kila kitu tayari kilikuwa kimeandaliwa.

  Nasikia mpango huo ulikatazwa na wakubwa wa chama hicho pale baadhi ya wafanyakazi wa hilo gazet walipovujisha habari hizo kwa wakubwa hao.

  Hofu yao ni ile ile – kwamba Dr slaa angeongoza katika kura hiyo. Habari zinasema kutokea hapo ndipo serikali ikaja na wazo la kutaka kudhibiti kura za maoni zinazofanyika nchini.
   
 2. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #2
  Oct 4, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Na bado
   
 3. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #3
  Oct 4, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,461
  Likes Received: 5,846
  Trophy Points: 280
  Matokeo yashapikwa tayari kuwa JK ashinde by %85(%5 zaidi ya 2005) na Lipumba awe wa pili.....sasa vichwa vinawauma ndio maana wanaanza kumwambia Dr Slaa akubali matokeo leo hii wakati uchaguzi bado....Kiravu anasubiri tu kuyasoma...hii midahalo na opinion polls wanogopa ziteendelea kumwonyesha Slaa juu zaidi....
   
 4. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #4
  Oct 4, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Lipumba awe wa pili? Kwa mikoa ya Lindi na Mtwara tu? Nahofia kwamba mwaka huu NEC imepanga kuleta vurugu kubwa hapa nchini haijiwahi kutokea. Waachane na mpango huo unaosukwa na akina RA na Makamba.
   
 5. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #5
  Oct 4, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Hi strategy yao ya kuwapa kazi ya kusambaza vifaa vya uchaguzi kutumia JESHI, in walakini!!!

  Yetu macho.:A S 13:
   
 6. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #6
  Oct 4, 2010
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Uhamisishaji uendelee mpaka siku yenyewe ya kura...
  Mabadiliko muhimu sasa...
   
 7. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #7
  Oct 4, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  duuu hapo sasa ndo pagumu hata kama ataiba na kuingia madarakani ajue wananchi hawakumpa ridhaa yao, ila jk hawezi kukubali chama kimfie yeye kwa njia yeyote ile!
   
 8. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #8
  Oct 4, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 417,680
  Trophy Points: 280
  Majibu wanayajua ila ushauri wangu kwa watumishi wa UHURU na Mzalendo anzeni kutafua kazi maana hilo gazeti litakufa kifo cha kibiashara baada ya Dr. Slaa na Chadema kukamata Ikulu.
   
Loading...