Mpango wa kum-'demonise' Magufuli umeshindwa bila hata ya kuanza, watu wanazidi kumpenda

kmbwembwe

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
10,412
7,197
Nchi za kibeberu na vibaraka wao wana tabia ya kuwazushia viongozi wanamapinduzi ubaya waonekane wabaya kama shetani.

Walipofanikiwa kumpindua Kwame Nkurumah wa Ghana walimzushia uongo mwingi hadi ikawa kisiasa ghana huwezi kufanikiwa kwa kuunga mkono siasa na sera za Nkrumah. Kutokana na propaganda za magharibi ikawa kama aibu mtu kuunga mkuno sera za ukombozi afrika na uchumi wa kijamaa. Waghana hadi leo hawampi nkurumah anayeheshimika Afrika nzima heshima anayostahili. Uwanja wa ndege wa kimataifa accra hadi leo unabeba jina la kotoko mtu aliyempindua Nkrumah.

Hata nchini guenea ni hivi karibuni tu kumeanza wimbi kuwaelimisha vijana na taifa Sekou Toure alikua kiongozi wa namna gani kwa waguenea na Afrika. Huyu naye alikua mwanamapinduzi ila ubeberu wamemchafua ili waguenea wasifuate mawazo yake.

Kwa nchi yetu ni tofauti kutokana na umoja na mwamko mzuri wa kisiasa wa wananchi. Licha ya kazi kubwa ya wapinga maendeleo wakiongozwa na ubeberu wameshindwa kumchafua Nyerere. Watanzania wanamkumbuka na kutaka dira yake ifuatwe. Hakuna mwanasiasa anaweza kufanikiwa tanzania kwa kumchafua Nyerere.

Tuliona baadhi ya viongozi wa Chadema wakitumika kuchafua jina na heshima ya nyerere hadi bungeni mmojawapo akiwa antipass lissu. Baada ya kuona wanajichafua kwa kujaribu kumchafua Nyerere wakageuza mbinu. Sasa wanajidai kumnukuu kila wakati nyerere ila kwa kupotosha kauli zake.

Magufuli amelinganishwa na nyerere kwa kutetea kwa nguvu maslahi ya umma kwenye uongozi wake. Tangu aitwe na mola wake tumeshuhudia furaha kwa wapinga maendeleo. Wamediriki hadi kumsifia mama kama mwokozi wa taifa dhidi ya uongozi uliyopita wa Magufuli. Juzi tu tumemsikia askofu mmoja akimtaka mama kutibu majeraha taifa.

Wanamapinduzi tunajua wenye majeraha ya magufuli ni fisadi na wazembe. Wale waliyojaribu kuiba mali au mashirika ya umma, wale waliyokua wamejimilikisha kinyemela mali za chama chao cha CCM, wale waliyokua wanashirikiana na barrick kuona madini ya nchi yanaibiwa makontena na makontena kwa kupewa ujira.

Sasa anatokea askofu eti mama ponya majeraha. Majeraha ya fisadi. Ina maana awarejeshe kwenye kudhulumu umma.
Tunamtahadharisha mama awe macho kukumbatiwa na watu waovu ambao wanategemea kuibia umma na kujitajirisha binafsi huku umma wa wananchi ukiendelea kufukarika.

Ni jambo la kutia moyo kuona jinsi wananchi wa tanzania wanavyomkumbuka magufuli. Ni hatari kwa kiongozi yeyote kutaka kufuata sera za kuwanufaisha wachache kwa gharama ya umma. Kimsingi CCM ni chama cha kulinda na kuendeleza maslahi ya umma. Wakifanya tofauti watapigwa chini.
 
Ghana ingeendelea kutawaliwa na Nkurumah ingekuwa nchi ya hovyo mpaka leo. Ghana imepiga hatua kubwa sana kimaendeleo na demokrasia tangu kuondolewa kwa huyu dikteta uchwara aliyekuwa analazimisha ujamaa uchwara.
 
Huna lolote wewe. Kwanza uandishi wako wa drs la tatu. Majina & nchi ya watu kwa herufi ndogo ?!!. Rudi kwanza MEMKWA

Pili huyu unaemtukuza alikuwa na mapungufu kibao, japo pia kuna kazi amezifanya . So muache Rais wa sasa afanye kazi zake kwa kipaji chake , na ueledi wake. Usimlazimishe kuishi kwenye kivuli cha aliyepita, ambaye ni failure wa haki za binadaamu na asiyefuata katiba.
 
Mjinga tu kwani hapa tunafundishana kuweka paragraph na vituo? Naona hoja ndio inakufanya kuhamaki. Tulia jibu hoja sio kuonesha ujinga.
 
Mjinga tu kwani hapa tunafundishana kuweka paragraph na vituo? Naona hoja ndio inakufanya kuhamaki. Tulia jibu hoja sio kuonesha ujinga.
Mimi sijakuita "mjinga" bali wewe umekimbilia kuita wachangiaji wajinga.

Uandishi wako uliobeba hoja ni aibu kwa walimu wako. Labda shule za kata nisikuonee bure . Magu ameshamaliza mwendo acha wengine waishi kivyao
 
images - 2021-10-11T224009.360.jpeg
 
Mimi sijakuita "mjinga" bali wewe umekimbilia kuita wachangiaji wajinga.

Uandishi wako uliobeba hoja ni aibu kwa walimu wako. Labda shule za kata nisikuonee bure . Magu ameshamaliza mwendo acha wengine waishi kivyao
Hujatoa hoja yoyote ya maana kuhusu kile nilichoandika. Sijui wewe ni mwalimu maana umeanza kusahihisha uandishi badala ya kuangalia ujumbe.

Hujui hata elimu yangu unanidharau..ila naona umekasirishwa na kile nilichoandika hadi unapoteza ufahamu. Huku kwenye mitandao hatufanyi mtihani wa uandishi. Lengo kuu ni kufikisha ujumbe.
 
Back
Top Bottom